Mimi nimepita 821 KJ kwenye OP Miaka Hamsini ya JKT.Nilikua kombania F chini ya sargeant major Abednego na O.C wetu alikua Lt Ntwa (RIP) baade Lt. Sheng'oma Wakati huo C.O alikua Major Mrosso ambae alistaafu mwaka uliofuata.
Namkumbuka private mwenye visa na vituko sana anaaitwa John a.k.a Wezele Wezele ,namkumbuka matron Manento ,namkumbuka Lt. Minzi na Mwakibinga na private mnaa wa kwata kikosi kizima anaitwa Tarimo
Moments za bustani,shamba la mahindi na mkesha pale uwanja wa damu.Mbio za cross country na mazoezi ya pori na kupiga risasi bandia kule kwenye vijiji vya raia
Kikubwa kuliko vyote nakumbuka chenja aisee
Namkumbuka afande RSM Mundeba E.B[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ana mikwara ni hatari