Je, unajua kwamba huyo mke/mme uliye naye sasa sio wako?

Je, unajua kwamba huyo mke/mme uliye naye sasa sio wako?

nikiona mtu anatafuta mwenza humu numuona dishi limeyumba kabisa,
 
Maana ya porneia katika Kigiriki cha Agano Jipya ni uasherati. Uasherati ni mahusiano ya kimwili kabla watu hawajafunga ndoa
Sasa hebu eleza ni kwa namna gani watu waliopo kwenye ndoa wanaweza kufanya uasherati, au ni namna gani uasherati unaweza kuwahusu watu walio kwenye ndoa mpaka wakaachana, ilhali uasherati ni kwa wale kabla ya ndoa
 
Sasa hebu eleza ni kwa namna gani watu waliopo kwenye ndoa wanaweza kufanya uasherati, namna gani uasherati unaweza kuwahusu watu walio kwenye ndoa mpaka wakaachana, ilhali uasherati ni kwa wale kabla ya ndoa
Ukisoma Biblia kwa makini utagundua kuwa nyakati za mwanzo mtu akiishatoa posa kwa mchumba wake, hata kabla hawajaoana, walikuwa wanaitwa mtu na mkewe. Soma Kum 22:23-24 na Mt 1:18-20. Katika hali hiyo ya uchumba, kama "mke" amefumaniwa amefanya uasherati na mwanaume mwingine tofauti na huyo waliyepeana posa, akapata mimba, ilikuwa halali kumwacha kwakuwa anaonyesha wazi sio mwaminifu. Ndiyo sababu Yusufu alitaka kumwacha Mariamu akidhani amefanya uasherati. Hata leo mambo yako hivyohivyo. Kuna watu wanakaa katika uchumba miaka hata miwili bila kukutana kimwili. Ikitokea mke amevunja agano la kuoana, akalala na mwingine, huyo mme yuko huru kumwacha. Huo ndio uasherati unaozungumzwa katika Kitabu kile. Sio uzinzi.
 
Kuna watu wanaodai kwamba kama mume au mke amefumaniwa akifanya uzinzi basi ni halali kumwacha au kumpa talaka na kuoa au kuolewa na mwingine. Wanatumia andiko la Mathayo 5:32 kuhalalisha madai yao. Andiko hilo linasema hivi:
Mathayo 5:32
"Lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini."

Ni muhimu kujua kuwa kuna tofauti kati ya uasherati na uzinzi.
Uasherati ni kabla watu hawajaoana. Uzinzi ni baada ya watu kuoana. Kumbuka jinsi Yusufu alivyotaka kumwacha Mariamu. Alifikiri amefanya uasherati. Malaika akamwambia asimwache kwakuwa mimba yake ni kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Kwa sababu hiyohiyo watu walio katika uchumba, hata kama wamepeana posa tayari, ikithibitika kuwa mmoja amefanya uasherati, huyo mwenzake ni ruksa kumwacha kwa sababu anaonyesha wazi sio mwaminifu. Lakini watu wakiishaoana, uzinzi siyo kisingizio cha kuachana. Mwenzako akifanya uzinzi msamehe. La sivyo, ukimwacha, ukae hivyohivyo, usioe/usiolewe. Ukweli huu ni mchungu. Lakini hakuna shortcut, kama tunataka kwenda mbinguni ni lazima tutii maagizo ya Mungu.
Depal Ni Kwamba ukimuacha ukae hivyo hivyo. Mi sifagilii kwakweli🤔
 
Ukisoma Biblia kwa makini utagundua kuwa nyakati za mwanzo mtu akiishatoa posa kwa mchumba wake, hata kabla hawajaoana, walikuwa wanaitwa mtu na mkewe. Soma Kum 22:23-24 na Mt 1:18-20. Katika hali hiyo ya uchumba, kama "mke" amefumaniwa amefanya uasherati na mwanaume mwingine tofauti na huyo waliyepeana posa, akapata mimba, ilikuwa halali kumwacha kwakuwa anaonyesha wazi sio mwaminifu. Ndiyo sababu Yusufu alitaka kumwacha Mariamu akidhani amefanya uasherati. Hata leo mambo yako hivyohivyo. Kuna watu wanakaa katika uchumba miaka hata miwili bila kukutana kimwili. Ikitokea mke amevunja agano la kuoana, akalala na mwingine, huyo mme yuko huru kumwacha. Huo ndio uasherati unaozungumzwa katika Kitabu kile. Sio uzinzi.
Hata sasa ukimtolea mwanamke mahari, technically anakua ni mkeo, hivyo mtu anayetoka nae anakua amemchukua mkeo. Huyu mwanamke anaachwa kwa sababu ya uzinzi na sio uasherati. Nimesoma hiyo Mt 1:18-20 ila sijaona mahali ambapo inasemwa Yusufu alitaka kumuacha Mariam sababu ya kudhani amefanya uasherati.

Mwaka 2011 kuna siku nilikuwa nasikiliza Radio Maria, nikamsikia Padri mmoja akieleza maana ya kuachana kwa uzinzi, akaeleza kuwa ni pale waliooana wanapogundua kuwa ni ndugu ambao uhusiano wao kibiblia umekatazwa, hapo wataachana, na ndio kilichomaanishwa. Ilikuwa ndio tafsiri ya huyo Padri akirejea maandiko ya kiyunani.

Mimi kwa tafsiri yangu, uzinifu unaozungumzwa ni wa mtu kuchakatwa nje. Huyu imeruhusiwa kumuacha.

Hata hivyo, hujaeleza kuhusu mwanamke ambaye ana tofauti ya imani na mumewe, si ameruhusiwa kuachwa? 1 Kor 7:15
 
Naongea na wewe uliyeachana na mwenzi wako wa kwanza na kuoa au kuolewa tena. Nakujulisha kuwa huyo mke/mume uliye naye sasa sio wako mbele za Mungu — unazini.

Katika dunia ya sasa ambapo talaka na ndoa ya pili au ya tatu zinaonekana kama jambo la kawaida, ni muhimu sana kwa watu wanaotamani kwenda mbinguni kufahamu msimamo wa Mungu juu ya ndoa, talaka, na kuoa au kuolewa tena baada ya talaka.

1. Ndoa ni agano la milele, sio mkataba wa muda
Biblia inafundisha kuwa ndoa ni muungano wa kiroho na kimwili uliowekwa na Mungu mwenyewe.
Katika Mwanzo 2:24 tunaambiwa:
“Kwa hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”

Muungano huu wa “mwili mmoja” si wa muda, ni wa kudumu mpaka kifo kitakapowatenganisha. Hili linasisitizwa tena na Yesu Kristo katika Mathayo 19:6
"Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe..”

Kwa hiyo, talaka haibatilishi kile Mungu alichokiunganisha. Ingawa mwanadamu anaweza kutoa talaka, mbele za Mungu bado mme na mke wa kwanza wanahesabika kuwa wameunganishwa.

2. Talaka haitoi ruhusa ya kuoa au kuolewa tena
Yesu mwenyewe alizungumzia jambo hili kwa uwazi sana. Katika Luka 16:18 anasema:
"Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine anazini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe anazini.”

Hapa tunaona wazi kuwa kuoa au kuolewa tena baada ya talaka ni uzinzi. Kwa lugha nyingine, kama ulimwacha mume au mke wako wa kwanza, ukaoa au kuolewa tena, basi huyo uliye naye sasa sio wako. Mbele za Mungu unahesabika unaishi katika uzinzi.

3. Talaka iliruhusiwa kwa sababu ya ugumu wa mioyo — sio mpango wa Mungu
Yesu alipoulizwa kuhusu talaka, alisema katika Mathayo 19:8:
“... Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo.”

4. Hatari ya kuishi katika uzinzi
Wale wanaoishi na wake au waume wa ndoa ya pili, wanaishi katika hali ya dhambi — yaani uzinzi wa kudumu. Na Biblia inasema wazi katika 1 Wakorintho 6:9-10:
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti.”

Hili ni onyo kali. Kama unaendelea kuishi na mke au mume asiye wako bila kutubu na kurekebisha, una hatari ya kupoteza uzima wa milele.

5. Suluhisho: Tubu na umrudie mme au mke wako wa kwanza
Suluhisho sio kuhalalisha mahusiano uliyo nayo sasa. Suluhisho ni kutubu kwa dhati, kujitenga na hali ya uzinzi, na kumrudia mwenzi wako wa kwanza. Kama huwezi kumrudia huyo wa kwanza, ukae hivyo hivyo peke yako.
Katika 1 Wakorintho 7:10-11, Paulo anaandika:
“Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.”

Biblia haiungi mkono ndoa ya pili baada ya talaka, bali inashauri ama kubaki bila kuolewa/kuoa au kumrudia mwenzi wa kwanza.
We mbona mchumba wako aliyekutoa b...... hajakuoa ukaolewa na kijana wa watu mcha Mungu
 
"kila amwachae mwenzi wake isipokua kwasababu ya zinaa na kumuoa mwingine azini"

Isipokua isipokua soma maandiko vizuri!!

Yupo hapa kasingizia wanaume watatu ujauzito yaani mumewe,kijana na mheshimiwa yaani alikua Hana uhakika was aliempa mimba kati ya watatu hai akabaki wote anawaambia mtoto ni wao!!

Talaka au kuachana kunaruhusiwa!!

Hubirini kweli ilivyo acheni kufundisha uongo!!
 
Pole secretarybird
Kuna mtu alisema: "The beautiful ones are not yet born." Hivyo usikate tamaa.
Yeremia 29:11
Kwa maana ninajua mipango niliyo nayo kwa ajili yenu, asema BWANA, ni mipango ya kuwafanikisha na wala si ya kuwadhuru, ni mipango ya kuwapa tumaini katika siku zijazo.
Amen 🙏
 
We mbona mchumba wako aliyekutoa b...... hajakuoa ukaolewa na kijana wa watu mcha Mungu
Waefeso 5:3-4
Lakini uasherati usitajwe miongoni mwenu kamwe, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu wa Mungu. Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu.
 
Waefeso 5:3-4
Lakini uasherati usitajwe miongoni mwenu kamwe, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu wa Mungu. Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu.
Amen na samahani kwa kukukosea na sitorudia kamwe
 
Ila hiyo profile picture yako inaweza kukufanya ukose mke mwema.
Your profile picture is your first introduction...
How you present yourself tells a lot about you
Naibadili maana siko tayari kukosa mke mwema.
 
Back
Top Bottom