Je, unajua? Ubatizo wa maji mengi ni ishara ya mtu kufa na kufufuka na Yesu Kristo

Je, unajua? Ubatizo wa maji mengi ni ishara ya mtu kufa na kufufuka na Yesu Kristo

Akili unayojivunia itumie basi kuwawezesha ndugu zako kuwa mamilionea. Wenye akili wanaotawala uchumi wa dunia wanamheshimu Mungu, na wiki hii wanasherehekea Pasaka, wewe ni nani hata tukusikilze?
Mbona unapaniki bidada? Umenielewa lakini? au umekaza kichwa😃
 
Mambo ya udini ni changamoto sana. Mitazamo inatofautiana ati
Mitazamo inatofautiana kwa sababu watu hawafuati Biblia kikamilifu. Wanafuata mafundisho ya watu badala ya kufuata Biblia. Ubatizo wa maji mengi umeelezwa wazi katika Biblia lakini watu siku hizi ni wabishi kama ambavyo Smart911 anapenda kusema.
"Mungu asema: Watu hawa huniheshimu kwa maneno tu, lakini mioyoni mwao wako mbali nami. Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu.." — Mathayo 15:8-9
Ukweli haupatikani katika dini au dhehebu, bali katika Yesu na Neno lake.
"Mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru." — Yohana 8:32
 
Mbona unapaniki bidada? Umenielewa lakini? au umekaza kichwa😃
Cha kunipanikisha ni nini. Shetani mwenyewe akinijia namfukuza kama mbwa koko
 
Jumatatu ya Pasaka, kuna makanisa huwa yanafanya ubatizo wa maji mengi kwa waumini wapya.
Naamini na mwaka huu itakuwa hivyo!
 
Back
Top Bottom