Umeeleweka,ila hapo katika habari za chumvi kidogo...panayumba.Kama mambo yangekuwa rahisi hivyo wale ma "beach boys" wangekuwa pazuri maana wale bahari yao kama samaki.Ila naamini mafanikio yanakuja kwa "calibrated efforts 100%".Tatizo wengi efforts zetu hazina mahesabu tunakomaa sana output inakuwa chini.Sasa hayo ya chumvi tutayamaliza kisha tuanze kutegemea "luck".Tuongezee tufanye nini pia ili mambo yaende.Sio kuoga machumvi ya mawe kisha tunaenda katika interview au mishe yoyote bila kuwa equiped in terms of skills and competence.
Pia naamini mafanikio ya bahati bahati huwa yanakuwa ya mashaka na wakati wowote anguko linaweza kutokea
Inashauriwa ufanye visualization na affirmations ya nini unataka na uicommand subconcious mind kupokea na kuifanya kuwa need yako. Ukiweza hili then Subconscious mind inajua lugha ya kuongea na universe (call it nature, God, Allah, Buddha, whatever kwa imani yako) then universe itakuletea solutions. Chumvi inatoa negative energies (call it mapepo) kusaidia kufocus kuziconcentrante positive energies. Kuna uzi wa Mayalla nafikiri unaongelea nguvu ya kutenda miujiza ambayo kila binadamu anayo na anaitumia bila kujua sometimes una sehemu kubwa pia ya huu mjadala.
Kwenye kitabu ya cha Napoleon Hill Think and grow rich kuna point anaongelea kitu kinaitwa autosuggestion hii inatokea ndani (kwa kufikiria mwenyewe) au nje (kwa kusikiliza suggestions za watu) yani ni limiting power ambayo inakwamisha watu wengi sana na kuua sn vipaji. Subconscious mind inapokea kila unachokiwaza, kukiona, kukitaka, na unachoambiwa au kusikia kwa watu na kukikubali etc kwa mfano unajisemea mwenyewe "siwezi" au mtu anasema huwezi na wewe unakubaliana naye.
Autosuggestion ni km unasema nataka mwaka huu nipate pesa ya kujenga nyumba na kufanya affirmation (wengine wanaita kunuia) zako then unaanza kujiwekea negativitiy mwenyewe km kusema "lkn ntapata kweli pesa"? Ukianza kujiuliza mwenyewe wakati umeweka lengo mwenyewe unaiconfuse nature inashindwa kujua ikupe nini, unachotaka au yale mashaka yako (bahati mbaya sn nature inatoa negative kiurahisi zaidi kunapokuwa na mixed feelings so unakosa unachotaka au unapata kidgo).
Wana maombi na watu wa kiroho wanaposema wakikuombea amini umepona, ni kwamba wanataka ufanye affirmation na visualization kwamba umepata tayari unachotamka then nature inachukua mkondo wake. Hamna mtu anaponya Bali nia na matakwa yako yanapokuwa strong enough. Hata Yesu alisema imani yako imekuponya au nataka takasika hamna mahali alisema amekuponya!
Ukisema napata kazi mwezi huu usirudi tena kuanza kutilia mashaka imani yako mwenyewe. Amini, komaa na chukua hatua, utaona matokeo! Kuna video nyingi sana YouTube za visualization na affirmations zina maelezo mengi mazuri na wengi wanafanikiwa sana kwa njia hii tu. Actually wakubwa kama kina Gates, Steve Jobs, Branson, na matajiri wengine huwa wanafanya visualization ya nini wanataka, wanatengeneza michoro, ideas, concepts, rRamani,picha nk then wanacommand inaingia kwenye subconscious mind halafu njia za kuumba zinaletwa na universe, zinaletwaje ni topic ingine kubwa, ndo maana unakuta mtu mwenye ndoto anaweza kuiimba na kuieleza in details hata kabla haijatokea physically bado. Ukimuuliza mtu anayevisualize kuitengeneza mashine utashangaa anavyoileza km vile tayari ailishaiunda.
Sijui km nimerukaruka bila kumaliza points au naeleweka. Humbly...