Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?


mmeshindikana uraiani ndio mmekuja hapa kushindanana ! ................. hapa hafukuzwi mtu !
 
Wakuu, kizazi kipya ambacho hakikupita JKT wanatulaumu kwamba tuliopita JKT wengi wetu ndiyo tumeshiriki kuifisadi nchi! Je hayo maneno yana ukweli wowote?
 
nakumbuka nikiwa Mafinga wakati BT akiwa Major Chacha(mrefu sana) na Co akiwa T Mlay. Kwa sabasu ya ile nyahenge(baridi) waliamua lijengwe bench na kwa bahati mbaya lile bench walipima urefu wa Chacha ambaye alikuwa mrefu mara 2 ya Mlay na hivyo akikaa miguu inaning'inia. Basi wale Macoplo walipigwa Kadebra ya kufa Mtu na maneno makali juu kwamba nani Co mimi au Chacha. Wako wapi ma RP Songolo, Maneno Mahenge
 

nilikuwa kambi ya mafinga JKT, kombania c (chale koy) chini ya afande Kweka AKISAIDIWA na RSM by that time Danda.sitasahau siku msitu wa mafinga ulipowaka moto na kuamuliwa kwenda kuzima mida ya saa tatu asubuhi ambapo zoezi hilo lilienda mpaka kesho yake saa 11 jioni na afande co aliagiza tuletewe shea zetu zote kuanzia uji chakula cha mchana cha jana yake, jioni, uji wa asubuhi siku ya pili kwa madai shea ya mtu jeshini hailiwi. sitasahau pia siku CO Mray ametoka dodoma na azimio la kilimo kwanza ulikuwa mwezi january/february ambapo tulilazimika kupelekwa idetero karibu na msitu wa mafinga na kwa wakati huo mvua ilikuwa nyingi sana ikiwa ni pamioja na radi kwa muda wa week mbili, lakini baada ya maombi ya wapiganaji (kuruta) mvua ilisimama/radi zilikoma, kimsingi tulijengewa sana "UVUMILIVU", "UZALENDO", NA UKAKAMAVU.

 
mmeshindikana uraiani ndio mmekuja hapa kushindanana ! ................. Hapa hafukuzwi mtu !

umenikumbusha mbali sana malizia na wimbo " mimi ni pweza..... Mwenda na maji..... Wimbi likija naliepuka!!!!! Mwanzishaji ni afande then kuruta aliitikia "wewe ni pweza... Mwenda na maji .... Wimbi likija waliepuka !!! Hapakutosha
 
waoh JKT MAKUTUPORA, AFANDE ZIMWI,AFANDE LUKANGA 'kamama unachambia wembe ?' sir major Kahiriko akigawa kondomu 'mwenyewe akisema ni viwembe mwende mkanyoane,CCM inawapenda imewaweka wanawake na wanaume hivyo imeleta viwembe kwa ajili ya kunyoana' mgao ulikuwa kwa wanaume tu.
Afande George Nyeriga Nyamhanga wa acha !!! HAKIKA KUTOKWENDA JKT VIJANA WANAMISS VITU ADIMU NA ADHIMU
 

1.KUNYAKUA USAWA WA GUDULIA
2.KUJIFANYA SELULE
3.KAMA NYIE NI FORM SIX BASI SISI NI MAFORM SEVEN
4.KUPOZA UJI KWA MAJI YENYE MKOJO WA NG'OMBE
5.WAKATI WA SERVICE MI NILIKUWA MPISHI.
Buhemba operation miezi 6.
 
JKT ni heri irudishwe tuu bse vijana wa leo ndo maana wanaaribika ukakamavu sifuri mara ooh mtoto si rzki.
Wale wa Mafinga mpo?
Tupo ! TN Mlay, C.O, Basi bwana kuna mshikaji kwenye grup yetu alikua anapiga mkuu wa kombani C Coy, (Captain) sasa siri ikavuja na akatafutwa mtoa huduma ! Grup likatafutiwa visa (tulikuwa 4) mie by the time nilikua 'AWOL' (nimetoroka!) washikaji wakanitaja mimi ! We acha tuu ! Nilirudi kumepoa lakini nilitolewa katika tangazo (nimesahau jina la yale matangazo ya kijeshi) siku naripoti nikakuta bogi la mlalakuwa nikaunga ! Wanashtuka niko Dar !
 
unakuwa sharp, makini, muangalifu, unaishi kwa tahadhari, unapiga hesabu kila nyendo yako ! Ukika bila kufanya kazi wewe bingwa. Unaweza kudhibitiwa 24hrs!
 
siku ya kumaliza mazoezi ya kijeshi 'pass out' TN MLAY alileta mtihani wa mahojiano, sie havkulijua hilo, mie akaniuliuza nimuoshe sox ya kulia ni ipi kati ya sox mbili, alooooh ! Sikujuaa kama sox ina kulia na kushoto!
 

Du! Hii nayo bibi kubwa!
 

ha ha kwakweli jeshi zuri sana,uwezo wa kufikiria lazima uongezeke.
 

Jayfour kumbe ni wewe? Wewe si ulikuwa ujenzi na akina Edward Nzigula na yule Engineer mwingine mjita mlikuwa mmetoka naye Mbeya Technical, alikuawa anaitwa Ngosi kama sikosei! Kole Sadiki yuko wapi?
Aisee mbona hujanitaja aisee babaangu? Au kwa vile niliwaacha kombania nikahamia chokaa kwa afande Mayila? Kazi inaisha saa 4 halafu tunaanza kuogelea ziwani, afande Jogoo na Makere wakija hatuelewi kitu.
Kule tulikuwa na akina Reuben Nkori, Busagala Masale, Haule, Mbuna, Chambo.
Wakati niko kombania mimi ndiye nilikuwa natangulia pale mbele ya mstari tukiwa na Karume Mbulwa ambaye baadaye alikuja kuwa ni RP, halafu wanafuatia wengine kama akina MC Nyamhanga, Commandoor Katani. Nawakumbuka sana wasichana wa Danger Coy akina Winifrida Bita, Eda (mnapata kichere mnakwenda kaseke), Esther Koroti, Yasinta John (kasheshe yake na afande Pima kwenye chenja unaikumbuka?, alirudia kutaja jina kama mara mia pale mbele ya hanga la wavulana D-coy).
Siku moja nikaokota filimbi. Niko na jamaa alikuwa anaitwa Mbogo Mnubi usiku katikati ya mahanga ya D na C, kule nyuma, nikawa napuliza filimbi "fiii" halafu Mbogo akawa anasema "ruka, ruka", halafu mimi naruka kichura na buti zangu pwaaa pwaaa, mahanga yote yakatimua mbio usiku chaga za vitanda zinadondoka chini watu wakadhani ni ma MP wako around. Baadaye na sisi tukakimbia kuogopa kibano sababu watu waligundua kuwa tumewachezea akili.
Mabigula ya usiku kwenda kuzima moto, tumeingia uchaka sana unaondoka na Blanketi mbili, kurudi majaliwa.
Mimi ndiye niliyekuwa naigiza sauti ya yule afande giant msukuma coplo alikuwa anaitwa Bujiku wa uvuvi. Akikukamata push-up una kosa anakwambia, "nipe zangu mbili, OC, Sir Major wa kombania naye tatu, OC naye nne,.... yaani we acha tu".
Halafu siku moja tunapiga kwata uwanja wa damu, mzee wa kadebula a.k.a commandoor Makoba akaingia ghafla halafu lisichana limoja la D-coy likaropoka "Cock up", mama yangu, kumbe amesikia! Akaanza, " nani amesema cock-up hapa, eeh nai,....jenga reli,... yaani ilikuwa ni issue, choka mbaya! Jeshini we acha tu, hadi nilitaka kuwa kujiunga nikasomee u-Rubani wa ndege szile ndogo za jeshi, Mungu hakujalia!

 

Jayfour;
Ilikuwa 92/93.
Hivi kumbe hata Joe Kihampa tuiklikuwa naye? Simkumbuki. Possibly alianzia mgombe hivyo wakati anarudi mimi nikawa nimeshahamia HQ.
 

Halafu ukimtaja Anterius lazima umtaje na Hussein nasibu, Boaz Nkoko, Muzeli Mazengo, Josephat Kataga (ukicheza naye karata akikupiku nasema "Kuleeeeee', wakati anadondosha karata yake". Aisee umenikumbusha mbali sana.
 
Hongereni mliofanikiwa kuonja utamu wa nchi yetu.
Je,mnaweza kuniambia kuwa J.K.T inaweza kupunguza migomo ya vyuo vikuu kama wabunge wetu walivyo sema mwaka juzi(2010)?
 
Nikumbushe Same sekondari kuchota maji Stesheni
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…