Je, unajua? Ubatizo wa maji mengi ni ishara ya mtu kufa na kufufuka na Yesu Kristo

Je, unajua? Ubatizo wa maji mengi ni ishara ya mtu kufa na kufufuka na Yesu Kristo

Ubatizo wa maji mengi ni ishara yenye maana sana kiroho. Mtu anapozamishwa ndani ya maji mengi, wakati wa kubatizwa, anaonyesha kuwa utu wake wa kale uliojaa dhambi, umekufa na kuzikwa pamoja na Kristo. Na anapotoka majini, ni ishara ya kufufuka pamoja na Yesu na kuanza maisha mapya ya utakatifu.

Mtume Paulo anasema katika
Warumi 6:4
"Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.”

Ubatizo wa maji mengi ni kitendo cha kuonyesha hadharani kwamba mtu ameacha maisha ya kale, amekubali Yesu Kristo awe Mwokozi wake, na sasa anaishi maisha mapya ya wokovu.
Hakika,
 
Upagani mtupu.
Yaani uovu uondoke kwa kudumbukizwa kwenye maji mengi?
Ama utakatifu uje kwa kudumbukizwa kwenye maji mengi?
 
  • Kicheko
Reactions: K11
Mada hii inawahusu zaidi Wakristo. Hivyo, kama wewe ni Mkristo, point yangu ni hii:
Wakati huu tunaposherehekea kufa, kuzikwa na kufufuka kwa Yesu tusisahau kuwa tukio hilo linahusiana pia na ubatizo wa maji mengi. Hivyo mtu akisema anamwamini Yesu Kristo, akubali pia kuonyesha ishara ya kuzikwa na kufufuka na Yesu kwa njia ya ubatizo wa maji mengi. Kuna watu wengi wanamwamini Yesu lakini ukiwaambia wabatizwe katika maji mengi, wanakuwa wabishi. Mada hii imefafanua kwa kina umuhimu wa kubatizwa katika maji mengi.
Umenipata, mkuu?
Unaposema maji mengi unamaanisha ni maji kiasi gani?
Kikombe?
Ndoo?
Kisima?
Bwawa?
Mto?
Ziwa?
Bahari?
 
  • Kicheko
Reactions: K11
Ubatizo wa maji mengi ni ishara yenye maana sana kiroho. Mtu anapozamishwa ndani ya maji mengi, wakati wa kubatizwa, anaonyesha kuwa utu wake wa kale uliojaa dhambi, umekufa na kuzikwa pamoja na Kristo. Na anapotoka majini, ni ishara ya kufufuka pamoja na Yesu na kuanza maisha mapya ya utakatifu.

Mtume Paulo anasema katika
Warumi 6:4
"Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.”

Ubatizo wa maji mengi ni kitendo cha kuonyesha hadharani kwamba mtu ameacha maisha ya kale, amekubali Yesu Kristo awe Mwokozi wake, na sasa anaishi maisha mapya ya wokovu.

Mathayo 28:19 ​

Nendeni basi, mkawafanye watu wa mataifa yote wawe wanafunzi wangu, mkiwabatiza kwa jina la Baba, na la Mwana, na la Roho Mtakatifu.

Wapi imeandikwa watu wabatizwe kwa maji mengi
 
Ubatizo maana yake kuzamishwa. Wewe unaweza kuzamishwa kwenye maji machache(ya kwenye bakuli)?
Maji ni ishara tu inayokamilishwa na maneno yatumiwayo kubatiza.

Maji na hayo maneno yanayotaja Utatu Mtakatifu si pekee vinaleta umaana wa ubatizo.

Umaana wa ubatizo ni kuishi katika utu mpya uliofufuliwa na Kristo Kwa njia ya ubatizo.

Elewa Theologia ya ubatizo. Kiasi Cha maji hakipimi uhalali wa ubatizo. Wala maji pekee ayahalalishi Ubatizo. ni pamoja na maneno yatumikayo kubatizia.
 
  • Thanks
Reactions: K11
Ubatizo wa maji mengi ni ishara yenye maana sana kiroho. Mtu anapozamishwa ndani ya maji mengi, wakati wa kubatizwa, anaonyesha kuwa utu wake wa kale uliojaa dhambi, umekufa na kuzikwa pamoja na Kristo. Na anapotoka majini, ni ishara ya kufufuka pamoja na Yesu na kuanza maisha mapya ya utakatifu.

Mtume Paulo anasema katika
Warumi 6:4
"Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.”

Ubatizo wa maji mengi ni kitendo cha kuonyesha hadharani kwamba mtu ameacha maisha ya kale, amekubali Yesu Kristo awe Mwokozi wake, na sasa anaishi maisha mapya ya wokovu.
Ufinyu wa akili ndiyo umesababisha kuongezeka Kwa dini na madhehebu.
 
Sijabisha ndugu nimesema wanaobatizwa kwa maji mengi au madogo ni vema.
Kumbuka kila wakati neno "ubatizo" maana yake ni kuzamishwa. Mtu hawezi kuzamishwa kwenye maji madogo(ya kwenye bakuli au kikombe). Ndio sababu Yesu alibatizwa katika mto Yordani wenye maji mengi.
Kilichozaliwa kwa maji ni maji na kilichozaliwa kwa Roho ni Roho.Unaweza kubatizwa kwenye ziwa lakini bado hujazaliwa Mara ya pili.
Acha kupindua Maandiko. Hakuna mstari unaosema kilichozaliwa kwa maji ni maji. Mstari unaojaribu kuunukuu ni Yohana 3:5; huo unasema hivi:
"Yesu akajibu, Amin, amin, nakuambia, Mtu asipozaliwa kwa maji na kwa Roho, hawezi kuuingia ufalme wa Mungu. Kilichozaliwa kwa mwili ni mwili; na kilichozaliwa kwa Roho ni roho."
Hapo Yesu hakutenganisha maji na Roho, bali alisema yote ni muhimu ili mtu azaliwe upya. "Kuzaliwa kwa maji" ni ubatizo wa maji mengi, na "kuzaliwa kwa Roho" ni kazi ya Roho Mtakatifu ndani ya moyo wa mtu.
Mtu anayebatizwa ni lazima kwanza awe ametubu na kumwamini Yesu. Ubatizo unakuwa ishara kwamba ametubu na kumpokea Yesu. Hivyo kauli yako kwamba unaweza ukabatizwa kwenye ziwa lakini ukawa bado hujazaliwa mara ya pili, haiko sahihi.
Makanisa yasiyo ya kisabato hubatiza watu wakiwa bado wananyonya si vema kuwazamisha katika maji mengi kwa usalama wao.Lakini wanapoongezeka umri hupata mafunzo ya kateksim na kubarikiwa baada ya wao wenyewe kumkana shetani.
Kumbuka tena ubatizo ni kuzamisha. Huwezi kumzamisha kwenye maji mengi mtoto anayenyonya. Halafu jiulize ni Andiko gani linaloagiza watoto wanaonyonya wabatizwe?
Maji mengi sio kigezo cha kuingia katika ufalme wa Mungu
Twende polepole. Kama una nia ya kuelewa, utaelewa.

Marko 16:16 inasema
“Aaminiye na kubatizwa ataokoka…”
Kwa andiko hilo ina maana ili tuingie katika ufalme wa Mungu tunapaswa kuamini na kubatizwa. Vigezo hapo ni kuamini na kubatizwa.
Sasa, kumbuka tena, neno la Kiyunani lililoleta tafsiri ya Kiswahili ya ubatizo ni "baptizo," hili linamaanisha kuzamishwa, kuzikwa ndani ya maji, au kufunikwa kabisa na maji.

Baptizo ndilo neno lililotumika katika maandiko ya awali ya Agano Jipya.
Kwa mantiki hiyo, tafsiri nzuri ya Marko 16:16 ni:
“Aaminiye na kuzamishwa katika maji mengi ataokoka…”

Yesu mwenyewe alizamishwa katika mto Yordani wakati anabatizwa
“Yesu alipokwisha kubatizwa, mara alipanda kutoka majini…”
(Mathayo 3:16)

Nini maana ya kupanda kutoka majini? Hii inaonyesha wazi alizamishwa na Yohana ndani ya maji mengi, kisha akapanda juu. Hakunyunyiziwa maji.

Ishara ya kuzikwa na kufufuka haiwezekani kwa kunyunyiziwa maji
“Tumezikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo...”
(Warumi 6:4)

Kwahiyo ndugu yangu tungatagaga , kuzamishwa ndani ya maji ndiyo picha kamili ya kufa na kufufuka pamoja na Kristo. Yesu alipokufa, alifunikwa kaburini. Jiwe kubwa liliwekwa kuziba kaburi. Siku ya tatu akatoka kaburini.

Ili tuingie mbinguni, ni muhimu tuyashike yote aliyoyaagiza Yesu. Ndio sababu Yesu alipowaagiza wanafunzi wake waende kuhubiri Injili ulimwenguni mwote aliwaambia wawafundishe pia watakaoamini kuyashika yote aliyoyaamuru
Mt 28:20
na kuwafundisha kuyashika yote niliyowaamuru ninyi.
Tusipoyashika/tusipoyatenda/tusipoyafanyia kazi aliyoyaamuru, itakuwa vigumu kwetu kuingia katika ufalme wake. Ubatizo wa maji mengi ni mojawapo ya maagizo ya Yesu tunayopaswa kushika.
Yesu anasema katika:
Marko 10:39-40
"...Kikombe ninyweacho mimi mtakinywea, na ubatizo nibatizwao mimi mtabatizwa."
Yesu alibatizwa ubatizo gani? Wa maji mengi.

Leta hoja nyingine zinazokufunga usibatizwe katika maji mengi tuzijadili.
 
Upagani mtupu.
Yaani uovu uondoke kwa kudumbukizwa kwenye maji mengi?
Ama utakatifu uje kwa kudumbukizwa kwenye maji mengi?
1 Wakorintho 1:18-31
Kwa sababu neno la msalaba kwao wanaopotea ni upuzi, bali kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. Kwa kuwa imeandikwa, Nitaiharibu hekima yao wenye hekima, Na akili zao wenye akili nitazikataa. Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi mwandishi? Yuko wapi mleta hoja wa nyakati hizi? Je! Mungu hakuifanya hekima ya dunia kuwa ni upumbavu? Kwa maana katika hekima ya Mungu, dunia isipopata kumjua Mungu kwa hekima yake, Mungu alipenda kuwaokoa waaminio kwa upuzi wa lile neno linalohubiriwa.
 
Ufinyu wa akili ndiyo umesababisha kuongezeka Kwa dini na madhehebu.
Akili unayojivunia itumie basi kuwawezesha ndugu zako kuwa mamilionea. Wenye akili wanaotawala uchumi wa dunia wanamheshimu Mungu, na wiki hii wanasherehekea Pasaka, wewe ni nani hata tukusikilze?
 
Mental slavery
Thank you my friend Mayu for your perspective. However, to categorize conscientious adherence to the explicit teachings and practices of Jesus Christ as “mental slavery” is, with all due respect, a gross oversimplification and an unfortunate mischaracterization of spiritual devotion.

The practice of baptism by full immersion is not a product of indoctrinated servitude, but rather an intentional act of volitional surrender, informed by scriptural exegesis and a desire to emulate the archetype set by Christ Himself.

“He that believeth and is baptized shall be saved…” (Mark 16:16)

To suggest that obedience to divine ordinances equates to psychological bondage is to conflate reverent submission with intellectual capitulation — a false equivalence at best.

In truth, the antithesis of mental slavery is the pursuit of theo-logical clarity, wherein one subjects personal assumptions to the authority of transcendent truth. This is neither blind adherence nor ecclesiastical subjugation, but rather epistemological liberation through divine revelation.

As Scripture affirms:
“And ye shall know the truth, and the truth shall make you free.” (John 8:32)

Thus, those who choose to be baptized as Christ was — not through superficial ritual, but through immersion reflective of death and resurrection — are not shackled minds, but liberated souls responding to eternal verity.
 
Nimeokoka nipo huru.
Huwezi kusema umeokoka halafu kanisani hukanyagi. Labda useme "umetoroka"
Pole lakini. Umeamua mwenyewe kufuata njia pana iendayo upotevuni.
Mathayo 7:13
Ingieni kwa kupitia mlango ulio mwembamba; maana mlango ni mpana, na njia ni pana iendayo upotevuni, nao ni wengi waingiao kwa mlango huo.
 
Unaposema maji mengi unamaanisha ni maji kiasi gani?
Kikombe?
Ndoo?
Kisima?
Bwawa?
Mto?
Ziwa?
Bahari?
Maji yanayotosha kumfanya mtu anayebatizwa afunikwe kabisa mwili wote.
 
Maji ni ishara tu inayokamilishwa na maneno yatumiwayo kubatiza.
Maji sio ishara. Maji ni maji
Maji na hayo maneno yanayotaja Utatu Mtakatifu si pekee vinaleta umaana wa ubatizo.
Hiki Kiswahili cha wapi. Inaonekana umekopi tu na ku-paste
Umaana wa ubatizo ni kuishi katika utu mpya uliofufuliwa na Kristo Kwa njia ya ubatizo.
Umaana?? Sentensi yenyewe inajichanganya tu
Elewa Theologia ya ubatizo. Kiasi Cha maji hakipimi uhalali wa ubatizo. Wala maji pekee ayahalalishi Ubatizo. ni pamoja na maneno yatumikayo kubatizia.
Theolojia ya ubatizo haipaswi kuacha kielelezo cha jinsi Yesu Kristo alivyobatizwa, wala kupunguza uzito wa maana ya neno lenyewe “ubatizo.”

Ubatizo (Baptizo) – kwa Kigiriki – halimaanishi kunyunyizia wala kupaka, bali kuzamisha katika maji mengi.

Yesu hakubatizwa kwa kunyunyiziwa.
"Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara aliibuka kutoka majini” (Mathayo 3:16). Hiyo ni ishara kwamba alikuwa ndani ya maji, akazama, akaibuka. Na Warumi 6:4 inasema:
“Tumezikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo...” Mtu hawezi kuzikwa kwenye bakuli la maji.

Ziko ibada nyingi zinazotumia maneno sahihi lakini bila ishara au tendo sahihi. Ibada za namna hiyo zinabaki kuwa za kimapokeo tu.

Maneno ni muhimu, lakini bila tendo halisi la kuonyesha kufa, kuzikwa na kufufuka na Kristo, maana kamili ya ubatizo inapotea. Hii ndiyo sababu maji mengi ni muhimu. Umeelewa ndugu yangu Servus ?
 
Maji yanaondoa dhambi na kukufanya uache dhambi, uovo na kuwa mtakatifu?
Hapana, maji kama maji hayaondoi dhambi — bali toba ya kweli na imani katika damu ya Yesu Kristo.

Ubatizo wa maji mengi ni ishara ya nje ya kile kilichotokea ndani ya moyo wa aliyeamini, yaani:
Ni tendo analolifanya mtu aliyeokoka, kukiri hadharani imani yake kwa Kristo, na kushiriki kwa vitendo kifo, kuzikwa, na ufufuo wa Yesu Kristo.

Ubatizo ni hatua ya pili ya imani. Yesu alisema:
"Aaminiye na kubatizwa ataokoka..." (Marko 16:16)
 
kinachomfanya mtu kuurithi ufalme wa Mungu ni kipi kati ya ubatizo na matendo mema?.
 
Ubatizo wa maji mengi ni ishara yenye maana sana kiroho. Mtu anapozamishwa ndani ya maji mengi, wakati wa kubatizwa, anaonyesha kuwa utu wake wa kale uliojaa dhambi, umekufa na kuzikwa pamoja na Kristo. Na anapotoka majini, ni ishara ya kufufuka pamoja na Yesu na kuanza maisha mapya ya utakatifu.

Mtume Paulo anasema katika
Warumi 6:4
"Basi tulizikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo katika mauti yake, kusudi kama Kristo alivyofufuka katika wafu kwa njia ya utukufu wa Baba, vivyo hivyo na sisi tuenende katika upya wa uzima.”

Ubatizo wa maji mengi ni kitendo cha kuonyesha hadharani kwamba mtu ameacha maisha ya kale, amekubali Yesu Kristo awe Mwokozi wake, na sasa anaishi maisha mapya ya wokovu.
Uongo mkubwa. Kwani huyo yesu yuko wapi?
 
Theolojia ya ubatizo haipaswi kuacha kielelezo cha jinsi Yesu Kristo alivyobatizwa, wala kupunguza uzito wa maana ya neno lenyewe “ubatizo.”

Ubatizo (Baptizo) – kwa Kigiriki – halimaanishi kunyunyizia wala kupaka, bali kuzamisha katika maji mengi.

Yesu hakubatizwa kwa kunyunyiziwa.
"Naye Yesu alipokwisha kubatizwa mara aliibuka kutoka majini” (Mathayo 3:16). Hiyo ni ishara kwamba alikuwa ndani ya maji, akazama, akaibuka. Na Warumi 6:4 inasema:
“Tumezikwa pamoja naye kwa njia ya ubatizo...” Mtu hawezi kuzikwa kwenye bakuli la maji.

Ziko ibada nyingi zinazotumia maneno sahihi lakini bila ishara au tendo sahihi. Ibada za namna hiyo zinabaki kuwa za kimapokeo tu.

Maneno ni muhimu, lakini bila tendo halisi la kuonyesha kufa, kuzikwa na kufufuka na Kristo, maana kamili ya ubatizo inapotea. Hii ndiyo sababu maji mengi ni muhimu. Umeelewa ndugu yangu @Servus ?
Yesu hakuwa na haja ya kubatizwa kabisa na akuhitaji ubatizo. Kubatizwa kwake inamaana tofauti kabisa na sisi kubatizwa. Kama unataka kubatizwa kama Yesu usichague baadhi ya vielezo na vingine unaacha. Nenda mto Yordani kabisa, tena maji yanayotembea si kujaza maji visimani na njiwa ashuke. Tena ubatizo wa toba (no Trinity formula)

Kielezo cha kuzama kwenye maji si kuzamisha mwili, theolojia yake ni kuzaliwa upya katika roho(yaaniza kuzamisha utu wa kale na kupata utu mpya) kama alivyomwambia Nicodemus.

Maji (halisi) tu yanatosha yawe mengi, machache au wastani,(maana maeneo mengine Kuna uhaba wa maji na watu wanahitaji ubatizo) na Maneno (J, ninakubatiza Kwa jina la Baba na la Mwana na La Roho Mtakatifu)

Usibeze Mapokeo, hayo ni sehemu ya rejea kwani Biblia nayo ni sehemu ya mapokeo. Kwani Injili ya kwanza ni ya Marko imeandikwa miaaka 70 baada ya Kristo.
 
Back
Top Bottom