Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Mimi nilikuwa Mafinga JKT na baadaye as a Serviceman Itende JKT , Mafinga nilikuwa C Coy na Itende nilikuwa D coy….
Nkaumbuka sana mambo muhimu yafuatayo:-
1. Mchakamchaka
2. Kilimo cha mahindi Idete(Mafinga), Kahawa Itende (Mbeya)
3. Kwata zote 72 (kama sijasahau)
4. Disko la kila jioni (kuimba hata kama hujui)
5. Fatiki (hasa za kufyatua matofali under Captain Waziri kule Mafinga
JKT ilitufunza uzalendo wa kweli na ukakamavu! Vijana wa siku hizi ni buree kabisa
 
"Ahsante mheshimiwa.vipi kuhusu target ya kuingia jwtz au intelligence inakuaje hasa ili kukamata hizo nafasi?na kama una professional ya IT and Network Engineering uhakika upo wa kupangiwa hiyo au ndio unaweza kutupwa kitengo kingine?"vipi kuhusu hili wadau?
 

Wewe njoo mengine utajifunzia huku taratibu,maana hapa msha anza ongopeana.
 

We ni nanga kuna info kama mshahara wa askari ni wapi unaweza kuona zaidi ya mhusika na mwajiri wewe unamwaga tu baadhi ya info kweli hazina shida ila wewe ni nanga ndio maana hujui info gani utoe na zipi udisclose yaani unatekenywa kidogo tu unajianika mpaka basi hii inaonesha uzalendo na jkt kwa ujumla ulitoka patupu. Hujui hata vyeo na kuhusu wazungu na mafunzo yao zile ni action kama wafanyavyo kina Anold, Rambo n.k na hufanywa ili kuhadaa wajinga kama wewe muone no secret na kutoa yenu wakati yao yapo intact. Kwanini wanamsakama Edward Snowden kama no secrets? Acha umbumbu kama askari wenyewe ndio kama wewe basi we are finished. Nenda Rwanda tu hapo jifunze waavyoishi na kuhusu TMA kufundisha mataifa ya nje au wakwetu kusoma nje. Kwanza jua military knowledge ni kama biology au physics principles na mengine ni hayo hayo world wide ila hautafilundushwa siri za nchini mwao mfano mambo ya mishahara ni siri, aina ya silaha mlizonazo na location na idadi ni siri kasoro tu zitumikazo katika nafunzo, na mengineyo amayo pia siwezi mwaga hapa. Ndio maana kuna wasemaji jamani si kila mtu anaropoka tu tena hapa. I wish ningekujua nikuelekeze baadhi ya impact ya haya mnayomwaga humu ninauzoefu na ninayaona yakitokea again mnawapa shida saaana makamanda wetu. Raia tunapenda mwende jeshini maana nchi ni yetu sote lkn nenda tu kwa mshauri wa mgambo wilayani au mkoani utapata info zoooote utakazo au nenda jkt kikosi chochote utapata info au Kikosi cha Jeshi pia usiogope vaa vizuri nyoa vizuri basi kika kitukitakuwa poa. Athari za kutaja mishahara na nengineyo unamrahisishia adui kujua what price may b paid to buy a combatant au waji.ga kama wewe kisha wakamwaga kika kitu. Naamini huyo si msoja maana angejua tu kuwa Islael waliingia vitani sababu ya Private tu kama angekuwa hajui kitu au hana maana wangesubiri atekwe General ndipo washtuke. Hata civilian tu anayejua haari japo kiduchu inatosa kuangamiza jeshi kwa taaria yako achilia mbali soldier. Vita vya Islael na waarabu chini ya AbdielNasa wa Egypt aliyeharibu mission ni secretary tena kwa kusema tu boss yupo na wageni wanasherekea ikatoshakuangamiza mission yote
 
Kwanini wakina Aisha na Joyce huliwa sana wakiwa JKT?
 
Ukitaka kumla bata usimchunguze we unataka kazi njoo mengine utakutana nayo huko huko kwani wao wameweza ni maroboti.GO FOR YOUR DREAM.
 

habari mkuu apakak! mimi naomba kufahamishwa kwa mwaka huu mafunzo hasa yanaanza lini rasmi?
 
Last edited by a moderator:
Unatoa hadi mshahara hadharani kweli wewe nanga japo inaonesha hujui kitu lakini si vema kutoa info kama mishahara hizo ni confidential matters/ unataka kujifanya umefika mpk TMA lkn yaonesha ulibebwa mbeleko ya chuma kama hujui vyeo, umeulizwa mkasi na .... umechemka. Hakuna mwanajeshi nanga kiasi hicho lkn pia jua nini kinaweza kuelezwa hadharani na kipi ni classified (tambua daraja la usiri) ndio maana kuna wasemaji wanajua what to say in public
 
Dah,noma sana yan wametoa nafas za jkt lakn watu wa diploma na degree,hakuna maana kuna age limit,so ubaguzi had jeshini,sasa wenye degree itakuaje hapo
 
Cadets wanatoka jkt

In short ili uajiliwe jeshini lazima upitie jkt

Baada ya miezi sita jkt unaenda miez 4 JW kozi ya TS

Baada ya hiyo miezi minne ndo unakuwa eligible for army officer training

ahsante mkuu kwa maelezo mazuri!

naomba kufahamu kwa wale ambao wanaenda uhamiaji, process zao zikoje?

na pia naomba kujuzwa katika idara ya uhamiaji wanachukua watu wa sifa gani?

ahsante!
 
ahsante mkuu kwa maelezo mazuri!

naomba kufahamu kwa wale ambao wanaenda uhamiaji, process zao zikoje?

na pia naomba kujuzwa katika idara ya uhamiaji wanachukua watu wa sifa gani?

ahsante!

Mkuu,

Kwa mfumo wa sasa vyombo vote vya ulinzi na usalama vinachukua vijana wake kutoka jkt

Ukimaliza kozi ya recruit "ukuruta" miezi sita unapanda cheo unakuwa service man

Kipindi hicho cha u-serviceman ndo wanakuja vyombo mbali mbali vya ulinzi na usalama kufanya udaili kutokana na mahitaji

Polisi,mgambo,magereza,uhamiaji,tanapa,jw wapo wazi wakati wa kudaili ila TISS wanadaili serviceman "kiajabu" zaidi

Kuhusu vigezo vya uhamiaji uwe physically and mentally fit
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…