Je, unaijua "Biblia" ya Shetani? Pita hapa nikujuze!

Setfree

JF-Expert Member
Joined
Dec 25, 2024
Posts
6,238
Reaction score
8,194
Katika siku hizi za mwisho, wapinga Kristo wameanza kutumia njia mbalimbali kuwapotosha waumini wa kweli. Mojawapo ya njia hizo ni kuzalisha Biblia potofu au tafsiri potofu za Biblia.

Kama huna habari kuna kitabu kinaitwa "The Satanic Bible" (Biblia ya Shetani), kilichoandikwa na Anton LaVey. Hii sio Biblia ya ki-Mungu bali ni kitabu kinachotukuza uasi, ubinafsi, na ibada za kishetani. Na wala sio tafsiri ya Biblia, bali ni maandiko ya kidini ya dhehebu la kishetani (Church of Satan).

Lakini pia yapo matoleo ya Biblia ambayo, japo yanadai kuwa ni tafsiri halali za kibiblia, yamehaririwa kwa makusudi ili kupotosha mafundisho ya msingi ya Kikristo. Tafsiri hizo huondoa au kubadilisha maandiko ya awali kuhusu Uungu wa Kristo, wokovu kwa neema, hukumu ya dhambi nk. Tuwe macho, hizi ni nyakati za mwisho.
1 Tim 4:1-5
"Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani.."

Hivyo, usiamini kila toleo jipya la Biblia bila kuelewa chanzo chake. Kwa wazungumzaji wa Kiswahili, nashauri wasome tafsiri ya kuaminika iitwayo: Biblia ya Kiswahili ya Union Version (SUV). Biblia hiyo imetafsiriwa kwa uaminifu mkubwa kwa kuzingatia lugha za awali za Biblia — yaani Kiebrania (kwa Agano la Kale) na Kigiriki (kwa Agano Jipya).

Kuna tafsiri mpya ya Kiswahili, imebadili kile kifungu: "Isipokuwa kwa sababu ya uasherati," wameandika: "Isipokuwa kwa sababu ya uzinzi." Uasherati na uzinzi ni maneno mawili tofauti. Mtu anaruhusiwa kumwacha mkewe kwa sababu ya uasherati tu, sio uzinzi.

Kwa wapenzi wa lugha ya Kiingereza tafuta Biblia ya King James(KJV). Ukiona kiingereza chake ni kigumu, tafuta toleo lake jipya(NKJV).

Tafsiri hizo pia zimezingatia lugha za awali.
 
Jinsi ya kutambua Biblia au tafsiri potofu:
  • Inapinga au kupunguza Uungu wa Yesu Kristo (Yohana 1:1, Kol. 2:9).
  • Inaondoa maneno muhimu kama “damu ya Yesu,” “toba,” au “msalaba.”
  • Inachanganya mafundisho ya Biblia na falsafa za kidunia au mapepo (1 Timotheo 4:1).
Na wanaozisambaza tafsiri hizo potofu za Biblia ni watu wanaoishi maisha yanayopingana na Neno la Mungu.
 
1 Yoh 2:18-23
"Watoto, ni wakati wa mwisho; na kama vile mlivyosikia kwamba mpinga Kristo yuaja, hata sasa wapinga Kristo wengi wamekwisha kuwapo. Kwa sababu hiyo twajua ya kuwa ni wakati wa mwisho. Walitoka kwetu, lakini hawakuwa wa kwetu. Maana kama wangalikuwa wa kwetu, wangalikaa pamoja nasi. Lakini walitoka ili wafunuliwe kwamba si wote walio wa kwetu. Nanyi mmepakwa mafuta na Yeye aliye Mtakatifu nanyi mnajua nyote. Sikuwaandikia ninyi kwa sababu hamwijui iliyo kweli, bali kwa sababu mwaijua, tena kwamba hapana uongo wo wote utokao katika hiyo kweli. Ni nani aliye mwongo ila yeye akanaye ya kuwa Yesu ni Kristo? Huyo ndiye mpinga Kristo, yeye amkanaye Baba na Mwana. Kila amkanaye Mwana, hanaye Baba; amkiriye Mwana anaye Baba pia."
 
Kumbuka Biblia ni kutabu cha historia kumuhusu Mungu. Inamaana huwezi kumjua Mungu leo pasipo kuijua historia yake kupitia Kitabu kinachoitwa Biblia.

Biblia ndani yake inashangaza maana inakupa maana zaidi ya unavyohisi kuvijua.

Kumbuka; Shetani ni sehemu ya Historia ya Mungu. Mungu unapojifunza kumuhusu ni lazima akupe na simulizi ya Shetani. Shetani hana historia nje na Biblia ya Mungu isipokuwa yeye anajipambanua ndani humo humo na uzuri Biblia imezungumza na mwisho wake utakavyokuwa.
 
Itapendeza kama ukiweka hapa bible ya Shetani nisome
Aisee! Uwe makini ndugu, usije ukapotoshwa. Wanaiita Biblia lakini kiukweli sio Biblia. Imejaa tu vifungu vya maneno ya uasi, kiburi, majivuno, uongo na maneno yaliyo kinyume na mapenzi ya Mungu.
 
Uasherati na uzinzi ni maneno mawili tofauti. Mtu anaruhusiwa kumwacha mkewe kwa sababu ya uasherati tu, sio uzinzi.
Hahaha leo ndio nimegundua wewe kweli kwenye maandiko ni mweupe kabisa, yaan hapa umekosea pakubwa sana sana saaaaana nitakufafanulia ila ulichoandika sio kweli ni uongo mtu anatakiwa kumuacha mke mzinzi ndio maana imeandikwa usizini sio usifanye uasherati
 
We kweli ni zerominus10 😀
Kama ulimwacha mke wako wa kwanza kwa sababu ya uzinzi ukaoa mwingine, basi umepotea. Mrudie fasta mke wa kwanza, vinginevyo unahesabika mzinzi. Uko tayari nianze kukupatia nondo za ukweli huo?
 
Na mimi nondo ninazo wala sihitaji nondo kutoka kwako mkuu, uzinzi upo ndani ya uasherati
 
zerominus10 ingawa umekataa kwamba hutaki nondo zangu, mimi nakupa tu ili kuitetea hoja yangu ile. Naomba usome kisha na wewe unipe nondo zako. You never know, labda za kwako zimeenda shule zaidi. Niko tyari kujifunza.

Mimi naamini hivi:

Mtu anaruhusiwa kumwacha mkewe kwa sababu ya uasherati tu. Biblia ya SUV inasema hivi katika Mathayo 5:32
"lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini.”

Neno la Kigiriki lililotumika hapo kwenye uasherati ni “porneia” – sio “moicheia” (uzinzi). Kwa hiyo sio sahihi kusema 'kwa sababu ya uzinzi'

Andiko hilo la Mt 5, linafafanuliwa vizuri na habari ya Yusufu na Mariamu katika Mathayo 1:18-19. Chunguza vizuri habari hiyo utaona kuwa walikuwa wachumba, ingawa Yusufu aliitwa “mumewe”
"...Mariamu mama yake alipokuwa ameposwa na Yusufu, kabla hawajakaribiana, alionekana ana mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. Naye Yusufu, mumewe, kwa vile alivyokuwa mtu wa haki, asitake kumwaibisha, aliazimu kumwacha kwa siri.”

Baadaye Malaika akamwambia Yusufu asimwache Mariamu “mkewe.” Hivyo hao waliitwa mume na mke kwa desturi za kiyahudi lakini walikuwa bado hawajaanza kuishi pamoja kikamilifu. Katika hali hiyo Yusufu alikuwa na haki ya kumwacha Mariamu kama angebaini amefanya “porneia” – uasherati.

Huo ndio mfano mzuri unaoonyesha uhalali wa kumwacha mke kwa sababu ya uasherati(porneia). Ndio sababu hata leo kuna msemo kwamba uchumba sio ndoa. In other words, mtu akitoa posa baadaye akagundua mwenzake amefanya uasherati, ni ruksa kabisa kumwacha au kuvunja huo uchumba.

Katika Mt 5:312 Yesu amepinga utoaji wa talaka. Angalia anavyosema: "lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa habari ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini."

Maandiko hayo maana yake ni kwamba ukimwacha mke wako kwa madai kwamba amefanya uzinzi, huyo mke atahesabiwa mzinzi maisha yake yote. Na mtu yeyote atakayemwoa, na yeye atahesabiwa mzinzi. Kwa hiyo kwa maneno mengine mwanaume aliyefunga ndoa halali hapaswi kumwacha mkewe.

Ndoa ikiishafungwa, wanandoa hawapaswi kutengana kwa sababu yoyote ile, hata uzinzi. Angalia Yesu anavyosema katika Mathayo 19:6 "Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe.”

Soma 1 Wakorintho 7:10-11 uone pia jinsi Paulo alivyosisitiza tusiachane:
“Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.”

Kwa hiyo, uzinzi sio sababu ya kuvunja ndoa. Kumbuka tena mafundisho ya Yesu kuhusu msamaha:
Mathayo 18:21-22
"Kisha Petro akamwendea akamwambia, Bwana, ndugu yangu anikose mara ngapi nami nimsamehe? Hata mara saba? Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.”

Je, kama tunawasamehe ndugu, marafiki na majirani, sembuse mwenzi wetu wa maisha?

Kumbuke tena yule mama aliyefumaniwa. Yesu alimwambia nini. Kumbuka yule mama msamaria aliyekuwa na waume watano, aliambiwa nini. Ni msamaha tu. Hata sisi tulipokuwa wenye dhambi, Yesu alitusamehe dhambi zote. Kwanini sisi tusisamehe?
Mt 6:14-15
Kwa maana mkiwasamehe watu makosa yao, na Baba yenu wa mbinguni atawasamehe ninyi. Bali msipowasamehe watu makosa yao, wala Baba yenu hatawasamehe ninyi makosa yenu.

Haya, mimi nimemaliza. Weka hapa sasa na wewe nondo zako, zinazokuambia kwamba ni halali mume kumwacha mkewe kwa sababu ya uzinzi.
 
Katika siku hizi za mwisho, wapinga Kristo wameanza kutumia njia mbalimbali kuwapotosha waumini wa kweli. Mojawapo ya njia hizo ni kuzalisha Biblia potofu au tafsiri potofu za Biblia.

Kama huna habari kuna kitabu kinaitwa "The Satanic Bible" (Biblia ya Shetani), kilichoandikwa na Anton LaVey. Hii sio Biblia ya ki-Mungu bali ni kitabu kinachotukuza uasi, ubinafsi, na ibada za kishetani. Na wala sio tafsiri ya Biblia, bali ni maandiko ya kidini ya dhehebu la kishetani (Church of Satan).

Lakini pia yapo matoleo ya Biblia ambayo, japo yanadai kuwa ni tafsiri halali za kibiblia, yamehaririwa kwa makusudi ili kupotosha mafundisho ya msingi ya Kikristo. Tafsiri hizo huondoa au kubadilisha maandiko ya awali kuhusu Uungu wa Kristo, wokovu kwa neema, hukumu ya dhambi nk. Tuwe macho, hizi ni nyakati za mwisho.
1 Tim 4:1-5
"Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani.."

Hivyo, usiamini kila toleo jipya la Biblia bila kuelewa chanzo chake. Kwa wazungumzaji wa Kiswahili, nashauri wasome tafsiri ya kuaminika iitwayo: Biblia ya Kiswahili ya Union Version (SUV). Biblia hiyo imetafsiriwa kwa uaminifu mkubwa kwa kuzingatia lugha za awali za Biblia — yaani Kiebrania (kwa Agano la Kale) na Kigiriki (kwa Agano Jipya).

Kuna tafsiri mpya ya Kiswahili, imebadili kile kifungu: "Isipokuwa kwa sababu ya uasherati," wameandika: "Isipokuwa kwa sababu ya uzinzi." Uasherati na uzinzi ni maneno mawili tofauti. Mtu anaruhusiwa kumwacha mkewe kwa sababu ya uasherati tu, sio uzinzi.

Kwa wapenzi wa lugha ya Kiingereza tafuta Biblia ya King James(KJV). Ukiona kiingereza chake ni kigumu, tafuta toleo lake jipya(NKJV).

Tafsiri hizo pia zimezingatia lugha za awali.

Biblia ya KJV na NKJV ni biblia mbili tofauti?
 
Kitu original ni lazima kiwe na vitu feki kwa jina hilo hilo:
Mifano
Samsung kuna Samsug
Hivyo Biblia zipo nyingi feki
Hivyo Shetani ni lazima awe na Biblia yake ili afurahi
Kuna
Satanic Bible
Freemasonic Bible
Mormonic Bible

Na hizo Bible zote zina wahusika wote wa kwenye Biblia halisi.
Yaani kuna Ibrahimu, Musa, Daudi, Sulemani, Yesu na wanafunzi wake wote 12:

Na kila hizo Bible zinasema wahusika wote ni wa hizo dini,.
Yaani Masonic Bible inasema Sulemani ni Freemason:

Ndio maana hata Qurani nayo inasema Suleimani ni Mwislamu:
Bible ni kiboko ya poti
 
Umekusudia biblia ipi kiboko yao ? Queen James Version, KJV, NIV, AV , au ni ipi kati ya maelfu ya biblia tofauti?
 
Acha Ushoga dogo:
Unakubali vipi mwanamume akupumulie kisogoni:

Nenda kwa Mwamposa akakuombee hayo mapepo ya Ushoga yaondoke:

Bila maombi ya kuyaondoa hayo mapepo huwezi kuuacha Ushoga:

Ushoga unasababishwa na kupagawa na mapepo ya Ushoga:

Yaani mwanamume unapenda kufirwa, ni mambo ya ajabu sana kwakweli:

Watoto wote hawa wazuri unaishia kuwakodolea macho tu:
Pumbavu sana wewe
 
Ukimaliza kunitusi jibu swali Mimi nimekusamehe Kwani Roho Mtakatifu wenu anawaongoza kutukana watu

Jibu swali

Umekusudia biblia ipi kiboko yao ? Queen James Version, KJV, NIV, AV , au ni ipi kati ya maelfu ya biblia tofauti?
 
Kitu original ni lazima kiwe na vitu feki kwa jina hilo hilo:
Mifano
Samsung kuna Samsug
Hivyo Biblia zipo nyingi feki
Hivyo Shetani ni lazima awe na Biblia yake ili afurahi
Kuna
Satanic Bible
Freemasonic Bible
Mormonic Bible

Na hizo Bible zote zina wahusika wote wa kwenye Biblia halisi.
Yaani kuna Ibrahimu, Musa, Daudi, Sulemani, Yesu na wanafunzi wake wote 12:

Na kila hizo Bible zinasema wahusika wote ni wa hizo dini,.
Yaani Masonic Bible inasema Sulemani ni Freemason:

Ndio maana hata Qurani nayo inasema Suleimani ni Mwislamu:
Bible ni kiboko ya poti

List of New Testament verses not included in modern English translations - Wikipedia List of New Testament verses not included in modern English translations - Wikipedia
 
Katika siku hizi za mwisho, wapinga Kristo wameanza kutumia njia mbalimbali kuwapotosha waumini wa kweli. Mojawapo ya njia hizo ni kuzalisha Biblia potofu au tafsiri potofu za Biblia.

Kama huna habari kuna kitabu kinaitwa "The Satanic Bible" (Biblia ya Shetani), kilichoandikwa na Anton LaVey. Hii sio Biblia ya ki-Mungu bali ni kitabu kinachotukuza uasi, ubinafsi, na ibada za kishetani. Na wala sio tafsiri ya Biblia, bali ni maandiko ya kidini ya dhehebu la kishetani (Church of Satan).

Lakini pia yapo matoleo ya Biblia ambayo, japo yanadai kuwa ni tafsiri halali za kibiblia, yamehaririwa kwa makusudi ili kupotosha mafundisho ya msingi ya Kikristo. Tafsiri hizo huondoa au kubadilisha maandiko ya awali kuhusu Uungu wa Kristo, wokovu kwa neema, hukumu ya dhambi nk. Tuwe macho, hizi ni nyakati za mwisho.
1 Tim 4:1-5
"Basi Roho anena waziwazi ya kwamba nyakati za mwisho wengine watajitenga na imani, wakisikiliza roho zidanganyazo, na mafundisho ya mashetani.."

Hivyo, usiamini kila toleo jipya la Biblia bila kuelewa chanzo chake. Kwa wazungumzaji wa Kiswahili, nashauri wasome tafsiri ya kuaminika iitwayo: Biblia ya Kiswahili ya Union Version (SUV). Biblia hiyo imetafsiriwa kwa uaminifu mkubwa kwa kuzingatia lugha za awali za Biblia — yaani Kiebrania (kwa Agano la Kale) na Kigiriki (kwa Agano Jipya).

Kuna tafsiri mpya ya Kiswahili, imebadili kile kifungu: "Isipokuwa kwa sababu ya uasherati," wameandika: "Isipokuwa kwa sababu ya uzinzi." Uasherati na uzinzi ni maneno mawili tofauti. Mtu anaruhusiwa kumwacha mkewe kwa sababu ya uasherati tu, sio uzinzi.

Kwa wapenzi wa lugha ya Kiingereza tafuta Biblia ya King James(KJV). Ukiona kiingereza chake ni kigumu, tafuta toleo lake jipya(NKJV).

Tafsiri hizo pia zimezingatia lugha za awali.
Mimi sijawahi kusikia Quran ya shetani.
Sijawahi kusikia Msikiti wa shetani!
Ila kuna Biblia ya shetani.
Kuna kanisa la shetani!
Hii dini inashida gani hadi inapendwa na shetani hivi?
 
Back
Top Bottom