Mimi nilikuwa OperesheniTIMIZA nikiwa na maafande wachache ninaowafahamu pale Ruvu, Marehemu Makame Mkuu wa Kambi, Urio nakumbuka alikuwa Luteni, Londo, Agnes, Afande machibya aliyewahi kuwa Mkuu wa Mikoa kadhaa etc. Nakumbuka sana kuchoma nyama porini hasa tukiwa zamu ya kupika, pili kula mayai mabichi hasa ukipangwa kwenda kufanya kazi kwenye mabanda, tatu siku Bendi ya muziki inapotumbuiza siku hiyo kwenye kambi la Ruvu. Mwisho hakuna ya Mwanamke au Mwanaume wote siku ya kwanza mnatupiwa bukta/pitishot ya kuvaa na ndiyo sare ya kila siku. Kweli ilipendeza na pale mara chache kuugua sababu ya mikiki mikiki ya pale.