Je, unaamini kuwa uchawi upo?

Je, unaamini kuwa uchawi upo?

Uchawi upo nakumbuka miaka mitatu iliyopita niko na wenzangu yapata saa 9 usiku tunatoka Harusini, Njiani tulikutana na kikundi cha wachawi wake kwa waume, wakifanya yako wakiwa watupu , tulipofika eneo lile kuna mwenzetu mmoja akaaza na yeye kupandisha mashetani wachawi walitoka mbio sana, ila mambo haya yanatisha sana.
Kweli mkuu uchawi Upo nashangaa baadhi yetu wanabisha kabisa kanakwamba hawaishi Tz

critical thinker
 
Njoo kusini kuna kijiji kimoja kinaitwa Ngende , Walimu wanakimbia mpaka shule kisa uchawi.
Mkuu ngende masasi au?hakuna makanisa ya kilokole?

Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app
 
Nataka nine kufungua kanisa hapo

Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app
 
Habari zenu...
Note:Kuamini kwako au kutokuamini kwako hakufanyi kitu kisiwepo.
Ni hivi ilikuwa siku ya jumamosi nikitoka katika mizunguko yangu ya kusaka maisha pande za Songea nikirudi dar kwa kutumia usafiri wa basi[Superfellow].

Ila tulipofika Kijiji kimoja kinaitwa kiwalala tulikutana na maajabu ya dunia.Tulipofika kiwalala tulikuta watu wengi sana wamezagaa maeneo ya barabara hivyo tulishindwa kuendelea na safari gari likasimama.Baada ya kudadisi kumbe kulikuwa na mkasa wa mambo ya uchawi mambo yalikuwa hivi~

Kuna bibi mmoja aliwapa kibarua mabinti wawili shambani kwake kazi ya kulima shamba lake.Wale mabinti walipofika shambani wakaanza kulima ghafla akatokea nyoka yule binti mmoja akamuuwa,baada ya kumuuwa wakaendelea kulima kabla hawajafika mbali akaja nyoka mwingine baada ya kuja nyoka wa pili akaja na yule bibi mwenye shamba.

Alipofika yule Bibi akamwambia yule binti aliyeuwa nyoka wa kwanza kama unaweza muuwe na nyoka huyu.Wale mabinti wakaanza Kuogopa wakashindwa kumuuwa yule nyoka mwingine.Kuanzia hapo Bibi akaanza kudai nyoka wake yule wa awali/kwanza aliyeuliwa.

Bibi akawa anawadai yule nyoka aliyeuliwa awali na wale mabinti,mabinti wakawa wanalia tu wanashindwa kumpa yule bibi nyoka wake.Ile kesi ilifika hadi serikali ya kijiji lakini cha ajabu yule bibi hakusita kudai nyoka wake.Kesi iligusa wananchi wengi wa maeneo ya kiwalala na viunga vyake.

kwanini bibi alidai nyoka ambaye ameshakufa?
Swali hili lilizunguka katika kichwa changu,ndipo nilipoanza kufanya udadisi kwa wananchi waliko pale.

Kumbe nyoka yule alikuwa ana matumizi mbalimbali katika ulimwengu wa giza.Nyoka aliyeuliwa alikuwa anamiliki vijiji 15 katika maeneo hayo alitumiwa kuuwa watu na kuiba vitu mbalimbali kama vile pesa,Kuku n.k.Pia nyoka huyo alikuwa anakodishwa kwa watu Kwa ajili ya matumizi mbali mbali yaani yule Bibi alikuwa anaishi kwa kutegemea yule nyoka.

Nyoka huyo ni wakawaida kama walivyo nyoka wengine?
Cha kushangaza kumbe yule nyoka hakuwa nyoka kama nyoka wakawaida bali alikuwa ni mtoto wa yule bibi alimfanya msukule kwa kumgeuza nyoka.Serikali ya kijiji ilishindwa kuamuwa kesi hiyo na kuamuru kesi ifike mahakamani.

Alafu kesi hii unaambiwa sio ya kwanza katika kijiji hiki kumewahi kutokea kwa kesi za namna hii nyingi sana hapo kiwalala.Kwa tukio hili nimeamini uchawi Upo.
Nawasilisha kwenu...

critical thinker

Hapo kiwalala hapana makanisa mkuuu?has a ya kilokoleeee,,kama VP niunganishe niende fungus kanisa hapo

Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app
 
Kuna Ngende mbili moja masasi, nyingine Newala zote hatari mpaka makanisa yanafungwa. Watoto wadogo wachawii hatari
At u sure mkuuu,,?

Sent from my TECNO W5 Lite using JamiiForums mobile app
 
Kama unaishi mjini tu huwezi jua jaribu kuzunguka maeneo mbalimbali mkuu,uchawi Upo kabisa nimeprove kwa macho yangu

critical thinker
hapana hata maeneo ambayo nimeish yanatokea mambo ambayo watu hushikana uchawi,ila katika misingi wanayoelezea ndipo napata shida kukubali au kuelewa kwamba huo,uchawi uko vp?
hivi mfano mtu kaumwa ama kaugua halafu,huyo mtu anasema kuna mtu kamroga,nawaza inakuwa vp au huo ugonjwa unakuwa vp na ubongo au moyo unapataje hayo maradhi bila kuguswa au kwa imani kama hiyo?
 
Chief, umeshuhudia hao wanakijiji walichokueleza. Nani alimmilikisha Nyoka hivyo vijiji? Huyo Nyoka alikufaje "kizembe" kama ana power za ajabu? Hizi ni imani tu.
kwanza mkuu yule nyoka aliyeuliwa na mtu wake akafa mbna alikufa kizembe zaidi ya huyo
 
Nyoka za songea hzo hazijawahi kuwaacha watu salama
Hii scenario ya pili kuacha ile ya yule mzee aliyebeba nyoka kwenye boksi
Inaonekana songea wanatumia sana nyoka
Kiwalala iko Lindi haiko songea

Sent from my Halotel H8401 using JamiiForums mobile app
 
Njooni sumbawanga,kutembea tuu.halafu mseme kwenu kuna uchawi.

Sent from my TECNO-N6 using JamiiForums mobile app
 
Hivi ni kweli ehee ? Asee umenikumbusha story za uchawi tukiwa bwenini acha tu vilikua vinatisha kweli.
 
Habari zenu...
Note:Kuamini kwako au kutokuamini kwako hakufanyi kitu kisiwepo.
Ni hivi ilikuwa siku ya jumamosi nikitoka katika mizunguko yangu ya kusaka maisha pande za Songea nikirudi dar kwa kutumia usafiri wa basi[Superfellow].

Ila tulipofika Kijiji kimoja kinaitwa kiwalala tulikutana na maajabu ya dunia.Tulipofika kiwalala tulikuta watu wengi sana wamezagaa maeneo ya barabara hivyo tulishindwa kuendelea na safari gari likasimama.Baada ya kudadisi kumbe kulikuwa na mkasa wa mambo ya uchawi mambo yalikuwa hivi~

Kuna bibi mmoja aliwapa kibarua mabinti wawili shambani kwake kazi ya kulima shamba lake.Wale mabinti walipofika shambani wakaanza kulima ghafla akatokea nyoka yule binti mmoja akamuuwa,baada ya kumuuwa wakaendelea kulima kabla hawajafika mbali akaja nyoka mwingine baada ya kuja nyoka wa pili akaja na yule bibi mwenye shamba.

Alipofika yule Bibi akamwambia yule binti aliyeuwa nyoka wa kwanza kama unaweza muuwe na nyoka huyu.Wale mabinti wakaanza Kuogopa wakashindwa kumuuwa yule nyoka mwingine.Kuanzia hapo Bibi akaanza kudai nyoka wake yule wa awali/kwanza aliyeuliwa.

Bibi akawa anawadai yule nyoka aliyeuliwa awali na wale mabinti,mabinti wakawa wanalia tu wanashindwa kumpa yule bibi nyoka wake.Ile kesi ilifika hadi serikali ya kijiji lakini cha ajabu yule bibi hakusita kudai nyoka wake.Kesi iligusa wananchi wengi wa maeneo ya kiwalala na viunga vyake.

kwanini bibi alidai nyoka ambaye ameshakufa?
Swali hili lilizunguka katika kichwa changu,ndipo nilipoanza kufanya udadisi kwa wananchi waliko pale.

Kumbe nyoka yule alikuwa ana matumizi mbalimbali katika ulimwengu wa giza.Nyoka aliyeuliwa alikuwa anamiliki vijiji 15 katika maeneo hayo alitumiwa kuuwa watu na kuiba vitu mbalimbali kama vile pesa,Kuku n.k.Pia nyoka huyo alikuwa anakodishwa kwa watu Kwa ajili ya matumizi mbali mbali yaani yule Bibi alikuwa anaishi kwa kutegemea yule nyoka.

Nyoka huyo ni wakawaida kama walivyo nyoka wengine?
Cha kushangaza kumbe yule nyoka hakuwa nyoka kama nyoka wakawaida bali alikuwa ni mtoto wa yule bibi alimfanya msukule kwa kumgeuza nyoka.Serikali ya kijiji ilishindwa kuamuwa kesi hiyo na kuamuru kesi ifike mahakamani.

Alafu kesi hii unaambiwa sio ya kwanza katika kijiji hiki kumewahi kutokea kwa kesi za namna hii nyingi sana hapo kiwalala.Kwa tukio hili nimeamini uchawi Upo.
Nawasilisha kwenu...

critical thinker
Nyoka ni kiumbe tu ambaye binadamu mwenye akili anaweza kum control.

Sisi Wasukuma tunawachukua nyoka na kucheza nao ngoma, ni sehemuya mila na desturi.

Katika dini za asili za Afrika, tulifundishwa kuishi vizuri na mazingira, jinsi gani ya kuishi sehemu yenye nyoka wengi na kuwaacha hawa nyoka waishi kivyao na sisi tuishi kivyetu bila kudhuriana, ndiyo maana wazee wengine wakikuona unataka kumuua nyoka ambaye anajipitia zake wanakukataza, kwa sababu yule naye ni kiumbe anapenda kuishi na hataki kufa kama wewe.

Sasa, kuna koo zilizama sana katika mafundisho hayo mpaka kufikia uwezo wa kuwasiliana na wale nyoka na kuweza kukaa nao na kuweza kuwatumia katika kazi zao.

Huu si uchawi. Ni sayansi tu, kama wewe unavyoweza kukaa na mbwa ukamfuga na kumfundisha jinsi ya kucheza nawe.

Kibaya ni kwamba sanaa hii ya zamani imekufa baada ya watu weupe kuja kwetu na kutuambia kwamba utamaduni wetu ni ushenzi.

Wametuambia nyokani shetani.

Sasa wakitokea watu wachache wanaojua sanaa hizi kwakuwa wamerithishwa kwao, wanaitwa wachawi.

Hiyo habari yako haina kitu chochote kinachothibitisha kwamba uchawi upo hata kama hayo yote uliyosema yametokea.

Tatizo ukishaamini uchawi,hata jambo la kawaida, au lisilo la kawaida ambalo halijajulikana vizuri likitokea, badalaya kufanya uchunguzi wa kutosha ujue nini kimetokea,unakimbilia kutoa jibu la haraka la uchawi.
 
Njooni sumbawanga,kutembea tuu.halafu mseme kwenu kuna uchawi.

Sent from my TECNO-N6 using JamiiForums mobile app
Nasikia wafipa ni wachawi balaa ila sasa mbona mkoa wenu maskini mkuu ? Bora uchawi wa mbesa/pesa ndio dili uchawi wa mwenzako unamfanyia fitna mngeacha looh dunia imebadilika
 
Kule Sumbawanga kuna wazee wanahamisha nyumba za wenzao kishirikina..yaani unaamka asubuhi uko sehemu tofauti lakini nyumba ileile..hii sio chai,its true..
 
Back
Top Bottom