Je unajua ni kwanini siku ina saa 24?

Lukansola

JF-Expert Member
Joined
Sep 5, 2010
Posts
5,435
Reaction score
1,604
Kama unajua tafadhali nielimishe, nimeijiwa tu na hili wazo from nowhere nikiwaza ingekuwaje siku ingekuwa na saa 48 kwa mfano; ningeweza kuwa na muda zaidi?

Si nadra siku kuisha ukiwa na viporo vya majukumu...

Anyways back to the topic, ni nani aliamua siku iwe na saa 24 tu?
 
Na ndo tungekufa tukiwa na umri mchache. Bora ingekua cku ina saa 12 tu.
 

Every thing is manmade Lukansola, unapozungumzia hizo saa 24 bado pengine ni saa 48, tunapozungumzia siku saba labda pengine ni miaka saba, hizi ni taratibu tu tumezikuta ziko hivyo na zimepenya vyema kwenye bongo na akili zetu mpaka tunaziona ni halisi.

Kwenye Bible kuna maneno yanasema kwa Mungu siku moja ni kama miaka 1000 na miaka 1000 ni kama siku moja...! Its a confusing phenomenon usipoielewa lakini iko hivi mchukue sisimizi, kinyonga panya mbwa binadamu simba na kiboko, watembee au wakimbie kilometa kumi tu, sisimizi au kinyonga wanaweza kufa kabla ya kumaliza safari ni mwendo mrefu mno kwao.

Hao waliobaki kila mtu atamaliza kwa muda wake kutegemeana na uwezo wake, lakini wengine watamaliza wakiwa hoi sana lakini wengine wataona ni kama ndo safari imeanza kwakuwa kwa siku wanaenda zaidi ya Mara kumi ya huo mwendo
 
Last edited by a moderator:
na kwa zamani siku ilikuwa ina timia pale jua linapozama.
Ref.
Alikufa ijumaa saa 9 akafufuka j'pili alfajiri ni masaa mangapi?

confusion depertment.🙂
 
Lukansola hata kama siku ingekuwa na saa 48, mambo yangekuwa yale yale, mimba ungebebwa miezi 18, labda tofauti ni kwamba watu waliokufa juzi juzi wangekuwa bado wapo na wengi angekuwa hajazaliwa!

Umechemka Wile GAMBA, kama ni mimba; kwa saa 48 kwa siku ingekuwa miezi minne na nusu au?
 
Last edited by a moderator:
na kwa zamani siku ilikuwa ina timia pale jua linapozama.
Ref.
Alikufa ijumaa saa 9 akafufuka j'pili alfajiri ni masaa mangapi?

confusion depertment.🙂

Hakuna, wakati anakufa kulikuwa hakuna Ijumaa wala jumapili!! Kasome tena kiongozi
 
Hee kwani siku ndo indetermine kufa kwa mtu,au kufa kwa mtu kunadetemine siku..willy gamba haupo sahihi
 
Mimi baada ya kukosa jawabu hata ya kubahatisha, niliuliza katika Google, "Why a day has 24 hours?" na nimepata jawabu za kunishawishi niridhike. Ninawashauri wale walio wadadisi watupie jicho huko.
 
Qur-an inasema allah amekuumbieni usiku na mchana ili mpate kujua idadi ya miaka( miezi,masiku,masaa) na hesabu(ahadi mlizowekeana). Kwa kuwa mchana unadumu kwa takriban masaa 12, na usiku unadumu kwa takriban masaa 12. Ndo tunapata masaa 24 ya siku. Allah knows best.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…