Je, unamfahamu mnyama anayeitwa Nyegere/Honey Badger? Mnyama mwenye wivu kupindukia

barafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2013
Posts
6,739
Reaction score
32,880

PICHA: Mnyama Nyegere


PICHA: Mtu aliyedhuriwa na mnyama Nyegere

PICHA: Nyegere akipambana na Simba

Nyegere ni moja kati ya wanyama wenye wivu sana hapa duniani. Chakula chake kikubwa ni asali,yeye hupanda juu ya mzinga wa asali na kuujambia, baada ya mashuzi yake nyuki wote hulewa na yeye kupakua asali na masega yake na kula. Mwili wake una ngozi ngumu sana kiasi hata nyuki akimuuma hakuna chochote kinatokea

Nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike

Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere,anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke,mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake(ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii.

Nyegere ndio mmoja kati ya "fearless animal" duniani, huweza kuwakabili Simba na Chui zaidi ya mmoja na kuwashinda,anasaidiwa na ngozi yake ngumu na kucha zake, awapo katika hatari ya kushambuliwa hukakamaa na ngozi yake kuwa ngumu kama "defensive mechanism" yake.

Kuna makabila ambayo waganga wa kienyeji hutumia mchanganyiko wa Nyegere kutengenezea limbwata,Yaani wamama huchukua dawa hiyo kuwawekea waume zao ili wawe na "upendo" wa Nyegere.

Wivu wa Nyegere hufanya awachukie sana binadamu wanaume,mwanaume ukiwa porini ukakutana na Nyegere akiwa na jike lake jiandae kupata kibano, huona wivu kuwa utamtamani jike,hivyo hukimbilia kumvamia mwanaume sehemu za siri akiamini ndizo zinazokupa jeuri ya kumtamani jike lake.

Nyegere hula nyoka wa aina yoyote,ana sumu kali ambayo akimng'ata nyoka wa aina yoyote haponi.

Ogopa sana kukutana na mnyama mwenye wivu Nyegere...

Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyelina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja, akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimya kimya.

ZAIDI TAZAMA HAPA
===

MICHANGO YA WADAU KUHUSU MNYAMA HUYU

---
Nimeenda Google, nimesoma sentensi hii, du! nimemuogopa huyu mnyama mdogo. The only sure way of killing them quickly is through a blow to the skull with a club or a shot to the head with a gun, as their skin is almost impervious to arrows and spears.
---
Fuata hiyo link kuju ukweli wa mnyama huyo bila chumvi.
---
---
---
 






1.Ni mnyama mdogo anayekula nyoka, kenge, majani, matunda, kenge, mizoga ya binadamu, chui, simba, duma, ndege n.k...kwa kifupi anakula kila kitu

2.ngozi yake ni ngumu sana kiasi kwamba mishale na mikuki au risasi ni ngumu kupenya..ukitaka kumuua ni kumpiga katika fuvu la kichwa chake na kitu kizito au risasi kichwani,

3.katika guines world book of records yeye ndio the most fearless creature on the planet

4.mwili wake haudhuriki na sumu ya nyoka wa kawaida na ikitokea ameumwa na nyoka mwenye sumu kali na sumu ikapenya kwenye damu yake itamfanya alale kwa masaa kadhaa tu kisha ataendelea na mambo yake

5.Ana meno makali/magumu sana yenye uwezo wa kupasua hata jumba la kobe

6.Ashawahi kukutwa akipigana na simba na hata tembo na vifaru katika nyakati tofauti

7.Anapenda kula asali, huwa anaupulizia hewa chafu mzinga na nyuki wote kulewa hivyo kula asali na kuondoka zake

8.Ni vigimu kumshambulia kwani ngozi yake inamfanya iwe rahisi kwake kujikaza na kujizungusha katika upande wowote anaotaka na kukujeruhi.

9.Ni mvivu katika maswala ya nyumba yake hivyo basi anapojisikia uvivu hujilaza sehemu yoyote inayomfaa..ishaonekana akiwa kajiliza katika pango la mbwa mwitu kama kwake.

Mengine angalia link ya youtube nimekuwekea chini[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]

 
Nimeenda Google, nimesoma sentensi hii, du! nimemuogopa huyu mnyama mdogo. The only sure way of killing them quickly is through a blow to the skull with a club or a shot to the head with a gun, as their skin is almost impervious to arrows and spears.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…