Je, unajua? Ubatizo wa maji mengi ni ishara ya mtu kufa na kufufuka na Yesu Kristo

Mbona unapaniki bidada? Umenielewa lakini? au umekaza kichwa😃
 
Mambo ya udini ni changamoto sana. Mitazamo inatofautiana ati
Mitazamo inatofautiana kwa sababu watu hawafuati Biblia kikamilifu. Wanafuata mafundisho ya watu badala ya kufuata Biblia. Ubatizo wa maji mengi umeelezwa wazi katika Biblia lakini watu siku hizi ni wabishi kama ambavyo Smart911 anapenda kusema.
"Mungu asema: Watu hawa huniheshimu kwa maneno tu, lakini mioyoni mwao wako mbali nami. Kuniabudu kwao hakufai, maana mambo wanayofundisha ni maagizo ya kibinadamu tu.." — Mathayo 15:8-9
Ukweli haupatikani katika dini au dhehebu, bali katika Yesu na Neno lake.
"Mtaifahamu kweli, nayo hiyo kweli itawaweka huru." — Yohana 8:32
 
Mbona unapaniki bidada? Umenielewa lakini? au umekaza kichwa😃
Cha kunipanikisha ni nini. Shetani mwenyewe akinijia namfukuza kama mbwa koko
 
Jumatatu ya Pasaka, kuna makanisa huwa yanafanya ubatizo wa maji mengi kwa waumini wapya.
Naamini na mwaka huu itakuwa hivyo!
 
Mimi za kuambiwa hua nachanganya na za kwangu...
Enhe, habari hizi nilizokuambia (za ubatizo wa maji mengi), baada ya kuzichanganya na habari za kwako, umepata hitimisho gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…