Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

sintosahau mkesha wa 'usiku wa mwafrika' pale ruvu uliosimamiwa na luteni chahe akishirikiana na kapteni mhagama na akitanda
Mzee umenikumbusha Chahe aiseee. Huyu jamaa ana roho mbaya Malaika mtoa roho akasome. Ana rafiki yake ngaugula Ni wanna sijapata ona.
Akitanda alikuwa poa sana, Mara kibao amenibeba pale ruvu.
 
Hahaa. Kombania C, kombania ya demo, mberee temb... Hault! Hapo ni Mgambo JKT Operation Nidhamu, wiki 2 za mwisho adhabu Kali kwa tuliochelewa foleni ya kwenda kula tukidhani hakuna shida. Shikamoo jeshi, Nina nidhamu za kutosha!
 
Hahaa. Kombania C, kombania ya demo, mberee temb... Hault! Hapo ni Mgambo JKT Operation Nidhamu, wiki 2 za mwisho adhabu Kali kwa tuliochelewa foleni ya kwenda kula tukidhani hakuna shida. Shikamoo jeshi, Nina nidhamu za kutosha!
Nimewapikia Vijana chai kwa maji ya visima sanaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Kulaa sana nyamaa pale jikonii wana wakiwa wanalima kwa msanga kuleee[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mabio nakimbilia kwenye machungwaa kule kisimaniii
 
Gendagenda Komsanga kwedzinga bwawani
Hahaa. Kombania C, kombania ya demo, mberee temb... Hault! Hapo ni Mgambo JKT Operation Nidhamu, wiki 2 za mwisho adhabu Kali kwa tuliochelewa foleni ya kwenda kula tukidhani hakuna shida. Shikamoo jeshi, Nina nidhamu za kutosha!
 
Nashauri Jeshi lifikirie umuhimu wa kutoa beji "Nishani" za JKT kwa kila "Operation" zilizopo na zilizopita ziuzwe au zitolewe bure kwa askari wote wa akiba,.... mujibu wa sheria na wa kujitolea waliohudhuria na kufuzu kwenye makambi yote ya JKT, Ili kwenye sherehe za kitaifa wale waliopo Duniani bado waweze kuning'iniza nishani zao. Nawasilisha!
 
Mi ni juzi tu operation miaka 50 ya jkt July -sept 2013 cjui Kama nimepatia Mana nishasahau.Nilikua kombania A mlale jkt,kulikua na afande mmoja msolid kidogo yeye zamu yake alikua anatuamsha kwa kudondosha Sahan ya bati chini,siku moja nilipatikana nilkua nimedoji kwenda bustani alinipa doso mpaka Leo nalikumbuka.

Siku ya Kwanza naliport kambini tunaambiwa eti sisi Cha kwetu ni roho tu lakini mwili niwa jeshi,c.o amewaagiza kuua takribani kadhaa kwa sababu mwaka ulioisha waliua wachache Apo nilihisi kufa kufa sema tulikua tumepelekwa naserikali kwa mujibu wa Sheria nikakaza.

Lakini pia watalaam wa kudoji tulikua tukiamka fresh,tunafoleni nje tunahesabu namba Kama kawaida,pale mabogi yanavoelekea bustani kwa mchaka mchaka mkali na chenja juu Basi tunavizia kigiza nyuma ya mti tunajificha.Bogi lote likiisha tunageuza kuumunya hangani.Saa kumi na mbili wakigeuza wanapofolen master parade Basi na sisi tupo tunahesabu pamoja.

Kuna mashamba ya mahindi mlale jkt yanaitwa embakasi ni mkubwa usipime kiangazi yote tulivuna mahindi,kuyasomba,kuyachambua mahindi dume na jike,kupukuchua,kuingiza garani n.k

But nimemiss kwata Sana moja ya vitu nilivyokua napenda Sana ni kwata Hadi Leo ukiniamusha usingizini nakupigia Bado nazikumbuka baadhi.
 
Asubuhi saa 4 silece 1 ya mkate na kimombe Cha chai Cha bati,mchana ugali nyama,mwanzo mtu unakula unashiba na ubakisha mpka wadada wanakuongezea lakini kadri siku zinavyoenda unatamani sufuria lote uachiwe wewe tu mpaka wadada wanakaba ukoko sio poa si kwa tifu lile
 
Namtafuta afande wangu maìsha yangu yote nimekuwa mzee nimestàfu nina hakika kwa umri ule atakuwa amestaafu.
Alikuwa ni staff Sajenti by then 1986 Ruvu JKT aliokoa maìsha yangu malaria ilipanda kichwani akalazimisha gari main gate nipelekwe Tumbi Kibaha wakati huo kulikuwa na outbreak ya ķipindupindu na homa ya uti wa mgongo(meningitis ) kwa weledi wake akalazimisha gari itoke kama sìo leo ningekuwa RIP namtafuta huyu mutu alikuwa anaitwa staff Sgt Shelukindo
Alikuwa Dr huyo shelukindo??

Kuna Dr mstaafu ana Clinic pale mlandizi alikuwa ruvu jkt
 
[emoji24][emoji24][emoji24]pole sana mkuu, hakika kila binadam ni muhim hapa dunia, maafande wangu wa Roadgan, kuku coy, main get mamaangu mpendwa kamanda Mamuya mkuje huku, wananchi wazalendo tuko pamoja, I miss them very much..


Namiss sana hanching hanching position[emoji58][emoji58]
Hahahahaha Mamuya mbabe huyu
 
Back
Top Bottom