Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Wanangu wa rwamkoma sasa tujuane..
Captain hassan(saivi meja),kinana
Wanoko Kama jeneza, shebuge.
Mimi Op:Tz ya viwanda
 
Mimi nilikuwa OperesheniTIMIZA nikiwa na maafande wachache ninaowafahamu pale Ruvu, Marehemu Makame Mkuu wa Kambi, Urio nakumbuka alikuwa Luteni, Londo, Agnes, Afande machibya aliyewahi kuwa Mkuu wa Mikoa kadhaa etc. Nakumbuka sana kuchoma nyama porini hasa tukiwa zamu ya kupika, pili kula mayai mabichi hasa ukipangwa kwenda kufanya kazi kwenye mabanda, tatu siku Bendi ya muziki inapotumbuiza siku hiyo kwenye kambi la Ruvu. Mwisho hakuna ya Mwanamke au Mwanaume wote siku ya kwanza mnatupiwa bukta/pitishot ya kuvaa na ndiyo sare ya kila siku. Kweli ilipendeza na pale mara chache kuugua sababu ya mikiki mikiki ya pale.
Nilikuepo Ruvu Op flani hv kuna huyo afande anaitwa Kahonda So poa yaani akiwakuta shambani hata kama ni wawili kazi aliyoipanga lazima iishe,
Mpaka ikafika muda mkiona gari lake kwa mbali mnapita migazini hao kurudi kambini.Mwingine ni afande Mariwa mtu poa sana yaani ila hatakagi ujinga kwenye kazi,ukipiga kazi kwa kujituma unakula zako tano mapemaa
LONG LIVE 833 KJ💪
 
Najiulizaga ngurutu wenzangu walipata wapi nguvu za kupigana mitiii??? Yani zile six weeks zilinichosha mashine haikusimama miezi mitatuuu

Sent using Jamii Forums mobile app
six week mi mwenyewe mtambo ulikuwa kimya,ila baada ya hapo sifa wepesi,kuna kaserengeti kamoja kakaleta urafiki urafiki,sikukalazia damu asee
 
Wazalendo;

Moja ya sehemu ya maisha yangu ambayo kamwe sitasahu ni kupitia JKT.

Nilijiunga na JKT Ruvu na baadaye nikaenda Service Buhemba Lwamkoma.

Sitosahau kamwe mafunzo ya ukakamavu, kwata, mchaka mchaka, disko na vitimbi mbalimbali kati ya Makuruta na Maafande. Nilikuwa Combania E.

Moja ya vituko vya kukumbuka ni simulizi kutoka- Operation OKOA, kulikuwa na huyu jamaa alikuwa ni mweusi sana anaitwa afande Lucas, badala ya kuwaaamsha kuruta kwa filimbi, alikuwa anaingia na kuvuta Sigara. Kuruta inatakiwa ukisikia harufu ya Sigara uamke na kufoleni nje. Usipotoka in time unakula mijeledi.

Basi siku moja Kuruta wakapanga wamfanyizie na wakatoka mapema nje na kujificha huku ndani kwenye Bweni wakiyaviringisha mablanketi mithili ya mtu amelala. Afande alipomaliza sigara hakuna aliyetoka akajua siku hiyo kuruta wamegoma kuamka na kuanza kuchapa viboko yale mablanketi yaliyovingirishwa. Alishtukia kaanza kushambuliwa yeye na kuruta toka nje ambao walikuwa na fimbo kibao mpaka akakoma.

Kisha kuruta wakafoleni nje. Nakumbuka Mkuu wa Kombania alipata habari na kulikuwa na drill si kawaida na mpaka push ups za kunusa mkojo katika nyasi walizokuwa wanakojoa kuruta usiku. Hata hivyo yule afande naye alikoma kwani hakurudia mchezo wa kuwaamsha watu kwa sigara.

Kwa waliokuwa Ruvu Operation Okoa:

Na miss

  • Ugali na korosho mnapojongo kambini
  • Mihogo ya Vibwende kwa Babu
  • Wali na Maembe
  • Uji wa Mestin ya Jeshi
  • Bukta na Green Vest
  • Kuokota kuni
  • Bustani
  • Michezo
  • Disco
... Ama Johnnnnn ambaaaa ambaaa John, amba Johnnn wa Tanzania. Arusha Mbali, Arusha Mbali, tukumbukane kwa Barua nk...

Nakumbuka pia siku moja sikuimbisha disco vizuri na kipindi kile 1985 bado kulikuwa kuna ubaguzi wa rangi Africa Kusini, basi afande akanipiga mkwala na kuniambia.

"Kuruta nitakutemea mate yenye sumu usoni upofuke macho, na sijui utatibiwa wapi kwani mipaka yote Afrika Kusini imefungwa. . . (Kana kwamba hakukuwa na hospitali ya kutibu mate ya sumu hapa bongo"

Jamani mliokosa JKT, mlikosa mengi, japo tulipata tabu lakini tulijifunza mengi katika maisha.


Je, wewe unakumbuka nini?
832 KJ bhana duh ni atar...............doso la kufa mtu,bustani kwa sana, afande Best na mabio yake ya mchana yalikera sana, ila nilikuwa napenda kuwah sana kule officers mess ili nkachukue kijogooo....hizi lugha ni walopta huko tu ndo wanaelewa.
 
yaan ndgu umenikumbusha mengi sana,nilianzia mafinga jkt op miaka 20 ya azimio la arusha(june 1987-june 1988) baada ya kumaliza form VI pale milambo sec tabora,nilipangiwa jkt mafinga nlikuwa na school mate wangu anthony thomas(tony lover) ,gosbert john(mwamba) wote hawa nilikuwa nao O-LEVEL Azania sasa hivi wote ni marehemu.

Nnakumbuka jinsi nilivyojifanya mimi ni usalama wa taifa na maafande kuniogopa kwa kunipa kazi ndogondgo,nawakumbuka afande lubega,masoli hawa co watu ni wanyama kabisa.

Service YANGU nilikuwa buhemba,kule kdgo ilikuwa safi lakini kuna afande mausha alinikera sana kwani mwanamke(service woman) aliyemtaki yeye alikuwa gf wamgu kwahiyo tulikuwa hatuivii kabisa.
Duh wakuu, nyie ni wahenga kabsa........ nimechangia mambo current sana, nisubiri kama after 40 yrs hivi ndo nianzshe huu uzi pia.
 
832 KJ bhana duh ni atar...............doso la kufa mtu,bustani kwa sana, afande Best na mabio yake ya mchana yalikera sana, ila nilikuwa napenda kuwah sana kule officers mess ili nkachukue kijogooo....hizi lugha ni walopta huko tu ndo wanaelewa.
Basi kwenye mabio ndo wengine tulipatia videmu hapo😁😁,afande best anatwambia anataka ndoo ila hajui utazitoa wapi,mpaka tukawapiga tukio d-coy kuja kufoleni kila mtu ana ndoo mbili🤣🤣🤣
 
Daah mm nilipigana na afande, nanika mpiga vibaya mno


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Back
Top Bottom