Inaonekana wewe umeingia katika hizi dini juzi juzi. Punguza speed dada yangu.Je, ni lazima mtu abatizwe katika maji mengi?
Ukisoma Biblia kwa makini utagundua kuwa ubatizo ulifanyika mahali penye maji mengi, kuthibitisha kuwa mtu anatakiwa kuzamishwa majini anapobatizwa.
Haya ni baadhi ya Maandiko yanayoonyesha kuwa ubatizo ulifanyika katika maji mengi
Yohana 3:23
"Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa."
Mdo 8:36-38
"Walipokuwa bado wanaendelea na safari, walifika mahali penye maji, na huyo ofisa akasema, Mahali hapa pana maji; je, kuna chochote cha kunizuia nisibatizwe? Filipo akasema, Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa. Naye akajibu, Naam, ninaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu. Basi, huyo ofisa akaamuru lile gari lisimame; na wote wawili, Filipo na huyo towashi wakashuka majini, naye Filipo akambatiza."
Wakashuka majini maana yake, maji yalikuwa mengi.
Sikosoi wanaobatizwa kwa maji mengi wala wale wanaobatizwa kwa maji kidogo mradi tu wanaamini.Jambo la mhimu ni kwamini kwamba Yesu kristo ni Bwana na mwokozi wako.Maji ni ishara tu.Je, ni lazima mtu abatizwe katika maji mengi?
Ukisoma Biblia kwa makini utagundua kuwa ubatizo ulifanyika mahali penye maji mengi, kuthibitisha kuwa mtu anatakiwa kuzamishwa majini anapobatizwa.
Haya ni baadhi ya Maandiko yanayoonyesha kuwa ubatizo ulifanyika katika maji mengi
Yohana 3:23
"Yohana naye alikuwa akibatiza huko Ainoni, karibu na Salimu, kwa sababu huko kulikuwa na maji tele; na watu wakamwendea, wakabatizwa."
Mdo 8:36-38
"Walipokuwa bado wanaendelea na safari, walifika mahali penye maji, na huyo ofisa akasema, Mahali hapa pana maji; je, kuna chochote cha kunizuia nisibatizwe? Filipo akasema, Kama unaamini kwa moyo wako wote unaweza kubatizwa. Naye akajibu, Naam, ninaamini kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu. Basi, huyo ofisa akaamuru lile gari lisimame; na wote wawili, Filipo na huyo towashi wakashuka majini, naye Filipo akambatiza."
Wakashuka majini maana yake, maji yalikuwa mengi.
Duh, pole sana BLACKTIGER . Familia walifurahi kweli sasa wanasikitika umerudi nyuma.Aise nakumbuka mara ya mwisho natoka ndani ya maji baada
ya ubatizo nikafunikwa na blanket zito
tukapiga picha na ndugu na familia wakifurah kweli
Hata mimi nilikuwa mbishi kama wewe tungatagaga kabla sijabatizwa katika maji mengi. Ila nilipoujua ukweli, nikakubali kubatizwa kwa kuzamishwa ndani ya mto, kama Yesu alivyobatizwa.Sikosoi wanaobatizwa kwa maji mengi wala wale wanaobatizwa kwa maji kidogo mradi tu wanaamini.Jambo la mhimu ni kwamini kwamba Yesu kristo ni Bwana na mwokozi wako.Maji ni ishara tu.
Nilikuwa mfungwa na sasa nipo huru Siwezi kurudi tena gerezani..Duh, pole sana BLACKTIGER . Familia walifurahi kweli sasa wanasikitika umerudi nyuma.
Huna tofauti na mwana mpotevu katika Luka 15:11-32.
Nakuombea urudi tena kwa Baba..
Wokovu unauona gereza kwa sababu bado unapenda maisha ya dhambi.Nilikuwa mfungwa na sasa nipo huru Siwezi kurudi tena gerezani..
nakushauri na wewe ujitathimini mienendo yako naamini ipo siku utatoka kwenye hilo gereza la giza kama mimi!
So what, pointi yako ni nini?Ubatizo wa maji mengi ni ishara yenye maana sana kiroho. Mtu anapozamishwa ndani ya maji mengi, wakati wa kubatizwa, anaonyesha kuwa utu wake wa kale uliojaa dhambi, umekufa na kuzikwa pamoja na Kristo. Na anapotoka majini, ni ishara ya kufufuka pamoja na Yesu na kuanza maisha mapya ya utakatifu.
Mtume Paulo anasema katika
Warumi 6:4
"Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.”
Ubatizo wa maji mengi ni kitendo cha kuonyesha hadharani kwamba mtu ameacha maisha ya kale, amekubali Yesu Kristo awe Mwokozi wake, na sasa anaishi maisha mapya ya wokovu.
Mada hii inawahusu zaidi Wakristo. Hivyo, kama wewe ni Mkristo, point yangu ni hii:So what, pointi yako ni nini?
Wale waliobatizwa maji machache hawajabatizwa?Mada hii inawahusu zaidi Wakristo. Hivyo, kama wewe ni Mkristo, point yangu ni hii:
Wakati huu tunaposherehekea kufa, kuzikwa na kufufuka kwa Yesu tusisahau kuwa tukio hilo linahusiana pia na ubatizo wa maji mengi. Hivyo mtu akisema anamwamini Yesu Kristo, akubali pia kuonyesha ishara ya kuzikwa na kufufuka na Yesu kwa njia ya ubatizo wa maji mengi. Kuna watu wengi wanamwamini Yesu lakini ukiwaambia wabatizwe katika maji mengi, wanakuwa wabishi. Mada hii imefafanua kwa kina umuhimu wa kubatizwa katika maji mengi.
Umenipata, mkuu?
Sijabisha ndugu nimesema wanaobatizwa kwa maji mengi au madogo ni vema.Kilichozaliwa kwa maji ni maji na kilichozaliwa kwa Roho ni Roho.Unaweza kubatizwa kwenye ziwa lakini bado hujazaliwa Mara ya pili.Makanisa yasiyo ya kisabato hubatiza watu wakiwa bado wananyonya si vema kuwazamisha katika maji mengi kwa usalama wao.Lakini wanapoongezeka umri hupata mafunzo ya kateksim na kubarikiwa baada ya wao wenyewe kumkana shetani.Maji mengi sio kigezo cha kuingia katika ufalme wa MunguHata mimi nilikuwa mbishi kama wewe tungatagaga kabla sijabatizwa katika maji mengi. Ila nilipoujua ukweli, nikakubali kubatizwa kwa kuzamishwa ndani ya mto, kama Yesu alivyobatizwa.
Umefanya vema sana kuchukua hatua hiyo ya kwanza ya kuamini kwamba Yesu Kristo ni Bwana na Mwokozi wako. Hatua ya pili ni kubatizwa(kuzamishwa).
Nafikiri hujaielewa maana ya ubatizo.
Neno "ubatizo" limetokana na neno la Kigiriki "baptizo" linalomaanisha kuzamishwa kabisa. Wengine hawajui hili, hivyo wanatumia maji machache wakidhani inatosha. Lakini kama tulivyoona, Maandiko yanaonyesha wazi kuwa ubatizo wa kweli ni kwa kuzamishwa ndani ya maji mengi (Yohana 3:23, Matendo 8:38). Kitendo hicho ndicho kinachoonyesha kuwa mtu amekufa, amezikwa na kufufuka pamoja na Kristo (Warumi 6:3-4). Hivyo kama kweli umeamua kumfuata Kristo na hujabatizwa katika maji mengi, ukweli umeujua. Fanya haraka ubatizwe katika maji mengi, uitimize haki yote kama Yesu alivyosema.
Vinginevyo Yesu anakushangaa kwanini unamwita Bwana lakini huyatendi aliyoagiza
Luka 6:46-49
“Kwa nini mnaniita, ‘Bwana, Bwana,’ nanyi hamfanyi ninayowaambia? Nitawaonesha jinsi alivyo mtu yule anayekuja kwangu na kusikia maneno yangu na kuyatenda. Yeye ni kama mtu aliyejenga nyumba, akachimba chini sana, na kuweka msingi kwenye mwamba. Mafuriko yalipokuja, mkondo wa maji ukaipiga ile nyumba, lakini haikutikisika, kwa sababu ilikuwa imejengwa vizuri. Lakini yeye anayesikia maneno yangu wala asiyatende, ni kama mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi bila kuweka msingi. Mafuriko yalipoikumba nyumba ile, ikaanguka mara na kubomoka kabisa.”
Kwa hiyo kwenda kanisani kwako ni ujinga? Haya bwana na Mungu akurehemu!Aise nakumbuka mara ya mwisho natoka ndani ya maji baada
ya ubatizo nikafunikwa na blanket zito
tukapiga picha na ndugu na familia wakifurah kweli
Ndo ilikuwa mara yangu ya mwisho kukanyaga kanisani mpaka leo na siji kurudia tena ujinga ule!
Nimeokoka nipo huru.