Prisoner 46664
JF-Expert Member
- Dec 18, 2010
- 1,948
- 1,238
Wakubwa,
Jana nilikuwa nasikiliza RFA kulikuwa na kipindi cha Afya, kuna jamaa wa dizaini kama ya Dr Ndodi, wanapima magonjwa kwa kutumia mashine inayoitwa Quantum ambayo ina uwezo wa kuainisha magonjwa mengi yanayomsumbua mtu, kwa kushika handle fulani kama 'mouse' inayoingia kwenye computer hiyo. Baada ya hapo wanauza dawa za aina ya vyakula ili kutibu magonjwa yaliyoonekana kwa mgonjwa.
Kilichonishitua ni kwamba walifika mahala wakawa wanataja vitu vinavyopelekea mtu kuwa na Uric acid nyingi mwilini, wakasema kuwa ulaji wa matunda mchanganyiko KWA MUDA MMOJA ni source kubwa na mbaya sana ya Uric acid!
Walisema wale wauzaji wa matunda wanaokata chungwa, embe, papai, pesheni, avocado, tango, ndizi etc, na kukuzia kwenye sahani waogope kama ukoma, maana wanakuletea sahani ya kifo.
Walieleza kuwa kinachotakiwa ni kula tunda la aina moja lililopo kwenye msimu, basi na si kula matunda mchanganyiko.
Najiuliza, kuna packed juice za mixed fruit, aidha huko majumbani tunablend na kunywa juice za kuchanganya matunda, je ndio tunajimaliza?
Mimi nadhani huyu jamaa alizidisha mbwembwe akadanganya,
Yeye ni tabibu wa kwanza namsikia akisema kitu kama hicho toka nianze kujua kuhusu magonjwa...kama wiki mbili hivi zilizopita nilimpeleka mtu wangu wa karibu kwenye clinic kama hiyo iliyoko pale mitaa ya mbezi samaki (hii clinic ina historia nzuri sana ya kutibu magonjwa cronic kama ya viungo ambayo yameshindikana hospitali..)..doctor alizungumza vitu logical tu vya kubadilisha kwenye maisha yake lakini hakukuwa na kimoja cha ajabu kama hiki...
Kuna daktari anaitwa Sunjay Gupta wa CNN, siku moja alisema wazi kuwa ulaji wa matunda walau aina 5 kwa wakati mmoja, ukijumlisha na mazoezi ya kila siku huchangia kwa kiasi kikubwa sana kupunguza uwezekano wa kupata kansa kwa waafrika (the riskiest ethnic group in the world in terms of cancer infection,,,)...mimi nikiwa mmoja wa watu wanaotumia hii style ya maisha sijaona kitu chochote kibaya hata sasa na sikumbuki mara ya mwisho nilipokwenda hospitali au kunywa dawa....
Rai yangu ni kuwa madaktari wa sanitarium clinics wanatofautiana upeo na ujuzi,,,mawazo yao changanya na ya kwako halafu ufanyie kazi