Je, unajua kwamba huyo mke/mme uliye naye sasa sio wako?

Je, unajua kwamba huyo mke/mme uliye naye sasa sio wako?

na kwa wale moja katangulia...nao wazikabili vipi hamu zao kimwili?
 
Kuna kitu hujakielewa Biblia ni ngumu sana kuichambua ukiisoma kama gazeti,
Ambacho hukijua ni kuwa Uzinzi upo ndani ya Uasherati.
Uasherati ni ngono yoyote ile isiyo halali yani Ushoga,Uzinzi, Usagaji yote hayo yapo ndani ya neno "Uasherati"
Kwa kifupi Nikisema uasherati it means nimejumuisha hayo mauchafu yote yanayohusisha ngono isiyo halali kwa sababu ngono halali pekee ni ile mnayofanya watu ambao mmeoana📌

So Biblia inaposema ukimuacha mkeo isipokua kwa sababu ya uasherati (either ni mzinzi au msagaji) unamfanya kuwa mzinzi It means kwamba Uasherati ni Mke kwenda kuzini na mwanaume tofauti na mume wake au kwenda kufanya ngono yoyote isiyo halali (kumbuka uzinzi ni aina ya uasherati) basi huyo ni wa kuachwa📌

So Bible iliposema Ukimuacha ISIPOKUA kwa sababu ya uasherati (Mkeo ni either ni mzinzi au msagaji) basi unamfanya kuwa mzinzi ikiwa na maana kwamba kama mkeo si mzinzi hupaswi kumuacha kwa sababu utamfanya kuwa mzinzi kweli.
Au kwa kiswahili rahisi ni sawa na kusema "ukimuacha mkeo isipokua kwa sababu ya uasherati unamfanya kuwa muasherati" kwamba hakua muasherati ila umemuacha kwa sababu zingine ambazo haziruhusiwi basi unamfanya akawe muasherati kweli.

Hakuna maandiko katika Biblia au Quran yanayomtaka mwanaume kuishi na mwanamke muasherati (Mzinzi, msagaji) Piga uwa achana na maandiko tu Mungu mwenyewe kakataa kuishi na mzinzi hakuna dhambi mbaya kama mwanamke kutoka nje ya ndoa ANAACHWA hapohapo yani hakuna utetezi hapo📌 tena kwa waislamu ndo wapo direct kabisa maana sheria zao zinawataka waasherati/wazinzi wauwawe📌
Asante kwa maoni yako. Kwanza nikutahadharishe: ChatGPT, haijui kila kitu. Majibu inayokupa yanatokana na kukusanya mafundisho ya aina nyingi sana. Hivyo ukiitegemea yenyewe tu ikupe majibu, unaweza ukapotoka.

Katika andiko ulilonukuu, neno lililotumika kwa Kigiriki ni "porneia." Hilo katika muktadha wa Wayahudi wa karne ya kwanza, lilimaanisha tendo la ngono kabla ya ndoa au kuvunja ahadi ya uchumba, kama ilivyokuwa kwa Yusufu na Mariamu (Mathayo 1:18-19). Hapo, Yusufu alitaka kumwacha Mariamu kwa siri kwa sababu alidhani alifanya uasherati kabla ya kuishi naye kama mume na mke.

Kwa kigiriki, "Uzinzi" ni "moicheia": ni tendo la mtu aliye kwenye ndoa kufanya ngono na mtu mwingine. Kwa hiyo kusema "uzinzi umo ndani ya uasherati" sio tafsiri ya Biblia. Hiyo ni nadharia ya watu.

Katika orodha ya watakaotupwa motoni, wazinzi, watukanaji, wezi, waongo... wote wapo kundi moja. Hivyo mke wako akifanya uzinzi, ni dhambi inayosameheka; "Msamehe hata saba mara sabini." (Mathayo 18:21–22). Maandiko yanasema ukimwacha ukae hivyohivyo usioe.

Kumbuka Yesu alimsamehe yule mwanamke aliyekamatwa katika uzinzi. Wewe ni nani unayekataa kumsamehe mke wako akifanya uzinzi na kuomba msamaha?

Katika 1 Wakorintho 7:12–13 Maandiko yanasema mke asiyeamini hapaswi kuachwa. Kama asiyeamini hapaswi kuachwa, sembuse mke aliyefanya uzinzi na kutubu?

Usisahau talaka zilitolewa kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya watu. Wewe ukitoa lalaka ina maana una moyo mgumu.

Ndoa ni agano takatifu, sio mkataba wa kuvunja kwa kosa moja.

Kumbuka pia Yesu alitusamehe dhambi zote pamoja na uzinzi. Hivyo tusiposamehe na sisi hatutasamehewa. Naamini Maandiko hayo unayajua.

Hivyo ndugu yangu, kama umemwacha mke wako wa kwanza, omba Mungu akuwezeshe mrudiane naye. Vinginevyo huyo mke unayeishi naye sasa sio wako. Unafanya uzinzi.
 
📌 tena kwa waislamu ndo wapo direct kabisa maana sheria zao zinawataka waasherati/wazinzi wauwawe📌
“Mwanamume akifumaniwa na mke wa mtu mwingine, wote wawili, mwanamume na mwanamke, lazima wauawe. Ndivyo mtakavyokomesha uovu huo miongoni mwenu."
Kumbukumbu.22.22.BHN

(BTW YESU alipowaambia wale jamaa waliokuwa wanamjaribu "asiye na dhambi awe wa kwanza kumpiga jiwe" yule mwanamke, wakapoteana, sababu ilikuwa walipindisha sheria hiyo 👆🏾, mwanamume yuko wapi?)
 
Hiyo ni amri ya Agano la Kale. Yesu alipokuja alituambia ndugu yako akikukosea msamehe hata saba mara sabini. Hivyo dhambi ya uzinzi au kufumaniwa inasameheka pia mtuhumiwa akitubu.
 
lakini tumekubaliana ndoa ni agano moja nafikiri
Ndiyo ni agano, lakini mmoja akitangulia agano linakuwa limevunjika ndio sababu Maandiko yanasema "ni mwili mmoja mpaka kifo kiwatenganishe."
 
Ndiyo ni agano, lakini mmoja akitangulia agano linakuwa limevunjika ndio sababu Maandiko yanasema "ni mwili mmoja mpaka kifo kiwatenganishe."
mfano nikiamua kusema natendana na wewe kutokana na kifo cha kiimani juu yako nitakua nakose
 
Asante kwa maoni yako. Kwanza nikutahadharishe: ChatGPT, haijui kila kitu. Majibu inayokupa yanatokana na kukusanya mafundisho ya aina nyingi sana. Hivyo ukiitegemea yenyewe tu ikupe majibu, unaweza ukapotoka.

Katika andiko ulilonukuu, neno lililotumika kwa Kigiriki ni "porneia." Hilo katika muktadha wa Wayahudi wa karne ya kwanza, lilimaanisha tendo la ngono kabla ya ndoa au kuvunja ahadi ya uchumba, kama ilivyokuwa kwa Yusufu na Mariamu (Mathayo 1:18-19). Hapo, Yusufu alitaka kumwacha Mariamu kwa siri kwa sababu alidhani alifanya uasherati kabla ya kuishi naye kama mume na mke.

Kwa kigiriki, "Uzinzi" ni "moicheia": ni tendo la mtu aliye kwenye ndoa kufanya ngono na mtu mwingine. Kwa hiyo kusema "uzinzi umo ndani ya uasherati" sio tafsiri ya Biblia. Hiyo ni nadharia ya watu.

Katika orodha ya watakaotupwa motoni, wazinzi, watukanaji, wezi, waongo... wote wapo kundi moja. Hivyo mke wako akifanya uzinzi, ni dhambi inayosameheka; "Msamehe hata saba mara sabini." (Mathayo 18:21–22). Maandiko yanasema ukimwacha ukae hivyohivyo usioe.

Kumbuka Yesu alimsamehe yule mwanamke aliyekamatwa katika uzinzi. Wewe ni nani unayekataa kumsamehe mke wako akifanya uzinzi na kuomba msamaha?

Katika 1 Wakorintho 7:12–13 Maandiko yanasema mke asiyeamini hapaswi kuachwa. Kama asiyeamini hapaswi kuachwa, sembuse mke aliyefanya uzinzi na kutubu?

Usisahau talaka zilitolewa kwa sababu ya ugumu wa mioyo ya watu. Wewe ukitoa lalaka ina maana una moyo mgumu.

Ndoa ni agano takatifu, sio mkataba wa kuvunja kwa kosa moja.

Kumbuka pia Yesu alitusamehe dhambi zote pamoja na uzinzi. Hivyo tusiposamehe na sisi hatutasamehewa. Naamini Maandiko hayo unayajua.

Hivyo ndugu yangu, kama umemwacha mke wako wa kwanza, omba Mungu akuwezeshe mrudiane naye. Vinginevyo huyo mke unayeishi naye sasa sio wako. Unafanya uzinzi.
Yani ushasema ChatGPT inatoa majibu kutokana na mafundisho ya aina nyingi afu unasema nisiitegemee😂 kwamba wewe una knowledge kubwa kuliko ChatGPT au,? jipe moyo nenda kamcheat mumeo afu utegemee kwamba atakusamehe labda awe zwazwa Hakuna kitabu chochote katika dini yoyote kinachoomesha kwamba mwanamke msaliti ni wa kuishi nae, Katika uislamu ndo kabisa imehalalishwa mwanamke msaliti ni wa kuuwawa katika ukristo hakuna andiko linaloonesha mwanaume aliesalitiwa akaamriwa asamehe na ndo maana Tanaka iliwekwa kwa sababu ilionekana kuwa ni kosa gumu kwa mwanaume kulisamehe wala usisingizie ni ugumu wa mioyo NO kumsaliti mumeo ni kosa halali ambalo linamruhusu akupe Talaka kwa mujibu wa maandiko.

Though Unachokifanya wewe ni kutumia Bible kuhalalisha usaliti wako then uexpect kwamba mwanaume atakusamehe, Bible hiyohiyo ambayo ukiisoma inakwambia usile nguruwe mbona mnakula,,? Bible hiyohiyo inayoonesha manabii walioa Wanawake zaidi ya mmoja but now wanaume wakitaka kuoa wanawake wawili au zaidi kama enzi za manabii povu linawatoka kama kweli mnafatisha biblia mbona suala hili huwa mnalikataa,,
Tafsiri Bible kwa unavyojua wewe ila Mwanaume timamu kamwe kamwe hawezi kuishi na mwanamke MALAYA📌
 
A
Hiyo ni amri ya Agano la Kale. Yesu alipokuja alituambia ndugu yako akikukosea msamehe hata saba mara sabini. Hivyo dhambi ya uzinzi au kufumaniwa inasameheka pia mtuhumiwa akitubu.
Kabla ya kuanza kulaumu kuwa mwanaume ana moyo mgumu anaenda kinyume na maandiko kwa kutokukusamehe jilaumu wewe kwanza kwanini ulienda kinyume na maandiko kwa kucheat
 
Yani ushasema ChatGPT inatoa majibu kutokana na mafundisho ya aina nyingi afu unasema nisiitegemee😂 kwamba wewe una knowledge kubwa kuliko ChatGPT au,?
Narudia tena: ChatGPT imekusanya mafundisho ya aina nyingi. Mengine ni mafundisho potofu. Hivyo unapoitumia, changanya na akili zako. Wenyewe wameandika chini ya app kwamba inakosea!
jipe moyo nenda kamcheat mumeo afu utegemee kwamba atakusamehe labda awe zwazwa Hakuna kitabu chochote katika dini yoyote kinachoomesha kwamba mwanamke msaliti ni wa kuishi nae,
Na mwanaume msaliti je? Apewe talaka? Maandiko yanasema ndugu yako akikukosea hata saba mara sabini msamehe. Hapo haijatajwa kwamba kuna makosa ya kusamehe na mengine sio ya kusamehe. Mbona sisi Yesu alitusamehe makosa yote? Tujifunze kwake. Kumbuka usiposamehe na wewe hutasamehewa.
Katika uislamu ndo kabisa imehalalishwa mwanamke msaliti ni wa kuuwawa
Wewe unasimama wapi kwenye imani yako? Mshika mbili moja humponyoka
katika ukristo hakuna andiko linaloonesha mwanaume aliesalitiwa akaamriwa asamehe na ndo maana Tanaka iliwekwa kwa sababu ilionekana kuwa ni kosa gumu kwa mwanaume kulisamehe wala usisingizie ni ugumu wa mioyo NO kumsaliti mumeo ni kosa halali ambalo linamruhusu akupe Talaka kwa mujibu wa maandiko.
Ugumu wa mioyo ni sababu aliyoitoa Yesu mwenyewe, sio mimi
Though Unachokifanya wewe ni kutumia Bible kuhalalisha usaliti wako then uexpect kwamba mwanaume atakusamehe, Bible hiyohiyo ambayo ukiisoma inakwambia usile nguruwe mbona mnakula,,?
Amri ya kutokula nguruwe ni ya Agano la Kale. Yesu alipokuja alileta Agano Jipya au amri na sheria mpya zinazoturuhusu kula nguruwe.
Bible hiyohiyo inayoonesha manabii walioa Wanawake zaidi ya mmoja but now wanaume wakitaka kuoa wanawake wawili au zaidi kama enzi za manabii povu linawatoka kama kweli mnafatisha biblia mbona suala hili huwa mnalikataa,,
Hao unaowataja kwamba walioa wake wengi, waliishi kwa kufuata amri na sheria za Agano la Kale. Kama nilivyokuambia hapo juu, Yesu alileta Agano Jipya. Hivyo kwa sasa tunaishi nyakati za Agano Jipya. Agano jipya haliruhusu mtu kuoa mke zaidi ya mmoja
Tafsiri Bible kwa unavyojua wewe ila Mwanaume timamu kamwe kamwe hawezi kuishi na mwanamke MALAYA📌
Kama unaona ni malaya, na hutaki kumsamehe, unaweza kumwacha. Lakini ukimwacha, huruhusiwi kuoa mwingine. Kaa hivyo hivyo ulivyo mpaka kifo kiwatenganishe. Ukioa mwingine unazini. Na wazinzi hawataurithi ufalme wa Mungu.
 
Naongea na wewe uliyeachana na mwenzi wako wa kwanza na kuoa au kuolewa tena. Nakujulisha kuwa huyo mke/mume uliye naye sasa sio wako mbele za Mungu — unazini.

Katika dunia ya sasa ambapo talaka na ndoa ya pili au ya tatu zinaonekana kama jambo la kawaida, ni muhimu sana kwa watu wanaotamani kwenda mbinguni kufahamu msimamo wa Mungu juu ya ndoa, talaka, na kuoa au kuolewa tena baada ya talaka.

1. Ndoa ni agano la milele, sio mkataba wa muda
Biblia inafundisha kuwa ndoa ni muungano wa kiroho na kimwili uliowekwa na Mungu mwenyewe.
Katika Mwanzo 2:24 tunaambiwa:
“Kwa hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, naye ataambatana na mkewe, nao watakuwa mwili mmoja.”

Muungano huu wa “mwili mmoja” si wa muda, ni wa kudumu mpaka kifo kitakapowatenganisha. Hili linasisitizwa tena na Yesu Kristo katika Mathayo 19:6
"Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe..”

Kwa hiyo, talaka haibatilishi kile Mungu alichokiunganisha. Ingawa mwanadamu anaweza kutoa talaka, mbele za Mungu bado mme na mke wa kwanza wanahesabika kuwa wameunganishwa.

2. Talaka haitoi ruhusa ya kuoa au kuolewa tena
Yesu mwenyewe alizungumzia jambo hili kwa uwazi sana. Katika Luka 16:18 anasema:
"Kila amwachaye mkewe na kumwoa mke mwingine anazini; naye amwoaye yeye aliyeachwa na mumewe anazini.”

Hapa tunaona wazi kuwa kuoa au kuolewa tena baada ya talaka ni uzinzi. Kwa lugha nyingine, kama ulimwacha mume au mke wako wa kwanza, ukaoa au kuolewa tena, basi huyo uliye naye sasa sio wako. Mbele za Mungu unahesabika unaishi katika uzinzi.

3. Talaka iliruhusiwa kwa sababu ya ugumu wa mioyo — sio mpango wa Mungu
Yesu alipoulizwa kuhusu talaka, alisema katika Mathayo 19:8:
“... Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu ya ugumu wa mioyo yenu. Lakini tangu mwanzo haikuwa hivyo.”

4. Hatari ya kuishi katika uzinzi
Wale wanaoishi na wake au waume wa ndoa ya pili, wanaishi katika hali ya dhambi — yaani uzinzi wa kudumu. Na Biblia inasema wazi katika 1 Wakorintho 6:9-10:
"Au hamjui ya kuwa wadhalimu hawataurithi ufalme wa Mungu? Msidanganyike; waasherati hawataurithi ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wafiraji, wala walawiti.”

Hili ni onyo kali. Kama unaendelea kuishi na mke au mume asiye wako bila kutubu na kurekebisha, una hatari ya kupoteza uzima wa milele.

5. Suluhisho: Tubu na umrudie mme au mke wako wa kwanza
Suluhisho sio kuhalalisha mahusiano uliyo nayo sasa. Suluhisho ni kutubu kwa dhati, kujitenga na hali ya uzinzi, na kumrudia mwenzi wako wa kwanza. Kama huwezi kumrudia huyo wa kwanza, ukae hivyo hivyo peke yako.
Katika 1 Wakorintho 7:10-11, Paulo anaandika:
“Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.”

Biblia haiungi mkono ndoa ya pili baada ya talaka, bali inashauri ama kubaki bila kuolewa/kuoa au kumrudia mwenzi wa kwanza.
Kwa maana hiyo hakuna mwenye mke wake kwa sababu kila uliye naye alishawahi kuwa wa mwingine.
 
Kwa maana hiyo hakuna mwenye mke wake kwa sababu kila uliye naye alishawahi kuwa wa mwingine.
Mke anayetambuliwa kwamba ni wako ni yule wa kwanza. Wote waliowaacha wake zao wa kwanza wakaoa wengine, hao wake sio wao. Wanazini.

Sio kweli kwamba hakuna mwenye mke wake. Wapo wengi. Katika makanisa ya watu waliookoka, Wachungaji kabla ya kufunga ndoa, wanahakikisha kwanza kwamba kijana hajaoa na binti hajaolewa
 
Watajuaje kama hajawahi kuwa na mpenzi?
 
Narudia tena: ChatGPT imekusanya mafundisho ya aina nyingi. Mengine ni mafundisho potofu. Hivyo unapoitumia, changanya na akili zako. Wenyewe wameandika chini ya app kwamba inakosea!

Na mwanaume msaliti je? Apewe talaka? Maandiko yanasema ndugu yako akikukosea hata saba mara sabini msamehe. Hapo haijatajwa kwamba kuna makosa ya kusamehe na mengine sio ya kusamehe. Mbona sisi Yesu alitusamehe makosa yote? Tujifunze kwake. Kumbuka usiposamehe na wewe hutasamehewa.

Wewe unasimama wapi kwenye imani yako? Mshika mbili moja humponyoka

Ugumu wa mioyo ni sababu aliyoitoa Yesu mwenyewe, sio mimi

Amri ya kutokula nguruwe ni ya Agano la Kale. Yesu alipokuja alileta Agano Jipya au amri na sheria mpya zinazoturuhusu kula nguruwe.

Hao unaowataja kwamba walioa wake wengi, waliishi kwa kufuata amri na sheria za Agano la Kale. Kama nilivyokuambia hapo juu, Yesu alileta Agano Jipya. Hivyo kwa sasa tunaishi nyakati za Agano Jipya. Agano jipya haliruhusu mtu kuoa mke zaidi ya mmoja

Kama unaona ni malaya, na hutaki kumsamehe, unaweza kumwacha. Lakini ukimwacha, huruhusiwi kuoa mwingine. Kaa hivyo hivyo ulivyo mpaka kifo kiwatenganishe. Ukioa mwingine unazini. Na wazinzi hawataurithi ufalme wa Mungu.
Hizi sheria mpelekee Yesu, Narudia usije ukamcheat mmeo then ukamletea hizi bible verse, mwenye uwezo wa kusamehe hizo 7×70 ni Mungu na Yesu mwenyewe kwa sababu hakuwa binadamu wa kawaida kama sisi, So usitegemee utamcheat mwanaume then akiwa na akili zake timamu akusamehe, Yani uombwe namba utoe uanze kutongozwa, unifiche jamaa akubembeleze na still unampa time unamsikiliza mpaka unakubali kwa akili zako timamu mnaanzisha mahusiano ya siri ambayo mumeo hayajui, mnapanga siku ya kukutana, mnakutana, mnaenda lodge au kwa jamaa mnapika mnakula mnavua nguo ukiwa na akili zako timamu, Unagongwa then kesho na kesho kutwa mnarudia tena mpaka siku Mumeo anakuja anagundua then unataka umletee hizi Bible verses akuelewe,,,, Mungu mwenyewe alijua kuna vitu ambavyo kwa mtu mwenye uelewa havisameheki na akaweka talaka alikua na maana yake,
Na kama ingekuwa hizi bible hamzingatii agano la Kale basi Biblia ingeanzia agano jipya bila kuwa na agano la Kale
No way ukimcheat mume wako Talaka inakuhusu na ana haki ya kuoa mwanamke mwengine
Yesu mwenyewe alisema Mtu akimuacha mkewe isipokuwa yani isipokuwa kwa sababu ya uasherati basi ukioa mwengine unazini, mpaka hapo Ukilazimisha mwanaume akae na mwanamke malaya Cheater utakuwa haupo timamu

Pole sana. Naona unajifariji tu. Haya maneno aliambiwa nani
Mt 18:22
Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
USIPOSAMEHE NA WEWE HUTASAMEHEWA, HIVYO SAHAU KUINGIA MBINGUNI, BADALA YAKE JIANDAE KUCHOMWA MOTONI MILELE😳
 
Kama unamaanisha mmoja aliyefariki, basi huyo aliyebaki yuko huru kuoa au kuolewa

Na mwanaume msaliti je? Apewe talaka? Maandiko yanasema ndugu yako akikukosea hata saba mara sabini msamehe. Hapo haijatajwa kwamba kuna makosa ya kusamehe na mengine sio ya kusamehe. Mbona sisi Yesu alitusamehe makosa yote? Tujifunze kwake. Kumbuka usiposamehe na wewe hutasamehewa.
Unajua maana ya kusamehe,,? Msamaha ni mtu kuacha kama alikuwa na kisasi na wewe basi anaachia but haimaanishi kuwa ni lazima aendelee kuwa na wewe,, naweza nikakusamehe but sitaki tena kuwa na ukaribu na wewe coz unanikumbusha maumivu so utamlazimisha mumeo akusamehe then arudi kama zamani, hata Adam na Hawa walipotenda dhambi bustani ya Eden Mungu aliwasamehe but hakuwaruhusu tena wabaki bustanini je utasema basi Mungu hakuwasamehe,, Big No, usimpangie mtu msamaha Mwanaume anaweza akakusamehe akaachia but asitake tena kuwa karibu na wewe coz itamrudisha nyuma na huwezi kumlaumu kwamba hajakusamehe akati ulifanya kosa kwa makusudi
Pili Biblia imefundisha tusameheane but haijampangia wala kumlazimisha mtu asamehe kosa but Mtu atasamehe kwa ajili ya faida zake binafsi na sio za kwako wewe mkosaji
Kingine Biblia imetaka msamaha kwa ndugu ikiwa na maana kwa yeyote anaekukosea unapaswa kumsamehe but Ndoa ni zaidi ya undugu ndoa ni agano so ukivunja agano usitegemee msamaha kirahisi na hata ukipata msamaha haikupi guarantee kwamba ndo tuwe kama zamani NO, Mtu anaweza akakusamehe ili kuweka Amani but haitamzuia kukuwekea mipaka, kukuweka mbali na yeye au kukutoa kabisa kwenye circle yake, kwa kifupi MTU ANAWEZA AKAKUSAMEHE BUT HUNA MAMLAKA YA KUMPANGIA NAMNA YA KUJILINDA ILI ASIWE DISAPPOINTED TENA NA WEWE
Na cha zaidi Biblia yenyewe imehalalisha ndoa kuvunjika kwa ajili ya Cheating ya mwanamke, Mwanaume anaweza akasamehe ndoa iendelee but hata akihitaji kuvunja ndoa still Biblia imempa uhalali kwa kosa hilo, unachokifanya wewe ni kutaka kugeuza maneno ya kiswahili na kuweka maana unazozijua wewe
Na ukiulizia kuhusu mwanaume msaliti atahukumiwa na Mungu, Biblia imetuhasa wanaume kuwapenda Wake zetu na kama tukiwatenda kwa ubaya Mungu mwenyewe atatuhukumu.
Biblia imemuweka mwanamke chini ya mwanaume na imemuweka mwanaume chini ya Mungu sasa ukitaka usawa mwanaume ahukumiwe kama wewe hapo utajiumiza mwenyewe📌
 
Pole sana. Naona unajifariji tu. Haya maneno aliambiwa nani
Mt 18:22
Yesu akamwambia, Sikuambii hata mara saba, bali hata saba mara sabini.
USIPOSAMEHE NA WEWE HUTASAMEHEWA, HIVYO SAHAU KUINGIA MBINGUNI, BADALA YAKE JIANDAE KUCHOMWA MOTONI MILELE😳
Narudia tena Hata Mungu aliwasamehe Adam na Eva but still aliwatoa bustanini, so Mwanaume anaweza akakusamehe but hauwezi ukampangia namna ya kujilinda baada ya kukusamehe
Na kingine bliblia hiyohiyo Yesu amesema “Nawaambia ninyi, Kila mtu atakayemwacha mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, akaoa mwingine, azini.” Mathayo 19:9
It means mwanaume yeyote ukimuacha MKE isipokuwa kwa sababu ya Uasherati (ni mzinzi, malaya, Cheater) basi ukienda kuoa mwingine unazini,
Mke anaweza akawa ana dharau, kiburi, maneno, roho mbaya but mwanaume anapaswa kumvumilia kwa madhaifu yake but akivuka mipaka ya hapo akaenda kufanya uasherati basi imehalalishwa kumuacha/talaka
So acha kutumia vifungu vya Biblia kumfunga mwanaume katika mateso ya mwanamke msaliti📌 Mwanaume akikupa talaka ni haki yake anaweza akakusamehe na still akakupa talaka na hiyo ni halali kwake huwezi kumpangia namna ya kureact📌 Hata wewe kuna watu waliokukosea ambao umewasamehe but huna ukaribu nao tena, Nafikiri nimeeleweka
 
Back
Top Bottom