Setfree
JF-Expert Member
- Dec 25, 2024
- 6,238
- 8,194
- Thread starter
- #81
Soma Maandiko kwa utulivu. Kama ndugu yako unapaswa kumsamehe 7x70 mke wako ambaye ni mwili mmoja na wewe si zaidi sana? Yesu alitusamehe dhambi zote isipokuwa uzinzi?Unajua maana ya kusamehe,,? Msamaha ni mtu kuacha kama alikuwa na kisasi na wewe basi anaachia but haimaanishi kuwa ni lazima aendelee kuwa na wewe,, naweza nikakusamehe but sitaki tena kuwa na ukaribu na wewe coz unanikumbusha maumivu so utamlazimisha mumeo akusamehe then arudi kama zamani, hata Adam na Hawa walipotenda dhambi bustani ya Eden Mungu aliwasamehe but hakuwaruhusu tena wabaki bustanini je utasema basi Mungu hakuwasamehe,, Big No, usimpangie mtu msamaha Mwanaume anaweza akakusamehe akaachia but asitake tena kuwa karibu na wewe coz itamrudisha nyuma na huwezi kumlaumu kwamba hajakusamehe akati ulifanya kosa kwa makusudi
Pili Biblia imefundisha tusameheane but haijampangia wala kumlazimisha mtu asamehe kosa but Mtu atasamehe kwa ajili ya faida zake binafsi na sio za kwako wewe mkosaji
Kingine Biblia imetaka msamaha kwa ndugu ikiwa na maana kwa yeyote anaekukosea unapaswa kumsamehe but Ndoa ni zaidi ya undugu ndoa ni agano so ukivunja agano usitegemee msamaha kirahisi na hata ukipata msamaha haikupi guarantee kwamba ndo tuwe kama zamani NO, Mtu anaweza akakusamehe ili kuweka Amani but haitamzuia kukuwekea mipaka, kukuweka mbali na yeye au kukutoa kabisa kwenye circle yake, kwa kifupi MTU ANAWEZA AKAKUSAMEHE BUT HUNA MAMLAKA YA KUMPANGIA NAMNA YA KUJILINDA ILI ASIWE DISAPPOINTED TENA NA WEWE
Na cha zaidi Biblia yenyewe imehalalisha ndoa kuvunjika kwa ajili ya Cheating ya mwanamke, Mwanaume anaweza akasamehe ndoa iendelee but hata akihitaji kuvunja ndoa still Biblia imempa uhalali kwa kosa hilo, unachokifanya wewe ni kutaka kugeuza maneno ya kiswahili na kuweka maana unazozijua wewe
Na ukiulizia kuhusu mwanaume msaliti atahukumiwa na Mungu, Biblia imetuhasa wanaume kuwapenda Wake zetu na kama tukiwatenda kwa ubaya Mungu mwenyewe atatuhukumu.
Biblia imemuweka mwanamke chini ya mwanaume na imemuweka mwanaume chini ya Mungu sasa ukitaka usawa mwanaume ahukumiwe kama wewe hapo utajiumiza mwenyewe📌
Halafu nilikuambia, ukiamua kumwacha mke wako, mwache, lakini usithubutu kuoa mwingine. Kaa hivyohivyo ulivyo