realMamy
JF-Expert Member
- Apr 28, 2024
- 7,450
- 19,184
Kuna Dini zenye Ibada zaidi ya Moja Ili kuhakikisha Kila mtu anapata nafasi ya kupata mawili matatu kutoka kwenye neno la Mungu.
Mojawapo ya maana ya Neno Ibada ni kumheshimu, kumshukuru, na kumuabudu Mungu kwa moyo, kwa vitendo, na kwa kweli.
Ibada ya kweli inajumuisha: sala, sifa, shukrani, mafundisho, sadaka, na utii.
Tunaweza kumuabudu Mungu Msikitini au Kanisani.
UMUHIMU WA KUHUDHURIA NYUMBA ZA IBADA.
1. Kujengeka Kiroho
Ukipata neno, unapata mwelekeo.
2. Umoja na Familia ya Imani
Peke yako unaweza kuchoka lakini kwenye wengi tunaimba, tunaomba, na kunasaidiana. _Waebrania 10:25.
3. Ulinzi na Mwelekeo
Nyumba ya Ibada ni shule ya maisha. Unafundishwa jinsi ya kushinda majaribu, ndoa, kazi, na maisha kwa ujumla.
4. Kumtolea Mungu Heshima Yetu.
Mungu anastahili muda wetu.
5. Baraka na Nidhamu
Utaratibu wa kuhudhuria unakufundisha nidhamu. Na Mungu anabariki utii na uaminifu katika mambo madogo.
TUONGEE:
Ni kitu gani kinakuzuia wewe?
- Muda?
- Kazi?
- Majeraha?
- Kuchoka?