Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Tupo Mlale Tupo. Afande Nguvu ya Nyani, Rweikiza. Sabuni, Mande, Chuma, Matron Grace na MWajuma Magagula na Lusonga sitaenda tena. Maafande wa Mlale watanisurubu! Dah Shamba la Embakasi. Ukarimu wa Wangoni watani zangu! Jamani ni kumbukumbu nzuri. Wimbo wangu daima ulikuwa ' Nimeuona mpilipili na maua yake nselema......' Ile nyumba ya mbao iliyokuwa ikihamishwa na Kuruta Dah!
Dah noma sana watoto wa mpuku
 
Mlale JKT- ruvuma jamani mko wapi? Kwa wenyeji kule chakula kebekebe tena ugali mkubwa wa makuruta shurti kusongwa na wanaume. Halafu ugali bure mnanunua tu mboga- maarufu kule kiti moto. Embakasi shamba la mahindi. Unapewa palilia mistari 3 ambayo unaona mwanzo tu mwisho wake huuoni.
Maafande: Nguvu ya Nyani ( a.k.a yake), Rweikiza, madame Grace ( Matron), Afande Sabuni, Mwaipopo, Mande??, Chuma n.k!
Tupo mkuu ila mie op kikwete
 
Ukijongo andaa nguvu sasa nyie nguvu hamna halafu mnadoji

Lazima mnuke mavi tu
[emoji23] [emoji23] ....
Hili songi "....sauti ya afandeee, inanichunguliaaa,hata kama nikidojiiiiiii inanichunguliaaa...."

Ukijongo usikae angani, kaaa around na eneo la CoY...ikiwezekana unafanya uchunguzi kama wiki hivi, bt usi doji daily, doji siku unayoona leo nisipo lala nitadata.
 
nakumbuka wimbo wa ---Tutawakumbuka makamanda wetu waliokufa kwenye mapambano...
Bhana huuu wimbo, una nkumbusha tulikuwa tume doji chimbo moja hivi.

Mara nyingi sio mbali na eneo la kazi ili movement za kurudi zikianza tusikie na kuanza ku move.

Sasa kuna muda mchiz wangu niliyekuwa naye , alikuwa kamwaga mate tu, huku anaota mindoto yake.

Ile ndoto ilimpelekea katika tukio kuwa tulidakwa na afande mmoja mnaaa kichizi, katupiga tifu jamaa aka kata ringi, hasa watu wakaenda kutoa heshima za mwisho.
Hii ndoto , ukijumuisha na hiii nyimbo anayo isikia kwa mbali, ili mfanya jamaaa aanze kupiga kelele acha tu....
 
Umenikumbusha B-Coy Mgambo JKT OP Kikwete 2015 mkuu.Kabeya alikuwa tall fulani hivi na English yake ya this time tomorrow.Wame nilikuwa simpendi kinouma maana jamaa alikuwa hatari sana kwa madoso na route za shamba.Matroni Beatrice alikuwa mrembo kinouma ila roho mbaya mamaeeeee.Kama kweli wewe ndio yule Amos basi nishakusoma mkuu.

Wapi GendaGEenda na Komsanga.
Hatari bravo coy mkipangwa shamba na wame mmeumia nawakumbuka kina mgeta kina agustino na yule ahadhi mnoko kishenzi[emoji2] [emoji2]
 
2001 operesheni Mkapa ruvu Jkt,A-coy mpo??bila kumsahau Afande salamba,kifaru ,kimpingu,mwambingu,na wengineo leo nimekumbuka mbali mno
 
Maisha safari ndefu sana Op mkapa A-coy tulikuwa na kuruta mwenzetu alikuwa alikiw anaitwa Henry paul kinemelo,Now ni major kuna siku nilimuona Ubungo,huyu jamaa sasa nakumbu wakati tunaanza kuingia kambini ruvu tukitokea mikoani,sisi wa kutoka mkoa wa Dar es sallam tuliwa ruvu pale sasa kama ujuavyo wadareslam tuna kawaida ya kujifanya sisi ndo wajuaji wa kila kitu,wakaja jamaa wa kutoka Rukwa bwana ,sisi tumetangulia tunajifanya tunajua mambo yote,wakati wa kukesha usiku huyo jamaa niliymtaja hapo juu akajifanya ni afande achamkua mmoja wapo wa wageni kutoka rukwa akampeleka kwenye giza akaanza kumpa doso la nguvu,la haula kumbe kuna afande intelegence oficcer kavaa kama kuruta kachanganyika na sisi,sisi tunajua ni mwenzetu kumbe kila kitu kinachofanyika kati yetu kinafika headquoter kwa wakati,sasa likaitishwa paredi la utambuzi ili yule jamaa aliyepewa doso amtambue alimuazibu,bwana weee Hendry akatambuliwa moja kwa moja akatermshwa main guar selo moja kwa moja adhabu ikaanza kesho yake,iyo kesho yake mi wakati wa chai mkiwa mmekusanyika wote ,iyo kazi aliyopewa Hendry ili iwe fundisho kwa wengine walahii akuna aliyeweza hata kunywa chai kwa asubuhi hiyo ,alafu mbaya zaid iyo adhabu inakwenda kwa siku tatu mfululizo,JKT ya op Mkapa inabaki kuwa ya pekee daima.
 
Ni kweli tulikuwa tunajifunza ukakamavu na mbinu nyingine za kukuwezesha kuishi. Ukifika wakati wa kwenda "usawa wa gudulia" hapo ndo palikuwa na tatizo. Utakuta afande "anatoa ruti" na anasema atakamata watatu wa mwanzo, kwahiyo wengine mnaendelea kukimbia huku njaa unauma! Operation NIDHAMU
 
Duh, nilikuwa Mgambo JKT operesheni Nidhamu 1986/87 Kombania C kombania ya demo. Kabla sijaripoti pale ilikuwa nimepangwa kwenda Masange Tabora lakini ajabu siku mbili mfululizo train haikupita pale Korogwe station kumbuka tulikuwa tunapewa hati za kusafiria bure ikiitwa warrant.

Sasa siku ya pili nilikuwa na baba mzazi akatokea afande na kutuchangamkia ile mzee kusema tumekosa usafiri yule afande akaunganisha kuniambia njoo Mgambo kila kitu kipo kama ulaya nikakubali. Walitupokea kwa ukarimu na upole sana nadhani kwa kuona watu wengi walikuwa wanatoroka. Lakini lo mafunzo yalipofunguliwa ndipo tulipogundua jeshi siyo mchezomchezo.
Kisa kimoja kidogo ntakieleza hapa siku ya pili kambini tulipelekwa kusomba tofari na maji katika ndoo, sasa kuna kuruta raia mwenye asili ya kihindi alibandikwa ndoo ya maji kichwani, ilikuwa shida yaani ni kutetemeka na kuyumbayumba, basi afande akamkemea na kumwambia wewe kesho utatoroka, na kweli jamaa siku ya pili hatukumuona tena.
Kuna mikasa mingi sana fikiria ilikuwa ni mwaka mmoja siyo mchezo. Hata hivyo sijutii kupitia JKT kuna mengi yametujenga kuwa hivi tulivyo.
Wewe tulikuwa operation moja (NIDHAMU) tulianzia kambi tofauti lakini tukawa wote Maramba kwa major Urio kama sijakosea. Maramba uraiani tulikuwa tunatafuna nazi kama vile hatukuwa na akili nzuri!
 
Hatari bravo coy mkipangwa shamba na wame mmeumia nawakumbuka kina mgeta kina agustino na yule ahadhi mnoko kishenzi[emoji2] [emoji2]
Nishakusoma, ww si ulikuwa ST ? mimi yule Doja ambaye siku ile tunagaiwa kombani nikairuka ile aliyonirushia ahadhi....mkala doso mlipo mzomea hahahaaha raha sana jkt...
 
Wewe tulikuwa operation moja (NIDHAMU) tulianzia kambi tofauti lakini tukawa wote Maramba kwa major Urio kama sijakosea. Maramba uraiani tulikuwa tunatafuna nazi kama vile hatukuwa na akili nzuri!
Duuuh.. shikamoo kaka hiyo 1987 ndio nimezaliwa [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Back
Top Bottom