Ally Kombo
JF-Expert Member
- Nov 11, 2010
- 11,429
- 2,650
Mafinga JKT Operation Miaka 25 (1988/89) i realy miss you. Danger coy mko wapi wakuu? Kayange, Double P, Chalamila, Nyaulingo where are guys? Namkumbuka Sir Major Mulembo akimfokea Kayange:
Afande Mulembo: We Kuruta unajifanya mjanja sana eeh?
Kayange : Kimya
Afande : mimi ninakuuliza wewe unanyamaza Kimya?Afande akikuuliza "unajibu ndiyo afande"
Kayange: ndiyo afande
Afande : unajifanya mjanja sana?
Kayange : Ndiyo Afande
Afande: pumbafu zako
Kayange: ndiyo afande
Afande: Unatuona sisi ni wajinga sana?
Kayange: Ndiyo afande
Afande: ( akiwa amekasirika) Unatuona sisi wapumbavu sana?
Kayange: Ndiyo afande
kombania tukashindwa kuvumilia tuaanza kucheka tukala push ups wote kwa kucheka huku bado akiwa hajui kuwa amem-limit Kayange kujibu 'Ndiyo afande' hata kwa negative statements.
mmeshindikana uraiani ndio mmekuja hapa kushindanana ! ................. hapa hafukuzwi mtu !