Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Jkt kanembwa 824 kj Afande CO bwegoge,
Chief instructor alikua Captain sebastian Tesha saivi ni major.
Kulikua na Luteni Mwakyobwe akahamishiwa mtabila afande mpenda kuruti ni major sasa uyu jamaa.
Private Marwa asee pt instructor
Marehemu magesa mboje mzee wa doso jamaa alikua anajipiga doso mweyewe anaruka uchura kilometer nne kutoka nduta hadi maini gate.[emoji23][emoji23][emoji23]
Huyu Mwakyobwe ni jamaa yangu sana.

Hapendi mtu aonewe
 
Nilikua chalii wa C coy alafu nilikua doja laana
Siku moja nilidoji nikakimbizwa na fande alafu kama jini vile nikapotelea chooni, yani namaanisha niliingia chooni alaf sijatoka afande nae akaingia kanitafuta bila kuniona

Jiulize nilijificha wapi? Nikiingia kwenye pipa la maji ya chooni alaf pipa lenyewe limejaaa maji full nilikua naibuka kidogo juu navuta hewa sekunde mbili alaf narud nazama ndani ya pipa dakika 4

Madoja wenzangu huko nje walipigwa tifu laana walikwepa ndege masaa 8
😂😂😂😂 Nimecheka balaa, ukageuka samaki bhana dah et unaibuka kidogo kuvuta pumzi afu unazama tena dah 😂😂😂🤣🤣🤣
 
OP Kikwete MGAMBO Jk 832 daah dada wili si akamchoma private kuwa anamtaka alafu alikuwa mtoto wa Mkubwa balaa yani yule Private alipiga magoti mbele ya Kurutu 2000 anamuomba yule binti msamaha alafu demu mwenyewe Mbovuu kinomaa Maafande walitukana balaa yani achaa tuu.....[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787] Jamani baada ya lile tukio Tulikulaaa kazi yanii mateso yale hapanaa ikawa kama Course ya Kadet mamaee week 6 zilikuwa Chungu mnoo kuna siku tulilazwa kwenye Mvua inanyeshaa dadekii kesho yake nikasema wakirudia tena natorokaa yanii napiga mguu kwa mguu mpaka niipate lami...[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Ilaa baadae nikaja kuwa doja balaa wakagawa vitengo picha linaanza nikakimbilia Upishiii...baadae nikawa nadoji msituni tu sieleweki nipo wapi then nikajiunga Ngoma Coy kwa wazalendo nilikuwa nalala kuanzia asubuhi mpaka jionii naamka kulaa tuu. Nilirudi jeshi shavu hilooo mpaka nikatamani kubaki yani wakanipa na 150k ya nauli enzi hizo za JK mambo safii.

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
Hahahahaha Wapi hiyo mwanangu!
 
Kenge wa Pakistan [emoji23][emoji23]daah umenikumbusha 822kj!!!
[emoji3][emoji3][emoji3] daàh nimemkumbuka kenge wa Pakistan 822kj doso lake ni kumbukumbu niliyobaki nayo,mkuu ulikua combania gani????
 
Yule sajenti alikuwa anatufundisha somo la darasani alikuwa anaitwa nani vile, namkubali sana yule mwamba
Itakuwa walikuja wengine, sisi tulipita mwanzo upande wa JKT baada ya hapo kuwa kituo Cha ulinzi(DET).

Tulikuwa tukijificha porini kwenye magofu ya makanisa ya warundi na hakuna hata mtu anayekuja kututafuta, kule ilikuwa ukiwa mzembe utafanya kazi mpaka ukome.

Ilikuwa una risk kujificha wiki ila ukikamatwa siku moja unakuwa tayari kwa drill nzito.
 
Itakuwa walikuja wengine, sisi tulipita mwanzo upande wa JKT baada ya hapo kuwa kituo Cha ulinzi(DET).

Tulikuwa tukijificha porini kwenye magofu ya makanisa ya warundi na hakuna hata mtu anayekuja kututafuta, kule ilikuwa ukiwa mzembe utafanya kazi mpaka ukome.

Ilikuwa una risk kujificha wiki ila ukikamatwa siku moja unakuwa tayari kwa drill nzito.
Kama ni 2015 utakuwa unamjua sema jina tu
 
[emoji3][emoji3][emoji3] daàh nimemkumbuka kenge wa Pakistan 822kj doso lake ni kumbukumbu niliyobaki nayo,mkuu ulikua combania gani????

A coy ya SM Bangu ..sema nilipita pale mujibu[emoji23][emoji23][emoji23]vip unamkumbuka Jeneza??!
 
Nina visa kadhaa pale mgambo jkt.
Kuna afande mmoja alikuwa anaitwa mjerumani huyo, kuna siku aliwalisha watu malimao na maganda yake huku akisema "kurutu" nataka nione mbegu tu hapo chini.
Sababu ikiwa ni ile ya kula machungwa yale yaliyopo barabara ya kuelekea kwenye mahanga ya madawili sitasahau ile moment.
Sisi wakati tunapita hapo mgambo machungwa yalikuwa mengi sana yaani tulikuwa tunayala kila siku na hayaishi kabisa

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
DANGER COY nipo hapa we ulikuwa kujitolea ?
Muujibu,

Nilikuwa C COY, hapo danger namkumbuka yule afande mzee wa mikwara alikuwa akipita kwetu anatuambia lazima au kurutu wa5, pia hapo danger namkumbuka volunteer mmoja alikuwa anaitwa BENZEMA mzeee wa bebebeeeeeeee mnaitikia Benzemaaaaa

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom