Je, unajua kuwa Roho huwa ina kawaida ya kutoka tulalapo?

Je, unajua kuwa Roho huwa ina kawaida ya kutoka tulalapo?

Hivi umeshawahi lala usiku halafu ukajikuta kama unaota hivi lakini fahamu zako zinakuonyesha kabisa upo macho na unajiona mwepesi Sana pasipo kawaida na saa nyingine huenda ukahisi kama upo hewani hivi

Au

Unaweza kwenda sehemu Fulani ambayo hujawahi fika lakini kuna kumbukumbu Fulani inakujia kana kwamba hiyo sehemu unaijua au ushawahi fika hivi.

Kifupi ni kwamba roho zetu huwa zinatoka katika viwili viwili vyetu na kwenda kupiga misele sehemu mbali mbali na mara nyingine hukutana na roho nyingine za ndugu zetu,ndio maana utasikia mtu atakwambia Jana nilimuota babu ananiambia moja mbili tatu na mara nyingi watu hao walikuwa Wacha Mungu.

Anyways sasa ni hivi, Kwa kawaida tunapo lala basi roho zetu huenda Kwa Mwenyezi Mungu kila siku ya Maisha yetu hapa duniani,sasa huenda zinaporudi ndio hukutana na roho nyingine na kukutana na matukio mbali mbali.

Kwa mujibu wa Qur'an inasema hivi Mwenyezi Mungu huzipokea roho zinazo kufa Kwa maana roho ambazo watu wameaga dunia,na roho ambazo watu wanakuwa wamelala,zile roho ambazo Mda wa kufa umefika huzizua na kubaki nazo,ndio hapa utasikia Fulani bwana kafa usingizini ujue roho yake haikurudi tena usiku huo na wale ambao mdao WA kufa bado basi Mwenyezi Mungu huziachia zile na kurudi katika miili yetu.

"MWENYEZI MUNGU huzipokea roho zinapo kufa. Na zile zisio kufa wakati wa kulala kwake, huzishika zilizo hukumiwa kufa, na huzirudisha nyengine mpaka ufike wakati uliowekwa. Hakika katika hayo bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri."
Azzumar : 42

Hayo ndio mambo ya Mwenyezi Mungu hakika mambo yake hakuna ayajuaye na hufanya katika namna atakavyo.

Ndio maana inatakiwa usiku Tulalapo basi tuombe msamaha na kuomba toba Kwa makosa yetu tuliyo fanya kutwa nzima kwani hatujui kama kesho tutaamka salama au laa!

Ni hayo Tu!

Kazakh destroyer
Msonjo
adriz
Nurain
Akhi
baby zu

roho huwa haitoki unapolala kinachotoka ni nafsi. nafsi ndio hutoka na kuzinguka. roho hutolewa na mtoa roho siku yako ya mwisho malaika mtoa roho
 
Sio kutoka tu sometimes roho hufanya time traveling... Spiritual time traveling.

Ndio maana unaweza kufika sehemu for the first time ukawa unahisi sio mara yako ya kwanza. The truth ni kua roho yako ilianza kufika kabla ya physical body yako.

Ps. Miili yetu hua nalimit uwezo wa roho zetu.
Mmh hiyo ya kufika sehemu na kuhisi siyo mara ya kwanza naona kila mtu anasema lake wengine husema inahusiana na reincarnation
 
roho huwa haitoki unapolala kinachotoka ni nafsi. nafsi ndio hutoka na kuzinguka. roho hutolewa na mtoa roho siku yako ya mwisho malaika mtoa roho
Kwa mujibu wa Qur'an kila tunapo lala roho huenda Kwa Mwenyezi Mungu na huyo ndo mwenye roho zake.

Kwa Sisi Waislamu kwakuwa ni Kitabu chetu tunaamini hivyo
 
Na kuna Ile unaweza kulala chali ukafake ubongo wako ujue kama umelala halafu unaanza hisi ganzi miguuni inapanda kuja mdogo mdogo nasikia ukikomaa Bila kuogopa unajikuta unatoka ndani ya mwili
Hiyo astral projection
 
Sio kutoka tu sometimes roho hufanya time traveling... Spiritual time traveling.

Ndio maana unaweza kufika sehemu for the first time ukawa unahisi sio mara yako ya kwanza. The truth ni kua roho yako ilianza kufika kabla ya physical body yako.

Ps. Miili yetu hua nalimit uwezo wa roho zetu.
Neville Gorddad
 
Yeah ila hiyo huwa ni voluntary process na si kila mtu hufanikiwa kuifanya
Yeah nilijaribu one time nikafeel ganzi inapanda toka miguuni inapanda kuja juu dah nikaogopa nikaona isiwe tabu nikajitingisha na kusitisha zoezi Ila nitajaribu tena
 
Yeah nilijaribu one time nikafeel ganzi inapanda toka miguuni inapanda kuja juu dah nikaogopa nikaona isiwe tabu nikajitingisha na kusitisha zoezi Ila nitajaribu tena
Haha ila mkuu si inasemekana kufanya hivyo ni dhambi
 
Lipo wazi, roho inaweza ikapiga trip nyingi Sana sehemu nyingi duniani kwa dakika chache, ndoto ni maisha halisi yanayoendelea duniani.
 
Roho ikikamatwa na wachawi ikiwa inazunguka duniani, mwili hauwezi amka ndio unasikia mtu alilala kalala jumla kufa usingizini. Means roho haikufanikiwa kurudi kwenye mwili.
 
Pili mtu akilala usikurupuke usimstue kumuasha kwa nguvu ni hatari kama roho iliacha mwili.
Dunia Ina mengi still bado sayansi haijatupa majibu
 
Write your reply...Mimi roho yangu inaonana na watu ila nakua siongei,napata raha kwenye kupaa.mda mwingine nakutana na wadada wazuri ila sijawahi wagusa
 
Kwanza kwakuwa roho inatoka Kwa mda mchache naona hatufi,kwasababu kufa hakuji Kwa bahati mbaya Ila visa ya kuisha duniani inakuwa imekwisha.

Kwa mfano unaweza jiuliza je wakati roho inatoka je tunaacha Kuota ndoto au tunaota?

Binafsi naona tunaota kama kawaida,Ila haya ni maono yangu Tu.

Viumbe vyote ambavyo vipo hai vina roho akiwemo sisimizi
Roho ina ubongo? Kama haina utendaji wake unaongozwa na nn?
 
Haha ila mkuu si inasemekana kufanya hivyo ni dhambi
Kwakwel sijui kama ni dhambi Ila nilidhibitisha kitu kimoja kuwa,kwanini tukiota usiku tunakimbia au kucheza au kupigana mbona huwa mwili umetulia Tu kitandani?

Kumbe mara tuanzapo kulala kuna ganzi ya asili ambayo huja mwilini na Kutofanya mwili utulie la sivyo tungekuwa tunaamka na majeraha Sana kutokana na ndoto tunazoota.

Binafsi mara moja moja Sana hujikuta narusha mguu usingizini na kugonga kitanda huenda ganzi ya asili huwa inapotea kiaina
 
Roho ina ubongo? Kama haina utendaji wake unaongozwa na nn?
Mkuu mambo ya roho au elimu ya roho imefichwa Sana na Mwenyezi Mungu.

Watu walimuuliza Mtume kuhusu roho,Allah akajibu kuwa elimu ya roho iko kwakwe na watu hawajui elimu yake isipokuwa Ile ndogo waliyopewa.

Kwahiyo hatuna zaidi tunachokijua zaidi ya kile kidogo alichotufahamisha.
 
Back
Top Bottom