Kwanza nikupe hongera kwa kufanya maamuzi sahihi ya kuingia kwenye chombo cha ulinzi wa taifa na watu wake...
JKT tofauti na wengi wanavyodhani ni tawi la TPDF likiwa na malengo mahususi ya kuandaa vijana kuwa na maadili ya kitanzania... kwa kifupi jkt haitoi ajira bali inapika/inawandaa vijana kimafunzo kuingia katika nyanja tofauti za ulizi kama jwtz, polisi, magereza, immigration, Tanapa, bandari, intelligence nk nk....
mafunzo ya jkt yapo in four phases ie; uraia, uzalendo, ukuruti, uservice....
1. Uraia
ni phase/cheo kinachodumu kwa si zaidi ya dkk 5-10, mara tu unapowasili katika kambi ya mafunzo utapokelewa kama kanali, utafanya registration ukimaliza utapikwa para la kijeshi (transformation from a citizen to a patriot) hapa hakuna fujo ya aina yoyote...
2. Uzalendo
Hii phase me naiitaga grace period,inalast to about 3-4 weeks hapa hakuna longolongo, its full of harmon.. unalelewa kama yai, ukikwazika unabembelezwa unafutwa machozi, hapa kuna mafunzo ya kawaida sana ushauri kutoka kwa wakuu, story na makamanda, kujifunza kuimba nyimbo za kibattle, its like a form of orientation.... kulala ni saa 3 kuamka saa 12 tena bila karaha...
3. Ukuruti(recrute)
hii ndio kozi halisi ya jkt, me naiitaga a battlefield... mtoto hatumwi sokoni, kama wewe ni mchele mchele lazma utoroke (kuacha unyoya)
inalast kuanzia 6-8 weeks, hapa ni mkesha mwanzo mwisho (omba mungu muwe na instructors wajanja/wachakachuaji) mnachanga vi100-100 hadi 15000-20000, mnalegezewa mkesha... hapa ndipo wakina aisha na joyce wanagegedwa kiulaini...
kuhusu kutokuvua viatu; usipokua mwepesi hii inaweza kukukumba at this phase... kiukweli huu huwa ni wakati mgumu sana, ikikachumbarishwa na intro.course, watu hizimia hadi 100 kulingana na wingi wa makuruti
Ukimaliz hizo wiki 6, japo bado utakuwa ni kuruti lakini ugumu utapunguzwa....