Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Wale wa Makutupora na Ol joro.....

Oyaa basi hapo Makutopora a.k.a Makutu, mnakumbuka ule mlima Kitunda? Ilikuwa ndo sehemu ya kufuata mawe ya kujengea. Basi kulikuwa na maandishi kibao yalioandikwa na intake zilizipita. "Wanyani" nilikuwa kombania ya mtunduruni E-coy operation miaka 25 ya JKT namkumbuka afande Msalaba, Semwenda a.k.a masikio. Basi huendi usawa wa guduria bila kunyakua. Embu waliopitia makutu operation hii tukumbushane mengine kama kichele maana mtu unalipwa 300/- kwa mwezi just imagine. Ila sidhani kama kuna sehemu poa kama jeshini
 
Ooh wanikumbusha bulombora op nidhamu.nawakumbuka afande sura ya kufa,Ghadafi, meja chale ,sijasahau zile dagaa ni misamaki ile jamani mpo?nawatakia uchaguzi mwema.
 
Kwa nn camp za Kigoma zinaaminika kutoa vijana wa JKT wakakamavu kuliko kwingine?

Wale wa Bulombora mnakumbuka kwenda kucheza mpira Kaseke na roli halina taa?mkirudi jioni barabarani kwenye lile daraja bovu tunavuka kwa kuwasha njiti za kiberiti.

Nafurahi sana kulitumikia taifa hili. Jeshini raha jamani, yale mateso ndiyo mbegu ya ukakamavu wetu mtaani
 
Wewe kuna camp inatwa chita..Kuna Buhemba,kuna Masange zote ni kambi hatare
 
Ooh wanikumbusha bulombora op nidhamu.nawakumbuka afande sura ya kufa,Ghadafi, meja chale ,sijasahau zile dagaa ni misamaki ile jamani mpo?nawatakia uchaguzi mwema.

Usisahau kiwanda cha chokaa ni nouma kabisa kupandidha magogo kwenye TANURU duuu hongera 821
 
Makutopora operesheni miaka 25 ya JKT ilikuwa nouma! Yaani hapo kombania ya mtunduruni a.k.a Eagle koy. Kwa afande msalaba, semwenda (masikio)
 
Dah nakumbuka 841kj pale mafinga .... Jkt ya zaman ilikuwa na mafunzo mazur sana... Sitawasahau makamanda hawa. Lt nkya, Lt liundi, Lt alloys, na wiliam Sagala... Mpaka leo nina alama mgongon na mkono wa kushoto... Nilichimba handak kwa sahan na panga
Mkuu mafinga ni balaa nilikuwa b coy kuna afande anaitwa saa ya mkebe akiwa anataka muimbe mpaka sauti isikike kwa mtoto wake Tony alieko changarawe pia mkiwa fatiki ili upate tano lazima upige picha na ukimlipa pay unakula tano za nguvu, pia mkono wa chuma kabla hajaongea tayari kashakupiga kibao pia bila kupasahau shambani kwa mwamunyange full maziwa na mayai baada ya fatiki saa nne
 
Kuna kamanda wetu mmoja, alikuwa na mambo ya kipuuzi sana huyu bwana.......kuna cku akatukuta mi na wenzangu kama watano hivi akaanza kusema:- yani leo mwili wangu una hamu sana ya kupigwa pigwa, nyie kuruta hebu njooni hapa mnipige......tukabaki kushangaa....tumpige tena...... ghafla kwa ukali akasema pum**fu mnakataa amri ya kiongozi wenu subirini mtakiona cha mtema kuni...... tukaangaliana usoni tukasema tumuwahi kabla hajafika mbali tumpige ili kuondoa huo uzia....... tukamvaa na kuanza kumkung'uta.......weeeeeeeee........jamani hapo ndo ilikuwa balaa kwetu jamani hata huwa ctaki kukumbuka adhabu tuliyopewa kwa kosa la kumshambulia kwa kipigo kamanda wetu
 
Back
Top Bottom