Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Najutia kupoteza mwaka mzima kule 832 KJ Mgambo/Operation Vyama vingi.
Hakuna chochote nilichofaidika zaidi ya kuupoteza mwaka wangu kule bila kitu chochote cha maana zaidi ya kukutana na marafiki wapya. Period!
Nililimishwa kama Valmet. Nilichuma machungwa kama ngedere. Nilifyeka nyasi kutumia jembe!
All in all it was a year lost. Labda kwa wengine mlifaidika ama mtaendelea kufaidika na JKT. Lakini to me personally hakuna cha maana nilichokiona huko. Ni waste of tax payers' money.
Samahani kama wengine mtakwazika

Sahihisho siyo 832 ni 835KV ( Kikosi cha Vita)
Hongera kama ulipata pafahamu Gendagenda,Komsanga na Kwa Bojo.
Hope ulitendewa Haki pale Uwanja wa Damu.
 
Kwanza nikupe hongera kwa kufanya maamuzi sahihi ya kuingia kwenye chombo cha ulinzi wa taifa na watu wake...

JKT tofauti na wengi wanavyodhani ni tawi la TPDF likiwa na malengo mahususi ya kuandaa vijana kuwa na maadili ya kitanzania... kwa kifupi jkt haitoi ajira bali inapika/inawandaa vijana kimafunzo kuingia katika nyanja tofauti za ulizi kama jwtz, polisi, magereza, immigration, Tanapa, bandari, intelligence nk nk....

mafunzo ya jkt yapo in four phases ie; uraia, uzalendo, ukuruti, uservice....
1. Uraia
ni phase/cheo kinachodumu kwa si zaidi ya dkk 5-10, mara tu unapowasili katika kambi ya mafunzo utapokelewa kama kanali, utafanya registration ukimaliza utapikwa para la kijeshi (transformation from a citizen to a patriot) hapa hakuna fujo ya aina yoyote...
2. Uzalendo
Hii phase me naiitaga grace period,inalast to about 3-4 weeks hapa hakuna longolongo, its full of harmon.. unalelewa kama yai, ukikwazika unabembelezwa unafutwa machozi, hapa kuna mafunzo ya kawaida sana ushauri kutoka kwa wakuu, story na makamanda, kujifunza kuimba nyimbo za kibattle, its like a form of orientation.... kulala ni saa 3 kuamka saa 12 tena bila karaha...
3. Ukuruti(recrute)
hii ndio kozi halisi ya jkt, me naiitaga a battlefield... mtoto hatumwi sokoni, kama wewe ni mchele mchele lazma utoroke (kuacha unyoya)
inalast kuanzia 6-8 weeks, hapa ni mkesha mwanzo mwisho (omba mungu muwe na instructors wajanja/wachakachuaji) mnachanga vi100-100 hadi 15000-20000, mnalegezewa mkesha... hapa ndipo wakina aisha na joyce wanagegedwa kiulaini...
kuhusu kutokuvua viatu; usipokua mwepesi hii inaweza kukukumba at this phase... kiukweli huu huwa ni wakati mgumu sana, ikikachumbarishwa na intro.course, watu hizimia hadi 100 kulingana na wingi wa makuruti
Ukimaliz hizo wiki 6, japo bado utakuwa ni kuruti lakini ugumu utapunguzwa....

Umejitahid kueleza lkn umechemka phase ya uzalendo at unafutwa machoz! hakuna kiyu km hicho na kwanza kwangu kat ya vpnd nilivoviona kwang vgumu n hichi kpindi cha uzalendo, unapofika langon tu unaambiwa ukimbiemchaka mchaka na soldiel box yako ambayo kwetu tunaita tranka kichwan sintasahau, labda inategemeana na kambi coz nackia nilokuwako watu wanaisema ya kibettle 842kj mnaamshwa saa 10 kpind cha uzalendo mnapiga jambo afande mpaka saa moja asubh hapo n kunyanyua mguu acha kabisa. kikubwa hata wao wanakwambia jitoe ufaham na akili zako uziache getn kila utachoambiwa n ndio afande hali si nzur hasa kwa hawa dadazetu
 
Sahihisho siyo 832 ni 835KV ( Kikosi cha Vita)
Hongera kama ulipata pafahamu Gendagenda,Komsanga na Kwa Bojo.
Hope ulitendewa Haki pale Uwanja wa Damu.

kambi ya mgambo ni 835kj...labda kama imebadilishiwa enzi zenu ilikuwa inaitwa kwa jina tofaut....umesahau na bwawani,machungwani na mjini kabuku
 
Ebana sie tulishafanyiwa uchunguz nov, 1. Kama mguu una uvungu 2. Unanyanyua mikono juu daktari anaangalia kifua chako ukiwa kifua wazi 3. Unaonesha mikono mbele na nyuma...tunasubiri kuitwa tena, je uchunguz mwingine wa kiifya huwa unafanywa au magonjwa gani wanapima? Au km tulifanyiwa huo uchunguz hakuna tena issue za vipimo? Kwa aliyejeshin anijuze plz
 
Ebana sie tulishafanyiwa uchunguz nov, 1. Kama mguu una uvungu 2. Unanyanyua mikono juu daktari anaangalia kifua chako ukiwa kifua wazi 3. Unaonesha mikono mbele na nyuma...tunasubiri kuitwa tena, je uchunguz mwingine wa kiifya huwa unafanywa au magonjwa gani wanapima? Au km tulifanyiwa huo uchunguz hakuna tena issue za vipimo? Kwa aliyejeshin anijuze plz

Kunyanyua mikono juu wanapima nn kwenye kifua?
 
Swala la JKT limekua compulsory kwa wale wote tunaosubiri nafasi za professionals za jeshi kwani ni lazima kwanza tu serve jkt for four months then ndio miezi sita ya officer cadet. Mimi naomba kwa wale ambao mmepitia huko (hususan walioapa juzi juzi) mtu habarishe nini cha ku expect huko, na since day 1 mlivowasili kambini ilikuaje etc. Hii itasaidia wengi kujiandaa psychologically and physically kwaajili ya mafunzo. Kwani huku mtaani speculations ni nyingi sana, wengine wanasema wiki sita za kwanza hamna kuvua mabuti wala kulala na rumours nyingine kama hizo hivyo kwa ambaye hatojali basi tungefurahi kama ata share na sisi hapa.
Regards,
Don Lucchese cc xir jyerphy

Mkuu pia unaweza kupitia uzi huu: https://www.jamiiforums.com/habari-...1863-je-unakumbuka-nini-enzi-zako-za-jkt.html
 
kweli tz kwa usalama tupo nyuma hivi mnahakika na uraia wa aliyeleta uzi huu? na hizi taarifa mnajua anataka kuzifanyia kazi gani hamna uanajeshi hapo ni uraia tu mjeshi aliyeiva kijeshi angefunga mdomo shame on you

Hizi sio zama za mawe!!! Wanakohifadhi bunduki na mizinga ni halali kufanya siri. Sasa kuwafahamisha watu kuhusu mchakamchaka nako kuwe siri?
 
Swala la JKT limekua compulsory kwa wale wote tunaosubiri nafasi za professionals za jeshi kwani ni lazima kwanza tu serve jkt for four months then ndio miezi sita ya officer cadet. Mimi naomba kwa wale ambao mmepitia huko (hususan walioapa juzi juzi) mtu habarishe nini cha ku expect huko, na since day 1 mlivowasili kambini ilikuaje etc. Hii itasaidia wengi kujiandaa psychologically and physically kwaajili ya mafunzo. Kwani huku mtaani speculations ni nyingi sana, wengine wanasema wiki sita za kwanza hamna kuvua mabuti wala kulala na rumours nyingine kama hizo hivyo kwa ambaye hatojali basi tungefurahi kama ata share na sisi hapa.
Regards,
Don Lucchese cc xir jyerphy

Mkakati wa watarajiwa wa JWTZ kUPITISHWA JKT ni ugoro wa watawala kutafuta kuingiza watu wao ndani ya JWTZ. JKT ni jeshi la kujenga taifa, liliwekwa kwa ajili ya wasio na ajira wakajiunge na kujifunza kujiajiri PAMOJA na kuwa wanajesi wa akiba wanaoweza kuitwa wakati wa dharura kutoa huduma za mwelekeo wa kijeshi. Waliokuwa wakilazimishwa kujiunga ni School leavers (X-FormVI na X-University) kabla hawajaiingia katika ajira. Madhumuni ilikuwa kujenga nidhamu yao, na kweli walikuwa na nidhamu hata kazi zao zilionekana hivyo. Mafisadi walikuwepo wachache sana.

Hawa wajanja wanaopeleka watoto wao JKT miezi 4 halafu wanawafanya ndio wenye sifa ya kujiunga na JWTZ ni waharibifu na matokeo yake mtayaona karibuni. Kuna "Shamsi Vuai Nahodha" mwingine atajiuzulu tu kwa ugoro wa wanajeshi hao.

HALAFU MNASEMA MNASHANGAA MAWAZIRI SASA WANASHINDWA KUONGOZA WIZARA ZAO HUKU MKIPELEKA NYENZO ZENYEWE ZA KUWAFANYA WASHINDWE KUFANYA KAZI. MAMA SITTA ALIPELEKA WALIMU BAMBUCCHA SASA MASAHIBU YANAMKUTA KAWAMBWA. NA KWA NINI KAWAMBWA NA SI MAJALIWA HAPO PIA UNABAKI KINYWA WAZI. HERI YAKE JAKAYA MAANA YEYE WAKIJIUZULU ANATEUA WENGINE, YEYE AAAAAAAAH!!!!!! WALIOSHINDWA NI WAO SIYO YEYE, YEYE YUKA AMERIKA.
 
Kama kungekuwa na uwezekano wa kukubondea like zaidi ya moja, ningekupa thumb up mara buku...

Kama us wanatoa mpaka video za recruit wa jeshi (sio national service), tena kupitia u tube, kunaubaya gani sasa wa kusema kuwa kule jkt wananyoa mapara, wanalima, wanafanya phys training, wanaenda mchakamchaka na route match, wanaimba, jinsi ya kuingia nk nk.......

Ndo maana nakupenda jamii forum, where we dare to speak openly....

Hahahaha, endelea na kuelimisha vijana mzazi. Huyo hajui kuwa youtube kuna mpaka video za navy seals!!
Majuzi nimeona edition moja ya achievements za navy seal team 6, ikiwa ni pamoja na maoni ya former members of the same team
 
Kambi. MANGE JKT KJ 245
CO. afande Sanga lt col
2ic .major Rajabu from znz
adjutant. capt Ngowo
lts Kajoro. mchina. Dr. lema
sgt. Wela
cpl. Mandevu mpu.u.zi sana huyu
vol. lcpl . Frida
operation. Nidhamu baada tu ya OKOA
 
Ambacho sitasahau ni siku moja afande alijisaidia kwenye mlango wa hanga akatusingizia. Tukapewa adhabu ya kuchukua kila mtu kidogo kidogo. Akajitolea mmjo kuzoa lakini wakakataa. Kila mtu alishika mpaka ikaisha.
 
Ambacho sitasahau ni siku moja afande alijisaidia kwenye mlango wa hanga akatusingizia. Tukapewa adhabu ya kuchukua kila mtu kidogo kidogo. Akajitolea mmjo kuzoa lakini wakakataa. Kila mtu alishika mpaka ikaisha.

Duuh hii kali . . .
 
Ambacho sitasahau ni siku moja afande alijisaidia kwenye mlango wa hanga akatusingizia. Tukapewa adhabu ya kuchukua kila mtu kidogo kidogo. Akajitolea mmjo kuzoa lakini wakakataa. Kila mtu alishika mpaka ikaisha.

Mlijuaje kama afande ndo kashusha mzigo ule mkuu? Yaan kama kumega ugali vile hahahahah!
 
Ndugu zangu

Naenda kambi ya Mgambo Kabuku Tanga kwa mafunzo ya jeshi la Kujenga Taifa. Ninaomba waliopita kambi hii wanijulishe mambo ya ndani ya kambi hii, historia yake na mazingira yake. Nataka nione maisha ya jeshini haswa na kama itawezekana nifanye kazi ya kujitolea kufundisha shule ya kata ya jirani kama ipo.

ufundishe shule ya kata wewe mwalimu!?
 
Hapo nitapenda kuwakumbusha wale tuliokuwa wote pale Mafinga JKT Kombania F chini ya OC Rweikaza na yule afande invisible aliye julikana kwa jina la Master Follow-up. Tutamkumbuka afande kijana aliyeitwa Mwakyosi. Nakumbuka siku moja tuliamshwa saa kumi alfajiri kama ilivyokuwa kawaida kukata mifagio wakati tukielekea huko porini kukata mifagio kwa mchaka mchaka tuliambiwa twende tukiimba, nikaanzisha wimbo "...Siasa yetu hapana mbaya. Isipokuwa maafande ndiyo wabaya..." Jamaa kusikia mistari ile akaamuru wote kuchuchumaa chini na kuruka kichura chura.

Upande wa Afande Master Follow-up au Afande Mlimbila ambaye sasa ni marehemu, nakumbuka siku moja alimuuliza kuruta mmoja kwamba alipataje kovu lililo katika paja karibu na nyonga. Tamko lile lilizua kilio kwa binti yule na binti alikwenda moja kwa moja kwa CO T N Mlay kutoa taarifa kuhusu mauza uza aliyoyaona usiku ambapo alisema alikuwa akiota kuna mtu amevinjari naye usiku kucha na iweje afande atamke kuhusu kovu wakati ni kweli analo na alijuaje wakati hajawahi kuwa naye kwa makubaliano.

Kifo cha Master Follow-up: Siku hiyo kulikuwa na mkutano mkuu wa wakuu wa vikosi Ma-CO nchini wakati huo Mlimbila alipangiwa kulinda kituo kidogo cha JKT kilichoitwa Sao Hill ambako kulikuwa na mradi wa kuchoma mkaa. Jamaa akakaimu kazi hii kwa mtu mwingine yeye akabaki kikosini. Pale kikosini kulikuwa na afande mmoja Mngoni aliyekuwa na mkewe dogo dogo aliyeishi karibu kabisa na apartment au hanga la Mlimbila. Na afande huyu Mngoni alipangiwa kulinda geti dogo karibu kabisa na nyumbani kwake na inaelekea alishapata fununu za mtoto (Mkewe) kuvinjari na Mlimbila. Muda wa saa mbili usiku bwaloni kukiwa na dance la kumalizika kwa mkutano afande Mngoni akaaga kwenda nyumani kwake "kukagu". Inasemekana alifika akagonga mlangoni bila kufunguliwa, kisha akaenda kuchungulia dirishani na kumuona Mlimbila akiwa ameketi kitandani akiwa mtupu na mke wake afande Mngoni. Alilenga SMG kupitia upenyo wa dirisha na kumkuta Mlimbila katikati ya paji la uso kuona vile binti alikimblia sebuleni na kufungua mlango na kukimbia. Mngoni aliingia na kuuchakaza mwili kila sehemu kwa risasi. Alibakiwa na risasi kama tisa tu. Mwili wake ulipelekwa Mafinga Hospital kujazwa pamba ili angalau uso wake uweze kutambulika. Haya ndiyo nayakumbuka sana ninawakumbuka kuruta wenzangu akina Tarama Mamkwe, Ndubula Msaki, Rachel Mapande, na wengineo.

Umenikumbusha mbali sana fisi maji mwenzangu! Unakumbuka kanali Mlay alikuwa akikasirika anatuita fisi maji? Kanali Mlay alikuwa mchungu hata kwa mkewe Cpt Mlay aliyekuwa catering officer wakati wetu! Tena bila shaka wewe ulipita 841 KJ wakati wa operation vyama vingi 1992-1993.

Namkumbuka aliyekuwa cheef cook wa F coy baadaye akaenda kitengo cha watu wenye nguvu cha kupasua magogo na kuni ambacho kiliifanya F coy kuwa mfano wa kuigwa kambini! Jamaa alikuwa poa sana kwenye maswala ya msosi siku nikijongo kwenda Idetelo shamba kwenye milaba ya mahindi.

Maishani mwangu sitasahau siku nilipokamatwa na MP nikikatiza uwanja wa ndege nikiwa nimebeba deli lenye chakula na dumu la lita 5 la ulanzi nilivyokuwa navipeleka kwa wenzangu niliokuwa nimewaacha Dubliganga wakipasua kuni! Nilirushwa kichura umbali wa mita 300 mpaka Kota guard na kupewa extra drill ya dakika 45 na kupelekwa mahabusu kisha kesho yake nikahukumiwa kifungo cha wiki moja!

Kuna siku tukiwa kijijini tukinywa ulanzi nyumbani kwa mama tuliyekuwa tunamwita mama wawili kutokana na kuwa na watoto mapacha, ghafla wakaingia maafande wakikamata kuruta na servicemen waliotoroka kambini kukatokea purukushani ya kujificha. Mimi nikaingia ndani ya gunia lililokuwa jirani na magunia ya mahindi yaliyokuwa yanapukuchuliwa na kujificha humo kimya huku wenzangu wakikamatwa na kupelekwa mahabusu!

Mafunzo ya mwaka mmoja niliyoyapata 841 KJ yamenifanya niwe mkakamavu, mwenye upendo na mtii kwa watu wa rika zote mpaka sasa! Nawakumbuka Amandus Manda, Juma kisyeri, Wangson Waya, Widala Malaba,Boniface Mwangole, Marehemu afande Israeli, Afande Cpt Koka, Afande Cpt Kweka, Afande Lucy, Afande Kawawa, wana Serengeti (makuruta wa kike) na wale wote waliokuwa wanapenda kusimamisha minazi usiku wakati wenzao wanapokuwa wakiimba nyimbo disko!
 
Umenikumbusha mbali sana fisi maji mwenzangu! Unakumbuka kanali mlay alikuwa akikasirika anatuita fisi maji? Kanali Mlay alikuwa mchungu hata kwa mkewe Cpt Mlay aliyekuwa catering officer wakati wetu! Tena bila shaka wewe ulipita 841 KJ wakati wa operation vyama vingi 1992-1993.

Namkumbuka aliyekuwa cheef cook wa F coy baadaye akaenda kitengo cha watu wenye nguvu cha kupasua magogo na kuni ambacho kiliifanya F coy kuwa mfano wa kuigwa kambini! Jamaa alikuwa poa sana kwenye maswala ya msosi siku nikijongo kwenda Idetelo shamba kwenye milaba ya mahindi.

Maishani mwangu sitasahau siku nilipokamatwa na MP nikikatiza uwanja wa ndege nikiwa nimebeba deli lenye chakula na dumu la lita 5 la ulanzi nilivyokuwa navipeleka kwa wenzangu niliokuwa nimewaacha Dubliganga wakipasua kuni! Nilirushwa kichura umbali wa mita 300 mpaka Kota guard na kupewa extra drill ya dakika 45 na kupelekwa mahabusu kisha kesho yake nikahukumiwa kifungo cha wiki moja!

Kuna siku tukiwa kijijini tukinywa ulanzi nyumbani kwa mama tuliyekuwa tunamwita mama wawili kutokana na kuwa na watoto mapacha, ghafla wakaingia maafande wakikamata kuruta na serviceman waliotoroka kambini kukatokea purukushani ya kujificha. Mimi nikaingia ndani ya gunia lililokuwa jirani na magunia ya mahindi yaliyokuwa yanapukuchuliwa na kujificha humo kimya huku wenzangu wakikamatwa na kupelekwa mahabusu!

Mafunzo ya mwaka mmoja niliyoyapata 841 KJ yamenifanya niwe mkakamavu, mwenye upendo na mtii kwa watu wa rika zote mpaka sasa! Nawakumbuka Amandus Manda, Juma kisyeri, Wangson Waya, Widala Malaba,Boniface Mwangole, Marehemu afande Isreli, Afande Cpt Koka, Afande Cpt Kweka, Afande Lucy, Afande Kawawa, wana Serengeti (makuruta wa kike) na wale wote waliokuwa wanapenda kusimamisha minazi usiku wakati wenzao wanapokuwa wakiimba nyimbo disko!




Nilikuwa operation Kujihami mwaka nadhani 1982. Nilikuwa Makutupora, tukaenda kozi ya
uongozi Ruvu tuliokuwa tumemalizia A level shule za mchepuo wa kijeshi. Kozi nadhani ilikuwa miezi sita.

Tulivyofaulu tukaenda kwenye gwaride la sherehe za Muungano hapo kurasini.
Tulipomaliza tukatawanywa tena wengine wakabaki hapo wengine tukaenda kumalizia mwaka Mbweni JKT. It was a nice experience na nivizuri km ukibahatika nenda kajifunze ukakamavu.

Ni mengi hasa tulipokuwa Makutu hadi Ruvu, wali wa Vibwende nk. Those days na simba wa Ruvu Mola mkubwa.
Happy New Year.
 
Back
Top Bottom