Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

unapakuliwa ugali, mchuzi wa nyama mwepesiii, na bonge ya fupa halina nyama, unauliza mbna umenipa mfupa mtupu? Unajibiwa kaumbe ng'ombe wako asiye na mfupa umlete tumpike
Jamani naona bulombora nilikuwa peke yangu, mbona wote wamekaa kimya, lakini nimecheka sana loo oh Dunia imebadilika hivi, those were the days
 
Sitosahau siku nimetoroka kambini Mgambo jkt Tanga na kurud nyumban kwa issue ya kufuatilia chet changu cha 4m 4 kwa muda wa cku mbili na ya ta3 nikarud na kupigwa <doso> na private na kudek bweni kwa nguo nilizokuwa nimeva (green vest and pt short~bukta) nilijuta kuingia jkt na aliamua kunipeleka mahabusu na nikafunguliwa maxhtaka na kuhukumiwa kifungo cha week 2 na kaz ngumu <kulimia michungwa> nilinxhukuru mungu kumaliza mafunzo ya miez 6 mpaka xaxa nimekuwa axkari mzuri xana, jkt ni chombo ambacho kinakufanya unakuwa na uzalendo na nchi yako. JKT nzr karibun makamanda 2we weng.
kutoka Ruvu kuja kuchukua vifaa mgulani, nilipata nusu saa ya kwenda kumuona mama yangu ( marehemu) , sijapata kuona akilia namna hiyo baada ya kuniona nilivyokuwa Mweusi na Mwembamba kama Mpini
 
dah mtoa Uzi umenikuna sana kwanza sababu Mimi hadi kwa sasa npo 832KJ op muungano. kwaio Mkuu unawapata kina Afande Shika, ndomba, skaponda, mgimbe,kaonde etc. vp kwa dosa?
 
AH 3570 OP MIAKA 50 JKT intake ya pili Jun 2013-Sep 2013 Mujibu wa sheria 832KJ Rvu JKT...dah..!!! sitosahau tulivoteseka na wananiboa eti saiv Ruvu wanaenda wale wagonjwa wa kuangushia
 
Nakumbuka hii kitu kutafuta samaki
 

Attachments

  • 1422180261221.jpg
    1422180261221.jpg
    10.2 KB · Views: 690
mgambo nilikaa mwezi tu; kwani nilichangamkia bogi la maramba; ticket ilikuwa packet moja ya sigara-sm.

Maramba nilikuwa ikulu, kila week end tanga nyumbani; nikirudi mkate, sukari na sigara quater gurd ilikuwa kwa wengine wasikuwa na 'mm' kama hizo

Unapakumbuka hapa??
 
Nilikuwa oljoro f-coy, nilienda bila kuaga watu wangu wa karibu hapa mtaani nilivyorudi nilisemwa kila kona kuwa nina ngoma wakijua nimetoka shule. Habar hizo nilizipata baada ya kurudia hali yangu ya kawaida kwan nilikuwa nimekonda sana + na paraa kali la wembe
 
mkuu skaponda si alikua mgulani au wamemuamisha ?
dah mtoa Uzi umenikuna sana kwanza sababu Mimi hadi kwa sasa npo 832KJ op muungano. kwaio Mkuu unawapata kina Afande Shika, ndomba, skaponda, mgimbe,kaonde etc. vp kwa dosa?
 
ni kumbukumbu nzuri sana nimefurahi, japo ni muda wa miaka 35 tangu nitoke jkt, 831kj mafinga, op tija c coy
 
ni kumbukumbu nzuri sana nimefurahi, japo ni muda wa miaka 35 tangu nitoke jkt, 831kj mafinga, op tija c coy

Kuweka records vizuri, Mafinga JKT siyo 831KJ ni 841KJ. Lakini kwa miaka uliyopita heshima kwako mkuu. Mimi nimepita JKT miaka 22 iliyopita Oljoro JKT, lakini Mafinga JKT naifahamu.
 
enzi zile makamanda hawakuwa na shule kabisa na walijitahidi kukariri maneno machache ya kingereza na kuyatumia kila mara.....nakumbuka ile adhabu ya push up!!!!!afande atakwambia ....haya...chini!down!chini!down....akimaanisha juu ..chini sasa ujifanye hujamuelewa!!!cha moto utakiona kwa kujifanya msomi!!!
 
Back
Top Bottom