Nimekumbuka msange Tabora OP Kikwete 2015, E coy chini ya OC Jomo, na Sir major Mudo, kuna siku tulikuwa tunapanga tanuru ile tunamaliza akapita luteni mmoja hivi jina limenitoka akatwambia hilo eneo tulilo panga Tanuri hapatakiwi kuchomea hapo tofari kwahiyo
tuhamishe tofari na tupange upya, alafu hapo jua limewaka balaa niliishiwa nguvu nakujilaani, ila nilivyozoea mazingira nikaanza kudoji, maisha ya Msange vyoo hakuna tunajisaidia kwenye shamba la mahindi, nilivyoona shida zinazidi nikajiunga ngoma COY huko nikuimba tu na kukata mauno na wagonjwa wa kudumu nimemic sana Mesi kwa afande Mafleta, maisha ya JKT yalinijenga naweza kuishi sehemu yoyote iwe mjini au kijijini