Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?


Sahihisho siyo 832 ni 835KV ( Kikosi cha Vita)
Hongera kama ulipata pafahamu Gendagenda,Komsanga na Kwa Bojo.
Hope ulitendewa Haki pale Uwanja wa Damu.
 

Umejitahid kueleza lkn umechemka phase ya uzalendo at unafutwa machoz! hakuna kiyu km hicho na kwanza kwangu kat ya vpnd nilivoviona kwang vgumu n hichi kpindi cha uzalendo, unapofika langon tu unaambiwa ukimbiemchaka mchaka na soldiel box yako ambayo kwetu tunaita tranka kichwan sintasahau, labda inategemeana na kambi coz nackia nilokuwako watu wanaisema ya kibettle 842kj mnaamshwa saa 10 kpind cha uzalendo mnapiga jambo afande mpaka saa moja asubh hapo n kunyanyua mguu acha kabisa. kikubwa hata wao wanakwambia jitoe ufaham na akili zako uziache getn kila utachoambiwa n ndio afande hali si nzur hasa kwa hawa dadazetu
 
Sahihisho siyo 832 ni 835KV ( Kikosi cha Vita)
Hongera kama ulipata pafahamu Gendagenda,Komsanga na Kwa Bojo.
Hope ulitendewa Haki pale Uwanja wa Damu.

kambi ya mgambo ni 835kj...labda kama imebadilishiwa enzi zenu ilikuwa inaitwa kwa jina tofaut....umesahau na bwawani,machungwani na mjini kabuku
 
Ebana sie tulishafanyiwa uchunguz nov, 1. Kama mguu una uvungu 2. Unanyanyua mikono juu daktari anaangalia kifua chako ukiwa kifua wazi 3. Unaonesha mikono mbele na nyuma...tunasubiri kuitwa tena, je uchunguz mwingine wa kiifya huwa unafanywa au magonjwa gani wanapima? Au km tulifanyiwa huo uchunguz hakuna tena issue za vipimo? Kwa aliyejeshin anijuze plz
 

Kunyanyua mikono juu wanapima nn kwenye kifua?
 

Mkuu pia unaweza kupitia uzi huu: https://www.jamiiforums.com/habari-...1863-je-unakumbuka-nini-enzi-zako-za-jkt.html
 
kweli tz kwa usalama tupo nyuma hivi mnahakika na uraia wa aliyeleta uzi huu? na hizi taarifa mnajua anataka kuzifanyia kazi gani hamna uanajeshi hapo ni uraia tu mjeshi aliyeiva kijeshi angefunga mdomo shame on you

Hizi sio zama za mawe!!! Wanakohifadhi bunduki na mizinga ni halali kufanya siri. Sasa kuwafahamisha watu kuhusu mchakamchaka nako kuwe siri?
 

Mkakati wa watarajiwa wa JWTZ kUPITISHWA JKT ni ugoro wa watawala kutafuta kuingiza watu wao ndani ya JWTZ. JKT ni jeshi la kujenga taifa, liliwekwa kwa ajili ya wasio na ajira wakajiunge na kujifunza kujiajiri PAMOJA na kuwa wanajesi wa akiba wanaoweza kuitwa wakati wa dharura kutoa huduma za mwelekeo wa kijeshi. Waliokuwa wakilazimishwa kujiunga ni School leavers (X-FormVI na X-University) kabla hawajaiingia katika ajira. Madhumuni ilikuwa kujenga nidhamu yao, na kweli walikuwa na nidhamu hata kazi zao zilionekana hivyo. Mafisadi walikuwepo wachache sana.

Hawa wajanja wanaopeleka watoto wao JKT miezi 4 halafu wanawafanya ndio wenye sifa ya kujiunga na JWTZ ni waharibifu na matokeo yake mtayaona karibuni. Kuna "Shamsi Vuai Nahodha" mwingine atajiuzulu tu kwa ugoro wa wanajeshi hao.

HALAFU MNASEMA MNASHANGAA MAWAZIRI SASA WANASHINDWA KUONGOZA WIZARA ZAO HUKU MKIPELEKA NYENZO ZENYEWE ZA KUWAFANYA WASHINDWE KUFANYA KAZI. MAMA SITTA ALIPELEKA WALIMU BAMBUCCHA SASA MASAHIBU YANAMKUTA KAWAMBWA. NA KWA NINI KAWAMBWA NA SI MAJALIWA HAPO PIA UNABAKI KINYWA WAZI. HERI YAKE JAKAYA MAANA YEYE WAKIJIUZULU ANATEUA WENGINE, YEYE AAAAAAAAH!!!!!! WALIOSHINDWA NI WAO SIYO YEYE, YEYE YUKA AMERIKA.
 

Hahahaha, endelea na kuelimisha vijana mzazi. Huyo hajui kuwa youtube kuna mpaka video za navy seals!!
Majuzi nimeona edition moja ya achievements za navy seal team 6, ikiwa ni pamoja na maoni ya former members of the same team
 
Kambi. MANGE JKT KJ 245
CO. afande Sanga lt col
2ic .major Rajabu from znz
adjutant. capt Ngowo
lts Kajoro. mchina. Dr. lema
sgt. Wela
cpl. Mandevu mpu.u.zi sana huyu
vol. lcpl . Frida
operation. Nidhamu baada tu ya OKOA
 
Ambacho sitasahau ni siku moja afande alijisaidia kwenye mlango wa hanga akatusingizia. Tukapewa adhabu ya kuchukua kila mtu kidogo kidogo. Akajitolea mmjo kuzoa lakini wakakataa. Kila mtu alishika mpaka ikaisha.
 
Ambacho sitasahau ni siku moja afande alijisaidia kwenye mlango wa hanga akatusingizia. Tukapewa adhabu ya kuchukua kila mtu kidogo kidogo. Akajitolea mmjo kuzoa lakini wakakataa. Kila mtu alishika mpaka ikaisha.

Duuh hii kali . . .
 
Ambacho sitasahau ni siku moja afande alijisaidia kwenye mlango wa hanga akatusingizia. Tukapewa adhabu ya kuchukua kila mtu kidogo kidogo. Akajitolea mmjo kuzoa lakini wakakataa. Kila mtu alishika mpaka ikaisha.

Mlijuaje kama afande ndo kashusha mzigo ule mkuu? Yaan kama kumega ugali vile hahahahah!
 

ufundishe shule ya kata wewe mwalimu!?
 

Umenikumbusha mbali sana fisi maji mwenzangu! Unakumbuka kanali Mlay alikuwa akikasirika anatuita fisi maji? Kanali Mlay alikuwa mchungu hata kwa mkewe Cpt Mlay aliyekuwa catering officer wakati wetu! Tena bila shaka wewe ulipita 841 KJ wakati wa operation vyama vingi 1992-1993.

Namkumbuka aliyekuwa cheef cook wa F coy baadaye akaenda kitengo cha watu wenye nguvu cha kupasua magogo na kuni ambacho kiliifanya F coy kuwa mfano wa kuigwa kambini! Jamaa alikuwa poa sana kwenye maswala ya msosi siku nikijongo kwenda Idetelo shamba kwenye milaba ya mahindi.

Maishani mwangu sitasahau siku nilipokamatwa na MP nikikatiza uwanja wa ndege nikiwa nimebeba deli lenye chakula na dumu la lita 5 la ulanzi nilivyokuwa navipeleka kwa wenzangu niliokuwa nimewaacha Dubliganga wakipasua kuni! Nilirushwa kichura umbali wa mita 300 mpaka Kota guard na kupewa extra drill ya dakika 45 na kupelekwa mahabusu kisha kesho yake nikahukumiwa kifungo cha wiki moja!

Kuna siku tukiwa kijijini tukinywa ulanzi nyumbani kwa mama tuliyekuwa tunamwita mama wawili kutokana na kuwa na watoto mapacha, ghafla wakaingia maafande wakikamata kuruta na servicemen waliotoroka kambini kukatokea purukushani ya kujificha. Mimi nikaingia ndani ya gunia lililokuwa jirani na magunia ya mahindi yaliyokuwa yanapukuchuliwa na kujificha humo kimya huku wenzangu wakikamatwa na kupelekwa mahabusu!

Mafunzo ya mwaka mmoja niliyoyapata 841 KJ yamenifanya niwe mkakamavu, mwenye upendo na mtii kwa watu wa rika zote mpaka sasa! Nawakumbuka Amandus Manda, Juma kisyeri, Wangson Waya, Widala Malaba,Boniface Mwangole, Marehemu afande Israeli, Afande Cpt Koka, Afande Cpt Kweka, Afande Lucy, Afande Kawawa, wana Serengeti (makuruta wa kike) na wale wote waliokuwa wanapenda kusimamisha minazi usiku wakati wenzao wanapokuwa wakiimba nyimbo disko!
 




Nilikuwa operation Kujihami mwaka nadhani 1982. Nilikuwa Makutupora, tukaenda kozi ya
uongozi Ruvu tuliokuwa tumemalizia A level shule za mchepuo wa kijeshi. Kozi nadhani ilikuwa miezi sita.

Tulivyofaulu tukaenda kwenye gwaride la sherehe za Muungano hapo kurasini.
Tulipomaliza tukatawanywa tena wengine wakabaki hapo wengine tukaenda kumalizia mwaka Mbweni JKT. It was a nice experience na nivizuri km ukibahatika nenda kajifunze ukakamavu.

Ni mengi hasa tulipokuwa Makutu hadi Ruvu, wali wa Vibwende nk. Those days na simba wa Ruvu Mola mkubwa.
Happy New Year.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…