Je, unajua kwamba huyo mke/mme uliye naye sasa sio wako?

nikiona mtu anatafuta mwenza humu numuona dishi limeyumba kabisa,
Umenena vema ndugu yangu Zzulu
Hakika, mwenza mwenye busara mtu hupata kutoka kwa Bwana, sio humu JF. (Mithali 19:14)
 
Maandiko hayo hayo yanasema mwanamke mpumbavu anastaili talaka
 
Pana watu wanatabia ngumu kuishi nao kwa waenda mbinguni kipi bora ubaki nae ukose ufalme au uachane nae uupate.
Maana hata Mungu tu alishindwana na shetani akamtimua,sembuse wewe mwanadamu.
 
Inaonekana wewe Setfree ni mzinzi ndiyo maana unahalalisha msamahakwa mzizi
 
Pia kile swali ka mjane au mgane hatujapata maelezo kutokan na maandiko
 
Mtu akisoma mada zako anaweza kudhani wewe huna dhambi kama wale wazee na maserafi.
 
Uasherati ni kufanya ngono nje ya ndoa ilhali mume wako yupo
Amfanya kuwa mzinzi- Mzinzi ni mtu anaefanya ngono ilhali hayupo kwenye ndoa
So "Lakini mimi nawaambia, Kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi; na mtu akimwoa yule aliyeachwa, azini." Maana yake ni kwamba Valid reason ya kumuacha Mkeo ni awe muasherati yaani anafanya ngono nje akati mpo kwenye ndoa ila kama sababu sio hiyo (Uasherati) bhasi huruhusiwi kumuacha Mkeo coz utamfanya awe mzinzi (akafanye ngono nje ya ndoa ilhali ulikuwa na ndoa nae na umeivunja) kwahiyo hapo wewe umefasili vibaya maandiko, Biblia inahalalisha wazi kabisa 100% kuachana na mwanamke wako kama ana tabia za Uasherati (kufanya ngono nje ilhali umemuoa) soma na uelewe, usikurupuke
 
Yusufu aliambiwa na malaika kwamba usimuache Mariam mkeo. Biblia inamtambua mwanamke/mwanaume walioposana kama mke/mume, tendo la ndoa ndo linalothibitisha ndoa na kuifanya kuwa halali.

Kwahiyo watu wasidhani kuwa mtu akitoka nje ya ndoa basi Yesu aliruhusu talaka itolewe. Mbaya zaidi hata makanisa mengi kwa sasa yameingia ktk huu mtego wa Ibilisi.
 
Unapotosha mtu wa Mungu, mleta mada yupo sahihi kabisa.
 
Sheria ya Bwana ni kali sana na isichezewe kama kijitabu kidogo cha katiba,mtii Bwana ili mema yawafuate
 
Unapotosha mtu wa Mungu, mleta mada yupo sahihi kabisa.
Hakuna usahihi hapo HAKUNA MAANDIKO ya kitabu chochote cha dini yanayoruhusu uendelee na mwanamke ambae ni muasherati📌
Unaelewa maana ya "Lakini mimi nawaambia, kila mtu amwachaye mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, amfanya kuwa mzinzi" Yaani kumuacha mkeo kwa sababu zingine ni ngumu ila isipokuwa labda awe muasherati yani ametoka nje ya ndoa hapo ni ruksa kumuacha elewa "kila mtu amwachaye mkewe ISIPOKUWA KWA SABABU YA UASHERATI ina maana kama sababu sio uasherati bhasi hutakiwi kumuacha mkeo, hizo story zingine achaneni nazo Hakuna maandiko matakatifu katika Quran na bibke yanayoruhusu kuishi na mwanamke msaliti HAKUNA Mke akishatoka nje ya ndoa hiyo ni tiketi moja kwa moja, eleweni maandiko acheni kufocus kwenye kutetea wanawake
 
Agano la Kale.
Agano Jipya ni mme mmoja, mke mmoja
Haijalishi akiwa mpumbavu anastaili talaka, upumbavu huu ndo unawafanya wanawake wengi wa Kikristo hawajitambui uutumia kuwavuruga wanaume
 
Mwanamke mchawi,mzinzi na muuaji haki yake kupewa talaka na unaruhusiwa kuoa mwingine.
NURU na Giza hawezi kaa nyumba moja.
Kwa maana atakuletea magonjwa, watoto wa nje, kifo, uchafu wa kiroho.
 
Unachoshindwa wewe kuelewa ni kufananisha situation ya Yusufu na sisi Wanadamu wa kawaida
1. Mariam alipata Mimba kwa uwezo wa roho mtakatifu unahisi kwanini Mungu hakutaka mariam akaingiliwe na mwanaume mwengine then amwambie Yusufu abaki nae,? Mariam hakupata Mimba kwa kuingiliwa na mwanaume so hata Yusufu alipotaka kumuacha kwa kuhisi amesalitiwa ilikuwa ni halali na ndo maana akaletewa maono kuwa asimuache mkewe na hapo ndo akaamini akaendelea na mkewe.
Wewe na Mkeo leo hii Mkeo akuletee mimba ya nje au ugundue mkeo ametoka kubatuliwa nje kaja kwenye nyumba yako utamuelewa,? Nitajie mstari 1 katika bible au Quran unaohalalisha kuwa ndoa haipaswi kuvunjwa endapo Mke atafanya usaliti,, HAKUNA
 
Uasherati ni kwa watu ambao hawajaoana kama ilivyokuwa kwa Yusufu na Mariamu. Yusufu alitaka kumwacha na ilikuwa halali kwake lakini akaambiwa asimwache kwa sababu mimba yake ilipatikana kwa uwezo wa Roho Mtakatifu.

Kwa waliooana, neno linalotumika ni uzinzi. Ukimwacha mke wako kwa sababu ya uzinzi, huruhusiwi kuoa mwingine
 
Kuna kitu hujakielewa Biblia ni ngumu sana kuichambua ukiisoma kama gazeti,
Ambacho hukijua ni kuwa Uzinzi upo ndani ya Uasherati.
Uasherati ni ngono yoyote ile isiyo halali yani Ushoga,Uzinzi, Usagaji yote hayo yapo ndani ya neno "Uasherati"
Kwa kifupi Nikisema uasherati it means nimejumuisha hayo mauchafu yote yanayohusisha ngono isiyo halali kwa sababu ngono halali pekee ni ile mnayofanya watu ambao mmeoana📌

So Biblia inaposema ukimuacha mkeo isipokua kwa sababu ya uasherati (either ni mzinzi au msagaji) unamfanya kuwa mzinzi It means kwamba Uasherati ni Mke kwenda kuzini na mwanaume tofauti na mume wake au kwenda kufanya ngono yoyote isiyo halali (kumbuka uzinzi ni aina ya uasherati) basi huyo ni wa kuachwa📌

So Bible iliposema Ukimuacha ISIPOKUA kwa sababu ya uasherati (Mkeo ni either ni mzinzi au msagaji) basi unamfanya kuwa mzinzi ikiwa na maana kwamba kama mkeo si mzinzi hupaswi kumuacha kwa sababu utamfanya kuwa mzinzi kweli.
Au kwa kiswahili rahisi ni sawa na kusema "ukimuacha mkeo isipokua kwa sababu ya uasherati unamfanya kuwa muasherati" kwamba hakua muasherati ila umemuacha kwa sababu zingine ambazo haziruhusiwi basi unamfanya akawe muasherati kweli.

Hakuna maandiko katika Biblia au Quran yanayomtaka mwanaume kuishi na mwanamke muasherati (Mzinzi, msagaji) Piga uwa achana na maandiko tu Mungu mwenyewe kakataa kuishi na mzinzi hakuna dhambi mbaya kama mwanamke kutoka nje ya ndoa ANAACHWA hapohapo yani hakuna utetezi hapo📌 tena kwa waislamu ndo wapo direct kabisa maana sheria zao zinawataka waasherati/wazinzi wauwawe📌
 
Jambo unaolileta linahitaji upeo mpana kulijadili, biblia kuielewa ni ishu, ilivyoandikwa ni tofauti na maana yake ndio maana ukiielewa biblia utajiri unakuja chap, i.e Mwamposa na tb joshua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…