Manowari ya KΓΆnigsberg (Naendelea)
Licha ya uwezo wake wa kurusha makombora na kasi, meli ya kivita ya Ujerumani ilitatizwa vikali na kutoweza kupata vifaa na makaa ya mawe yenye ubora.
Hatimaye Max Looff aliipatia KΓΆnigsberg makaa ya mawe kutoka kwa meli ya ugavi ya Ujerumani, pwani ya Somalia, (meli ya kivita ilikuwa chini ya tani 14 tu za makaa ya mawe) na kuendelea kutafuta meli za washirika za mizigo, lakini bila kupata yoyote. Mapema Septemba,1914 huku KΓΆnigsberg ikihitaji marekebisho ya injini, Max Looff aliipeleka meli hadi kwenye Delta ya Rufiji.
Wakati wa ukarabati huo, taarifa za kijasusi zilimfikia Looff na kikosi chake kwamba meli ya kivita ya Uingereza imeingia katika bandari ya Zanzibar.Wakaanza safari mara moja kutoka mafichoni Delta ya Rufiji, mapema asubuhi iliyofuata (20 Septemba 1914) KΓΆnigsberg ilikuwa nje ya kisiwa cha Zanzibar. Ujasusi ulikuwa sahihi, HMS Pegasus ilikuwaimetia nanga na bila wasiwasi wowote.