Je, unamfahamu mnyama anayeitwa Nyegere/Honey Badger? Mnyama mwenye wivu kupindukia

Ni mdudu pia ambaye hapendi kukanyaga umande
 
Zamani umewahi kukutana na kibwana mdogo flani uwezo wa kukipiga unacho ila unaogopa timbwili lake?

Vipo vi bwana mdogo flani yaani unaweza piga halafu wewe ukachoka.kanakufuata tu kanakupiga na mawe,gogo,mchanga na kila kitu....yaani inabidi wewe ukimbie sasa.. basi ndo Nyegere.

Yaani Nyegere usije ukapumbazwa na jina lao maana hapo utawaza Nyege... Achana na hbr hizo. Hivi vinyama ni vibishi....acha. huwa vina mapepo flani hivi...ukikitibua hakikuangalii usoni. Ndo wale watu wanakwambia "nguse kama sijakuchana chana na viwembe"

Wanyama wana vifahamu hivi viumbe....we imajini vinakunywa sumu ya nyoka ndo kilevi chao...eeeehhh....usibishe.hata nyoka akikagonga...kanaanguka kama kamekufa ...halafu ghafla kanainuka kuliendeleza chezo.kakimuua kanamnyonya mate....kanalewa.kanaalala kakikoroma.

Sasa jichanganye kukaamsha... Utajuta.Ukikosana na Nyegere atakufuata popote uendapo.... Yaani kama utapanda gari ukamwacha atakuja tu akifuata barabara na kuulizia njian... Washkaji mliona gari flani imepita hapa.... Mpaka katafika kwako.

Yaani Nyegere anaweza kukuma mguu halafu asiuachie. Ukapiga mpaka wewe ukakaribia kufa kwa kuchoka. Unaweza ukakachoma choma na kisu kakang'ang'ania tu mguu huku kanavuja damu kinoma.yaani ni vibishi.

Ukikuta kimemgomea simba kupisha njia ndo utacheka.kanagoma kabisa na wala hakakwepeshi macho...sasa simba huwa wanaelewa kuwa hiki kibwana mdogo ikatokea tu kimeshika sehemu ndo basi.hakiachii. mwishowe simba huwa anasema ....dogo we jifanye kukomaa kuna siku ntakiwasha hapa tuonane wabaya" basi utasikia "usintishe wala nini...hayo manyama tu hata kwenye sambusa yapo" simba hapo anajifanya hajasikia anaondoka.

Sasa shida kubwa ya hivi vimnyama. Wewe huwa unasema xxxxx ana wivu sana....siwezi ishi naye nmechoka.huyo hana wivu. Nyegere ana wivu bwana. Ana wivu balaaa. Hafai.

Akiwa anatembea na mkewe yeye anakuwa nyuma analinda uchi wa mkewe. Ikatokea hata jani likagusa tu. ..asalaleeee....balaa lake.katalichana chana jani kinyama na kulifakilia mbali.kakiamini jani limefaidi utamu wake. Yaani kana wivu haka kamnyama acha. Hapo mkewe atasema 'baba ukwaju...yaani jani kugusa tu inakuwa issue..?twende bwana" kanajibu huku kametuna kanahema.

" Na wewe usinchanganye saahizi ntakuchenjia..." Hapo wife anajua itakuwa issue basi ili wafike salama anakikisha sehemu zake za siri haziguswi na jani lolote njiani.

Hawa wanyama wanapenda asali kinyama.... Unajua vinakula wanyama na wadudu wa ajabu halafu vinashushia na juice ya sumu ya nyoka. Sasa usiombe vikajamba ..unaweza kukufa hapo hapo kama afya yako haina amani...yaani ina mgogoro.

Basi huwa vinaenda ilipo asali...vinatoa gesi kwa nyuma (ashakum si matusi, vinajamba) hapo nyuki ule ukali wao huwa si kitu.. wanalewa wanalala. Kanaenda kuchukua asali.kanakula mpaka kabavimbiwa.

Na wakati mwingine vinaweza kutoa harufu flani kali sana ya kukwaza matakoni kukera tu wapita njia...ni tukorofi sana hutu tumnyama. Yaani bora uende ukawachokoze fisi walioketi wanapiga stories kuliko kuanzisha beef na haka kamnyama.

Huwa hakasamehi. Unaweza ukatibuana nako leo ila baada ya miaka miwli ukikutana nako hakakuulizi kuwa why siku ile ulinifanyia hivi?kanalianzisha upyaaaa.

Wanyama wengi hupenda kutengeneza amani nako sababu wanajua.kabishi kinyama.katukutu,kakorofi na hakaambiliki.

Huyo ndo Nyegere. Kaa mbali naye ukienda porini...anaweza kukufuata hadi kwako.na kama upo ndani kanakusubiria mlangoni....ni kama kanakuwa kanakudai hivi ....
 
Duh asante kwa kutushurikisha

Kanaitwaje jina lake kizungu nukatafute makala yake YouTube
 
Habari za nyegere kunyonya sumu ya nyoka ni yakutunga,ukweli ni kwamba nyegere huwa anakula nyoka,na sio kweli kwamba kinywaji chake ni sumu ya nyoka hapa unapotosha,ukweli ni kwamba huyu mnyama huwa akigongwa na nyoka analewa kwa muda mchache na baada ya hapo huwa amnakaa sawa na anaendelea kuhangaika nae mpaka anamuua na kumfanya Chakula.
Jitahidi kumsoma vizuri mpaka umfahamu ndipo ushushe uzi JF vinginevyo utapotosha kundi kubwa sana humu.
Kifupi nyegere anahangaika na nyoka kama kitoweo na sio kunyonya sumu ya nyoka.
 
Sema umeiwasilisha vizuri sana, inahamasisha kuendelea kusomwa.
Kweli jamaa kaiwasilisha mada hii kuhusu nyegere kisanii. Yaani kaongeza manjonjo, madoido na mbwembwe ili kumvuta msomaji aweze kutiririka naye vizuri

Hapo anaposema nyegere anaongea na simba au binadamu ni mtindo tu wa kuhadithia facts kumuhusu huyo mnyama ili story isichoshe
 
Hata mimi nimelazimika kuimaliza dadadeek
 
Mkuu huyo mzee hiyo mikono kalimjambia? Hako kajamaa basi ni noma...kesho ntaenda kufanya presentation ofisini kuhusu haka kamnyama...bosi aki-mind kivyake
Tupo mrejesho wa prezenteshen ofisin kwako bosi aliipokea vp
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…