Je, unajua kuwa Roho huwa ina kawaida ya kutoka tulalapo?

Kwa mujibu wa Qur'an kila tunapo lala roho huenda Kwa Mwenyezi Mungu na huyo ndo mwenye roho zake.

Kwa Sisi Waislamu kwakuwa ni Kitabu chetu tunaamini hivyo
Hata wenye midhambi [emoji848][emoji848][emoji849][emoji15][emoji15][emoji15][emoji3064][emoji3064]
 
Roho ikikamatwa na wachawi ikiwa inazunguka duniani, mwili hauwezi amka ndio unasikia mtu alilala kalala jumla kufa usingizini. Means roho haikufanikiwa kurudi kwenye mwili.
Katika hili la wachawi naomba nikupinge kidogo, Kwa mujibu wa Imani yangu na Kitabu changu.

Allah anasema zile roho zilizo hukumiwa kufa basi huzizuia na kubaki nazo na zile ambazo Mda wake bado huziruhusu kurudi ktk miili yetu.

Anyways hiyo ni Imani yetu kwahiyo kuwa huru kuamini kile unacho amini
 
Hata wenye midhambi [emoji848][emoji848][emoji849][emoji15][emoji15][emoji15][emoji3064][emoji3064]
Haijalishi mwenye dhambi nyingi au ndogo kwasababu hakuna mwanadamu Mkamilifu

Huo ndio utaratibu WA hizo roho kwenda kuripoti kwake
 
Mkuu mambo ya roho au elimu ya roho imefichwa Sana na Mwenyezi Mungu.

Watu walimuuliza Mtume kuhusu roho,Allah akajibu kuwa elimu ya roho iko kwakwe na watu hawajui elimu yake isipokuwa Ile ndogo waliyopewa.

Kwahiyo hatuna zaidi tunachokijua zaidi ya kile kidogo alichotufahamisha.
Kwann anaficha? Kama alitupa kama sehemu ya zawadi ya uhai haikupaswa kuifahamu ili tuwe na chaguzi sahihi za namna ya kuitumia? Ukizingatia atakuja kuichoma moto iwapo hukuitumia vzr?
 
Natamani Hilo swali ungemuuliza yeye mkuu

Lkn naamini kwa elimu yake na ujuzi wake kuna hekima kubwa juu ya hilo
 
Mnanitisha basi nitakuwa nalala mchana usiku nakesha
Hatujaambiwa kuwa Ni usiku Tu madam, just imagine je mtu ambaye anafanya kazi night shift INA maana roho yake haiendi Kwa Mungu?

Huenda akilala yeye mchana ndio roho yake huenda Kwa Mungu,na by the way huenda ni safari ya sekunde chache au dakika chache Tu mara paap zoezi limekamilika.

Haina haja kuogopa ni utaratibu wake mwenyewe ameupanga
 
Natamani Hilo swali ungemuuliza yeye mkuu

Lkn naamini kwa elimu yake na ujuzi wake kuna hekima kubwa juu ya hilo
Anyway, sioni kwann mambo yawe kwa mfumo uliopo. Kama tumeumbwa kwa mfano wake basi sioni sababu yoyote ya kuogopa kujiuliza maswali magumu sababu ujasiri lazima umetoka kwake. Na swali mojawapo ni kwann amejificha na siku atajitokeza atakuja na kiberiti kwa waliokosea kutokana na kujificha kwake.
 
Swadakta mkuu ni kweli kabisa

Kuna siku moja nilishtuka usiku na kujiona mwepesi sana na kwakuwa nishayajua hayo mambo basi nikatulia kimya kabisa bila kujitingisha hata kidogo nikaona naelea na kwenda sehemu nyingine kabisa.
Chai tembele
 
Katika hili la wachawi naomba nikupinge kidogo, Kwa mujibu wa Imani yangu na Kitabu changu.

Allah anasema zile roho zilizo hukumiwa kufa basi huzizuia na kubaki nazo na zile ambazo Mda wake bado huziruhusu kurudi ktk miili yetu.

Anyways hiyo ni Imani yetu kwahiyo kuwa huru kuamini kile unacho amini

Ieleweke kwamba mchawi hana uwezo wa kuua mtu bali Mwenyezi Mungu pekee afanyacho mchawi ni kumficha mtu asionekane kwa macho ya kawaida, lakini Muumba anaendelea kumuona dunian.
Kuna kifo kwa matakwa ya wanadamu na matakwa ya Mungu yaani unafutika kabisa duniani.
 
Anyway, sioni kwann mambo yawe kwa mfumo uliopo. Kama tumeumbwa kwa mfano wake basi sioni sababu yoyote ya kuogopa kujiuliza maswali magumu sababu ujasiri lazima umetoka kwake. Na swali mojawapo ni kwann amejificha na siku atajitokeza atakuja na kiberiti kwa waliokosea kutokana na kujificha kwake.
Mkuu unajua uwepo wa Mwenyezi Mungu ni Imani, ndio maana Tunatakiwa kuamini juu ya uwepo wake ,kupitia Mitume wake na vitabu vyake.

Na wanao mwamini ndio watafanya mambo mema na na hatimaye kupata raha ya milele na wasio mwamini wataona Dini ni upuuzi na kuacha kufanya mambo mema na kuingia Motoni.

Siku ya mwisho mara paap Mungu huyu hapa,hapo ndo utatamani uwe mchanga upotee ardhini
 
Ieleweke kwamba mchawi hana uwezo wa kuua mtu bali Mwenyezi Mungu pekee afanyacho mchawi ni kumficha mtu asionekane kwa macho ya kawaida, lakini Muumba anaendelea kumuona dunian.
Kuna kifo kwa matakwa ya wanadamu na matakwa ya Mungu yaani unafutika kabisa duniani.
Nakubaliana na wewe mkuu hakuna kinachofanyika pasina idhini yake.

Ila nilitaka kukwambia kile ambacho nilipaswa kukwambia kuhusiana na roho na mtu kufa usingizini
 
Mkuu unajua uwepo wa Mwenyezi Mungu ni Imani, ndio maana Tunatakiwa kuamini juu ya uwepo wake ,kupitia Mitume wake na vitabu vyake.

Na wanao mwamini ndio watafanya mambo mema na na hatimaye kupata raha ya milele na wasio mwamini wataona Dini ni upuuzi na kuacha kufanya mambo mema na kuingia Motoni.

Siku ya mwisho mara paap Mungu huyu hapa,hapo ndo utatamani uwe mchanga upotee ardhini
Sasa kwann imani iwe ina mwisho wa kikatili hivyo?

Kwani mabaya yanayotendwa na wasioamini hayatokani na udhaifu wa mfumo uliopo uliosababisha suala la MUNGU liwe la kiimani? Iwapo MUNGU angetokea paap leo bila kiberiti na akafuta suala la imani na kuweka uhalisia je idadi ya watakaochomwa itapanda au kushuka?
 
Mungu yupo fair Sana Kwa mfano wale watu ambao hawajafikiwa na Mitume Kwa maana moja ama nyingine anajua namna ya kuwahukumu,Kwa maana ambao hawajapa kusikia neno lake.

Na hata huko nyuma hakuangamiza mji wowote maadam hakupeleka Mtume wa kuwaonya, huko sodoma na Gomora alifanya hivyo baada ya kuwaonya na kuwakanya waache upuuzi wao.

Ninachotaka kusema hapa hawa wasio na Imani na Mwenyezi Mungu hawana sababu ya kufanya hivyo kwakuwa vitabu vipo na mawaidha yanatolewa kila kukicha.

Na ebu tuwe kwakweli kama sio upuuzi ni nini,ebu ajiulize binadamu mwenyewe ameumbwa na Nani,je ulimwengu huu imetokana na Nani na akitafakari Kwa ujumla wake hakika utajua kuna muanzilishi WA haya yote.

Kwahiyo wanajifanya viburi Tu pasina sababu yoyote ile
 
Wewe huna marafiki, ndugu, jirani ambao ni wema kwako na hawana imani yako?

Utaona ni sawa daktari aliyeokoa maisha yako bila malipo akiungua sababu si wa imani yako? Kuna roho mbaya kuzidi hiyo?
 
Mkuu yanayo mfanya mwanadamu afaulu Kwanza amtambue Mola wake kuwa Ni mmoja Tu Hana mshirika
Na mengine ni kufanya mema na kuacha mabaya.

Na mwisho wa siku kuna mizani ya kupima matendo yetu,ikiwa matendo yako ni mazito kuliko maovu yako umefaulu na ikiwa maovu Yako ni mazito kuliko mema umefeli.

Haina haja kucomplain tuwajibike Kwa matendo yetu
 
Hatujaambiwa kuwa Ni usiku Tu madam, just imagine je mtu ambaye anafanya kazi night shift INA maana roho yake haiendi Kwa Mungu?

Huenda akilala yeye mchana ndio roho yake huenda Kwa Mungu,na by the way huenda ni safari ya sekunde chache au dakika chache Tu mara paap zoezi limekamilika.

Haina haja kuogopa ni utaratibu wake mwenyewe ameupanga
Niambe hiki kitu mtu akisikia baridi halafu akawa viungo vyake havifanyi kazi Kwamuda wamadakika hii mnaitaje??
 
Kwaiyo wanaokufa ni kwamba roho imeenda kucheza inapoenda kuchezaga na haijarudi
 
Mkuu kuna maelezo mengi Sana kuhusu roho na mambo yake

Ila Kwa muktadha WA Uzi huu nimezungumzia roho kwenda Kwa Mungu Kwa mujibu wa Qur'an , na kuripoti kwake,na zile zilizo hukumiwa kufa usiku huo zitabaki kwake Kwa maana huyo mtu siku ya kufa umefika,na wale ambao bado mpaka Mda huu tupo Jf roho zilirudishwa na Sasa tunaendelea kuperuzi mitandaoni
 
Back
Top Bottom