Je, unadhani ni sahihi viongozi kutenguliwa baada ya kusema 'siri' za serikali? Au wangepewa fursa ya kutengua kauli?

Je, unadhani ni sahihi viongozi kutenguliwa baada ya kusema 'siri' za serikali? Au wangepewa fursa ya kutengua kauli?

Mjadala uendelee. Mada hiyo hapo mezani. Nitakuwa wa mwisho kutoa maoni yangu. Karibuni wana jukwaa.

Rejea utenguzi wa mhe. Nape, Ndugai, Dc wa longido nk.
Inabdi watenguliwe na wakafunguliwe mashtaka serikali iwakane kuwa wakiyatenda wenyewe peke yao kwa mapenzi yao. Iwe sawa na special mission za kijeshi ambapo ukikamatwa nchi inakukana
 
Mjadala uendelee. Mada hiyo hapo mezani. Nitakuwa wa mwisho kutoa maoni yangu. Karibuni wana jukwaa.

Rejea utenguzi wa mhe. Nape, Ndugai, Dc wa longido nk.
Siri? Wizi wa kura kumbe ndo siri za serikali? Sikuwa najua hilo....
 
Siri? Wizi wa kura kumbe ndo siri za serikali? Sikuwa najua hilo....
Siri ni jambo lolote lisilojulikana kwa wengi au kwa wasiohusika. Na ndio maana kuna siri kuu, siri ya muda fulani na siri sana!
 
Siri ni jambo lolote lisilojulikana kwa wengi au kwa wasiohusika. Na ndio maana kuna siri kuu, siri ya muda fulani na siri sana!
Kama alichoongea DC ni sahihi, je, ni jinai au sio jinai? Kama ni jinai, ina sifa ya kuwa siri?
 
Kwamba kuiba kura au watu kupita bila kupingwa nayo ipo katika kundi la siri?.

Location : Kihonda kanisani
 
Mjadala uendelee. Mada hiyo hapo mezani. Nitakuwa wa mwisho kutoa maoni yangu. Karibuni wana jukwaa.

Rejea utenguzi wa mhe. Nape, Ndugai, Dc wa longido nk.

Pia soma:Kuelekea 2025 - DC wa Longido aliyesema alihusika kutengeneza mazingira ya Madiwani kushinda 2020 atenguliwa
Unyumbu ni tabia ya wanao pewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza ama kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga kwa viongozi wao, human herding is an occurrence of entrusted people suspending their individual reasoning because of flattering, working towards group objectives for person gains and fear of their leaders
 
Siri sio kwenye maovu..viongozi wote wanakula kiapo cha kutetea katiba, kulinda amani na usalama wa wananchi na kuleta maendeleo.Siri zote halali na zenye maslahi kwa taifa zinapaswa zijikite hapo. Siri za kuumiza wananchi kama huyo DC alivyoongea namna demokrasia haipo...hiyo sio siri ni kuficha maovu, ni kusubbotage katiba, ni kussubotage wananchi...HIZO WAZISEME KWA MASLAHI YA WANANCHI.
Maovu hayavumiliki ndo maana kuna - whistleblowers...kama huyo aliyesambaza hiyo clip..angeweza naye kukaa kimya sababu et ya SIRI
 
Hicho kinachoitwa "siri za serikali" ni mipango ya kihalifu ya serikali dhidi ya wananchi na taifa.
 
Back
Top Bottom