Allah anasema sura tusiyoijua, sasa kwanini wewe tayari umeishaijua??
Tuaposema roho itahukumiwa ni sababu yenyewe ndio mbeba taarifa za matendo ya mtu, mfano wa Roho ni kama black box kwenye ndege, na ndio maana mfano muuaji watu wanaweza kumuita mtu mwenye roho mbaya kwasababu ni roho yake ndiyo inabeba taarifa za maovu yake.
Unauliza inayoadhibiwa na kuhukumiwa ni roho na mwili au??, inayohukumiwa na kuadhibiwa ni roho mwili ni kama chombo tu cha kubeba huo mwili na ndio maana Allah kauita huo mwili umbo tusilolijua. Roho ndani ya huo mwili ni sawa na dumu la mafuta ya taa ndani ya nyumba, ukipiga kiberiti dumu ndilo litashika moto na mafuta yakiisha moto utazimika, hapo sasa utaona kwamba mafuta ndio dhambi, dumu ndio roho na nyumba ndio huo mwili tusioujua na moto ndio afhabu ya jehanamu, huo ni mfano tu waila الله يعلم.
Mkuu naona hapa unachanganya madesa.
Kwanza umeniuliza je imekuwaje Hilo umbo nimeshalijua nilikwambia kutokana na melezo ya Mtume.
Lakini pili, je unajua upi ni msingi WA hiyo Aya ya 56:60?
Msingi WA hiyo ni Aya ya 47 ya Sura hiyo hiyo
"Na walikuwa wakisema: Tutakapo kufa na tukawa udongo na mafupa, ati ndio tutafufuliwa?"
57:47
Allah anawazungumzia watu ambao wanaona ni vigumu baada ya kuoza na kubakia mifupa kuwa hataweza kufufuliwa, ndio inakuja hii aya
نَحْنُ قَدَّرْنَا بَيْنَكُمُ الْمَوْتَ وَمَا نَحْنُ بِمَسْبُوقِينَ
Sisi tumekuwekeeni mauti; na wala Sisi hatushindwi
عَلَىٰ أَن نُّبَدِّلَ أَمْثَالَكُمْ وَنُنشِئَكُمْ فِي مَا لَا تَعْلَمُونَ
Kuwaleta wengine badala yenu na kukuumbeni nyinyi kwa umbo msilo lijua.
وَلَقَدْ عَلِمْتُمُ النَّشْأَةَ الْأُولَىٰ فَلَوْلَا تَذَكَّرُونَ
Na bila ya shaka mlikwisha jua umbo la kwanza, basi kwa nini hamkumbuki?
56:60-62
Ukiangalia Aya hii Allah anajaribu kuwaeleza au kuwafahamisha kwamba hata Sisi tukifa au baada ya umauti wetu Kwa uwezo wake hashindwi kuleta viumbe wengine,maana wao walidhani ni vigumu kufufuliwa ndio anazidi kuwaambia kana kwamba sio kufufua Tu Bali hata viumbe wengine anaweza kuwaleta
Na
Amesema hashindwi kuleta kutuumba katika umbo tusilolijua,hapo inaonyesha kwamba ametoa mfano Tu lakini hajasema kuwa tutakuwa katika umbo tusilolijua na akaendelea katika ya 62 Kwa kusema bilashaka tulishajua umbo letu la awali alilotuumbia je ni kipi cha ajabu mpaka hatukumbuki uwezo wake?
Na Mimi kukuuliza wewe je inaadhibiwa roho na mwili au roho peke yake?
Ni kwamba Allah amesema ataujaza Moto WA jahanamu Kwa majini na watu, na hakusema atajaza huo Moto na roho.
Vile vile anaendelea katika Aya nyingine Kwa kusema kuwa kila mwanadamu atakapo kuwa anaungua basi atambadilishia ngozi nyingine ili machungu yaendelee ,na kwanini ngozi?
Kwasababu ngozi ndio organ ambayo inahusika na hisia za maumivu.
Natumaini umepata mwanga kidogo