Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Kama kichwa cha habari kinavyojieleza.
Em kama kuna watu humu waliopitia JKT kuanzia op Miaka 50 ya uhuru/ya JKT op sensa na uzalendo.
Naomba mje tupige swaga kidogo kama atakuwepo aliepita 821 itapendeza zaidi.
Mimi ni op Uzalendo.
Karibuni.
Mike umenikumbusha kitambo sanaa, kurutu ni mdudu, nimemtafta sana malela, mguu mbele mguu nyuma, ubata ubata, kuroli, kuna Afande alikua anaanza kujipiga nua kama ndoo 5 ivi, inamaanisha kinachofata ni nua mwanzo mwinga, Afande Meja mtoto hatari sana, tobo tobo kawaida asubuhi ileeee! Ni kula doso na kufanya kazi za watu, Usawa wa kulia,Over.
 
842KJ MlaleSongea. Op miaka 50 ya jkt. A- Coy private Mahamud na private Matiko walikuwa ni faya.
Matiko alichezea miezi 3 kwenye mahakama ya kijeshi baada ya kutembeza doso kwa dogo mmoja hadi akazimia. Mwendo wa kukwepa ndege haukumuacha salama.
Wapi afande kitomari?
Baba wewe tulikuwa intake moja.Mimi nilikuwa Denjalo na akina afande Veno, Nyingo, Mshanga, Gwamaka, Erasto n.k kwa CO Major Mpuku ! ILIKUWA NI MOTO.Saiv nahtaj kurudiko mazima lkn usawa ni tight vbay Kamanda.
 
Bulombora ya demo 821 kj kitambo sana maafande hawa sitakaa niwasahau
1.silima huyu jamaa kwenye mkesha alikuwa mnaaa sana..[emoji16] [emoji16] hatoi tano hata kidogo
2.mwakibinga
3.mpemba
4.Nguyanyi huyu afande anapenda salala na kujira hatari
5.Ngwashu huyu afande alikuwa na nyimbo zake burudani sana
7.Fred huyu afande yuko vizuri sana kwenye kwata
8.simfukwe huyu afande ukisikia filimbi yake uwe umeshafoleni kombania
9.RSM Mundeba utamsikia wote kwa ujumla.....[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]

Maisha ya jeshi ni raha sana nakumbuka kunasiku afande mpemba alituambia haya maisha uwezi ukaishi sehemu yeyote ile maana nikikumbuka jinsi nilivyokuwa na doji na jinsi nilivyokuwa napewaga doso ni hatari
Mwakibinga nmekutana nae mwaka jana milambo tabora amekua captain
 
842KJ MlaleSongea. Op miaka 50 ya jkt. A- Coy private Mahamud na private Matiko walikuwa ni faya.
Matiko alichezea miezi 3 kwenye mahakama ya kijeshi baada ya kutembeza doso kwa dogo mmoja hadi akazimia. Mwendo wa kukwepa ndege haukumuacha salama.
Wapi afande kitomari?
Matiko n hatari Mimi nilikua C-Coy kwa afande chavala na R.P mshanga huyu alikua anakupiga doso hadi uhisi upo course ya ukomando
 
Baba wewe tulikuwa intake moja.Mimi nilikuwa Denjalo na akina afande Veno, Nyingo, Mshanga, Gwamaka, Erasto n.k kwa CO Major Mpuku ! ILIKUWA NI MOTO.Saiv nahtaj kurudiko mazima lkn usawa ni tight vbay Kamanda.
Mimi nilikua o.p miaka 50 ya muungano mshanga alihamishiwa C coy n hatari huyo kamanda cku tumedoj kombania na wana akaja saa 6 kutuamsha alitupiga doso had saa 9 afu baada ya hapo bustani
 
Mimi nilikua o.p miaka 50 ya muungano mshanga alihamishiwa C coy n hatari huyo kamanda cku tumedoj kombania na wana akaja saa 6 kutuamsha alitupiga doso had saa 9 afu baada ya hapo bustani
MSHANGA BHANA, ET KURUTUUUU... "NITAKUNYAKUAAAA ? WE TEATEA TUU " HAHAHAH YULE JESHI LIKO DAMUNI
 
835 Kj tupo pamoja Mgambo.

Route ya chai
Vipi unamkumbuka Private magera? Asee ilikuwa noma sana
Magera namkumbuka mkuu.Kama sikosei OP yetu alikuwa Danger au Eagle Coy ..

Kuna koplo alikuwa anaitwa MAYAI.Huyu jamaa ukikutana nae tu ujue umeisha(hata kama huna kosa).

Kuna kamanda mwingine anaitwa KABEYA na BABU WA LOLIONDO..
 
MSHANGA BHANA, ET KURUTUUUU... "NITAKUNYAKUAAAA ? WE TEATEA TUU " HAHAHAH YULE JESHI LIKO DAMUNI
Akija kuamsha mchaka mchaka au bustani utasikia anapita katikat ya hanga anasema "we lalaaaaa si ulikuja kulalaa" hapo ishatoka sa we usiamke
 
Akija kuamsha mchaka mchaka au bustani utasikia anapita katikat ya hanga anasema "we lalaaaaa si ulikuja kulalaa" hapo ishatoka sa we usiamke
Ahahah nna namba yake ya simu bhan, huwa nafurahia sana nikongea nae nikakumbuka madoido yake hahah
 
835KJ

Muimbishaji:Braaaaavooooooo coy oyeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee,
Wote:Ayeee
Muimbishaji:Bravooooo
Wote:Ayeeee
Muimbishaji:Braavoo mamaaa
Wote:Ayeee
Muimbishaji: 😛Piga kelele na shangwe
Wote:Keleleeee
Muimbishaji: 😀Dushee
Wote:Kelele za shangwe
Niko michungwani naelekea bwawani hapa,
 
Mimi nimepita 821 KJ kwenye OP Miaka Hamsini ya JKT.Nilikua kombania F chini ya sargeant major Abednego na O.C wetu alikua Lt Ntwa (RIP) baade Lt. Sheng'oma Wakati huo C.O alikua Major Mrosso ambae alistaafu mwaka uliofuata.

Namkumbuka private mwenye visa na vituko sana anaaitwa John a.k.a Wezele Wezele ,namkumbuka matron Manento ,namkumbuka Lt. Minzi na Mwakibinga na private mnaa wa kwata kikosi kizima anaitwa Tarimo

Moments za bustani,shamba la mahindi na mkesha pale uwanja wa damu.Mbio za cross country na mazoezi ya pori na kupiga risasi bandia kule kwenye vijiji vya raia

Kikubwa kuliko vyote nakumbuka chenja aisee

Namkumbuka afande RSM Mundeba E.B[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] ana mikwara ni hatari
Danger coy ya mpemba
 
Magera namkumbuka mkuu.Kama sikosei OP yetu alikuwa Danger au Eagle Coy ..

Kuna koplo alikuwa anaitwa MAYAI.Huyu jamaa ukikutana nae tu ujue umeisha(hata kama huna kosa).

Kuna kamanda mwingine anaitwa KABEYA na BABU WA LOLIONDO..
Hakuna kamanda aliyekuwa anatisha kama babu wa loliondo
 
Back
Top Bottom