Je, unajua kwamba huyo mke/mme uliye naye sasa sio wako?

nikiona mtu anatafuta mwenza humu numuona dishi limeyumba kabisa,
 
Maana ya porneia katika Kigiriki cha Agano Jipya ni uasherati. Uasherati ni mahusiano ya kimwili kabla watu hawajafunga ndoa
Sasa hebu eleza ni kwa namna gani watu waliopo kwenye ndoa wanaweza kufanya uasherati, au ni namna gani uasherati unaweza kuwahusu watu walio kwenye ndoa mpaka wakaachana, ilhali uasherati ni kwa wale kabla ya ndoa
 
Sasa hebu eleza ni kwa namna gani watu waliopo kwenye ndoa wanaweza kufanya uasherati, namna gani uasherati unaweza kuwahusu watu walio kwenye ndoa mpaka wakaachana, ilhali uasherati ni kwa wale kabla ya ndoa
Ukisoma Biblia kwa makini utagundua kuwa nyakati za mwanzo mtu akiishatoa posa kwa mchumba wake, hata kabla hawajaoana, walikuwa wanaitwa mtu na mkewe. Soma Kum 22:23-24 na Mt 1:18-20. Katika hali hiyo ya uchumba, kama "mke" amefumaniwa amefanya uasherati na mwanaume mwingine tofauti na huyo waliyepeana posa, akapata mimba, ilikuwa halali kumwacha kwakuwa anaonyesha wazi sio mwaminifu. Ndiyo sababu Yusufu alitaka kumwacha Mariamu akidhani amefanya uasherati. Hata leo mambo yako hivyohivyo. Kuna watu wanakaa katika uchumba miaka hata miwili bila kukutana kimwili. Ikitokea mke amevunja agano la kuoana, akalala na mwingine, huyo mme yuko huru kumwacha. Huo ndio uasherati unaozungumzwa katika Kitabu kile. Sio uzinzi.
 
Depal Ni Kwamba ukimuacha ukae hivyo hivyo. Mi sifagilii kwakweli🤔
 
Hata sasa ukimtolea mwanamke mahari, technically anakua ni mkeo, hivyo mtu anayetoka nae anakua amemchukua mkeo. Huyu mwanamke anaachwa kwa sababu ya uzinzi na sio uasherati. Nimesoma hiyo Mt 1:18-20 ila sijaona mahali ambapo inasemwa Yusufu alitaka kumuacha Mariam sababu ya kudhani amefanya uasherati.

Mwaka 2011 kuna siku nilikuwa nasikiliza Radio Maria, nikamsikia Padri mmoja akieleza maana ya kuachana kwa uzinzi, akaeleza kuwa ni pale waliooana wanapogundua kuwa ni ndugu ambao uhusiano wao kibiblia umekatazwa, hapo wataachana, na ndio kilichomaanishwa. Ilikuwa ndio tafsiri ya huyo Padri akirejea maandiko ya kiyunani.

Mimi kwa tafsiri yangu, uzinifu unaozungumzwa ni wa mtu kuchakatwa nje. Huyu imeruhusiwa kumuacha.

Hata hivyo, hujaeleza kuhusu mwanamke ambaye ana tofauti ya imani na mumewe, si ameruhusiwa kuachwa? 1 Kor 7:15
 
We mbona mchumba wako aliyekutoa b...... hajakuoa ukaolewa na kijana wa watu mcha Mungu
 
"kila amwachae mwenzi wake isipokua kwasababu ya zinaa na kumuoa mwingine azini"

Isipokua isipokua soma maandiko vizuri!!

Yupo hapa kasingizia wanaume watatu ujauzito yaani mumewe,kijana na mheshimiwa yaani alikua Hana uhakika was aliempa mimba kati ya watatu hai akabaki wote anawaambia mtoto ni wao!!

Talaka au kuachana kunaruhusiwa!!

Hubirini kweli ilivyo acheni kufundisha uongo!!
 
Amen 🙏
 
We mbona mchumba wako aliyekutoa b...... hajakuoa ukaolewa na kijana wa watu mcha Mungu
Waefeso 5:3-4
Lakini uasherati usitajwe miongoni mwenu kamwe, wala uchafu wa aina yoyote, wala tamaa, kwa sababu mambo haya hayastahili miongoni mwa watakatifu wa Mungu. Wala pasiwepo mazungumzo machafu ya aibu, au maneno ya upuzi au mzaha, ambayo hayafai, badala yake mshukuruni Mungu.
 
Amen na samahani kwa kukukosea na sitorudia kamwe
 
Ila hiyo profile picture yako inaweza kukufanya ukose mke mwema.
Your profile picture is your first introduction...
How you present yourself tells a lot about you
Naibadili maana siko tayari kukosa mke mwema.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…