Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Je, unakumbuka nini enzi zako za JKT? Ni mambo gani yalikufurahisha au kukukwaza?

Muujibu,

Nilikuwa C COY, hapo danger namkumbuka yule afande mzee wa mikwara alikuwa akipita kwetu anatuambia lazima au kurutu wa5, pia hapo danger namkumbuka volunteer mmoja alikuwa anaitwa BENZEMA mzeee wa bebebeeeeeeee mnaitikia Benzemaaaaa

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
Yule afande NYUNDO mzee wa vitisho nasikia alifukuzwa jeshi
 
rikiboy wee lazima nitakuwa nakujua maana nilidoj Sana porini kule kwenye kisima na Hadi kule bwawani nilidoji, nilidoji Sana asubuhi kule nyuma ya D coy kuwasha Moto , asubuhi naamkia pale, nikadoji Kwemye Ngoma kwa afande Mbuge, tukawa tunaombia kule mesi.Kna demu alikuwa wa C coy anasauti nyororo alikuwa anatuimbisha,jina alikuwa Anita au happy .

Noma Sana .Yule demu aliyemfanya private apige goti kule uwanja wa damu mbovu Sana , libonge ila baba yake Maj general, hapo ndo mziki ulipoanzia.... Na yule anasimulia sisi pushapu unamkumbuka?
 
Mkwayu alikuwa jamaa mrefu anapenda sana kwata. RSM kayange alikuwa anapenda kusema ukiharisha jua umekula m*vi mabichii.
Nilikuwa D-coy luteni walikuwa masalu na mbuga hao ndo nawakumbuka. Kwenye kwata alikwepo pia mzee matonya kwenye "guzmachi" alikuwa na kawimbo kake.
Mabichi [emoji16][emoji16]
Alikuwa anapenda chenja ile ya Helena dada helena
 
Jibaba Bonge,
Bigula la moto kule Sao Hill ndugu yangu... yani we acha tu!
Basi Mlai alikuwe mshenzi kweli...tulikuwa tumezima moto siku 2..wakati tunaendelea mabasi ya abiria toka Songea na Mbeya yakasimamishwa..abiria wakapata kibano kuzima moto..yaani kuokoa raslimali za Taifa! walilalamika lakini wapi!

Nilijifunza, uvumilivu na uzalendo na nyimbo za kupenda Tz kuliko wakati wowote ktk maisha yangu!

Wale waliokuwa Danger Coy..1990 je mnamkumbuka Singano na Afande Sagaya?

Sagaya:-Afande Sumu ya Mamba!
 
Bulombora 821 KJ
OP UCHUMI WA KATI

Mkuu wa kikosi Major general Victatus
OC BM Alphonce

Eagle coy (E Coy)

My favorite soldiers
-Private Mweta (huyu afande alikuwa mtata [emoji119][emoji119])
-Private Khamis
-Private Mwamvua
-Private Tarimo (michezo ya nyani fisi haiwezi [emoji16][emoji16])
-Koplo Kadulege (hapa ni mahali pa takatifu hairuhusiwi kupiga kelele)
-Koplo Ambari ( uwanja wa damu, kwata)
-Sir Major Mushi
 
Kanembwa pale kwa mzee mbiji,, Afande kibutu,,Teddi mtu m-bad kabsa serengeti wanachura sema mda wa kusimamisha jogoo ndo aupo[emoji34]
 
Kwani wote walikwenda JKT na kwanini JKT na siyo shule au mambo mengine ya maana?
 
Afande bafeni D COY pale RUVU JKT 2014
Nilikuwa nabust sana kwenye misos, niliwahi kusepa na misos kwenye beseni nkaenda kulia angani halafu nkashindwa kutembea.
Nilikuwa dogger hatari.
Kuigiza mgonjwa wa kudumu.
Kucheza hasa kigodoro.
Madoso Yale hatarihatari.
Chenja.
Jkt raha.


Sent using Jamii Forums mobile app
Majirani zetu nyie, sisi tulikua Eagle coy
 
rikiboy wee lazima nitakuwa nakujua maana nilidoj Sana porini kule kwenye kisima na Hadi kule bwawani nilidoji, nilidoji Sana asubuhi kule nyuma ya D coy kuwasha Moto , asubuhi naamkia pale, nikadoji Kwemye Ngoma kwa afande Mbuge, tukawa tunaombia kule mesi.Kna demu alikuwa wa C coy anasauti nyororo alikuwa anatuimbisha,jina alikuwa Anita au happy .

Noma Sana .Yule demu aliyemfanya private apige goti kule uwanja wa damu mbovu Sana , libonge ila baba yake Maj general, hapo ndo mziki ulipoanzia.... Na yule anasimulia sisi pushapu unamkumbuka?
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Kule kisimani noma sana mzee... pale danger tumewasha moto kinoama kipindi kile unaona kombania yako inakula kazii wewe umetulia tu dadekii... tulibeba kigodoro tukapeleka kule juu kwenye mashamba ambayo kuna Vifutu kule tukawa tunatumia na kasimu flani kuchat... yule manzi alituponza sana

Sent from my SM-G611K using JamiiForums mobile app
 
Wazalendo;

Moja ya sehemu ya maisha yangu ambayo kamwe sitasahu ni kupitia JKT.

Nilijiunga na JKT Ruvu na baadaye nikaenda Service Buhemba Lwamkoma.

Sitosahau kamwe mafunzo ya ukakamavu, kwata, mchaka mchaka, disko na vitimbi mbalimbali kati ya Makuruta na Maafande. Nilikuwa Combania E.

Moja ya vituko vya kukumbuka ni simulizi kutoka- Operation OKOA, kulikuwa na huyu jamaa alikuwa ni mweusi sana anaitwa afande Lucas, badala ya kuwaaamsha kuruta kwa filimbi, alikuwa anaingia na kuvuta Sigara. Kuruta inatakiwa ukisikia harufu ya Sigara uamke na kufoleni nje. Usipotoka in time unakula mijeledi.

Basi siku moja Kuruta wakapanga wamfanyizie na wakatoka mapema nje na kujificha huku ndani kwenye Bweni wakiyaviringisha mablanketi mithili ya mtu amelala. Afande alipomaliza sigara hakuna aliyetoka akajua siku hiyo kuruta wamegoma kuamka na kuanza kuchapa viboko yale mablanketi yaliyovingirishwa. Alishtukia kaanza kushambuliwa yeye na kuruta toka nje ambao walikuwa na fimbo kibao mpaka akakoma.

Kisha kuruta wakafoleni nje. Nakumbuka Mkuu wa Kombania alipata habari na kulikuwa na drill si kawaida na mpaka push ups za kunusa mkojo katika nyasi walizokuwa wanakojoa kuruta usiku. Hata hivyo yule afande naye alikoma kwani hakurudia mchezo wa kuwaamsha watu kwa sigara.

Kwa waliokuwa Ruvu Operation Okoa:

Na miss

  • Ugali na korosho mnapojongo kambini
  • Mihogo ya Vibwende kwa Babu
  • Wali na Maembe
  • Uji wa Mestin ya Jeshi
  • Bukta na Green Vest
  • Kuokota kuni
  • Bustani
  • Michezo
  • Disco
... Ama Johnnnnn ambaaaa ambaaa John, amba Johnnn wa Tanzania. Arusha Mbali, Arusha Mbali, tukumbukane kwa Barua nk...

Nakumbuka pia siku moja sikuimbisha disco vizuri na kipindi kile 1985 bado kulikuwa kuna ubaguzi wa rangi Africa Kusini, basi afande akanipiga mkwala na kuniambia.

"Kuruta nitakutemea mate yenye sumu usoni upofuke macho, na sijui utatibiwa wapi kwani mipaka yote Afrika Kusini imefungwa. . . (Kana kwamba hakukuwa na hospitali ya kutibu mate ya sumu hapa bongo"

Jamani mliokosa JKT, mlikosa mengi, japo tulipata tabu lakini tulijifunza mengi katika maisha.


Je, wewe unakumbuka nini?
Mambo ya jandoni kuyaweka kijiweni ni noumaa aisee
 
Back
Top Bottom