Je, unamfahamu mnyama anayeitwa Nyegere/Honey Badger? Mnyama mwenye wivu kupindukia

Je, unamfahamu mnyama anayeitwa Nyegere/Honey Badger? Mnyama mwenye wivu kupindukia

HUYU NDIE KIUMBE HATARI ZAIDI DUNIANI


Huyu ndie. Mbabe wa Nyika na Chaka lakini Asiyevuma. Huenda ukiambiwa utaje wanyama hatari zaidi duniani utaanza na simba ama chui kwa haraka lakini ukweli ni kuwa Nyegere ama Honey badger ni miongoni mwa wanyama hatari zaidi duniani, kwa tarifa zenye uhakika ni kuwa hata nyoka, chui na simba hufyata kwa Nyegere.

1. Nyegere ndio mmoja kati ya wanyama wasioogopa kitu chochote duniani, huweza kuwakabili Simba na Chui zaidi ya mmoja na kuwashinda. Vile vile hategemei wenzake (uwingi wao) kwakua Njegere ni mmoja wa wanyama wanaotembea kivyake wakati wote isipokuwa wakati wa kupandana tu.

2. Nyegere ana gozi gumu zaidi kuliko wanyama wote wa mwituni kiasi ambacho ni ngumu sana kumuua kwa mshale au hata panga, Vile vile gozi la mnyama huyu linafanya sindano nyembamba ya nyuki kudunda... katika mapambano .anasaidiwa na kucha zake, ndefu na ngumu, kama haitoshi awapo katika hatari ya kushambuliwa ngozi yake huwa ngumu na kukakamaa zaidi ("defensive mechanism).

3. Nyegere hula vyote iwe nyama iwe majani na hii imemfanya kustahili shuruba za mazingira yote iwe nyikani ama mwituni. Chakula chake kikubwa ni asali.

4. Nyegere hula nyoka wa aina yoyote kwakua pia ana sumu kali ambayo akimng'ata nyoka wa aina yoyote haponi ingawa wapo nyoka wenye sumu ambao Nyegere akiwala anaweza kuzimia kwa masaa kadhaa kutokana na ukali wa sumu ambayo inakuua wewe kwa dakika tu.

5. Utafiti unathibitisha kuwa mnyama huyu ana meno na taya ngumu na kali sana kiasi cha kuvunja na kutafuna gamba la kobe kiurahisi.

6. Nyegere ni mnyama mwenye wivu sanaa nyegere hutembea nyuma ya jike yan hata jani likigusa jike lake basi vita yake na jani itakua ni kubwa saaanaaa

7. Hivi unajua kama nyegere ni mlevi [emoji3][emoji3][emoji3] hutumia sumu za nyoka na wanyama wenye dumu kali kama kilevi oindi anapowaua analala kwa mda ataamka kuendelea na shughuli zake.

8. Nyegere hua natabia ya kula sana asali yani anapeenda asali kupitiliza na hujambia mzinga nyuki hulewa then yy heendelea na shuhuli yake.

9. OLe wako uchukue asalinya nyegere atafuatilia harudi mpka ulipoishia na hua anakuja usiku anaweza kufanya vurugu kubwa sana kama kulipiza kisasi hata ikiwa Dar-Moro [emoji3][emoji3][emoji3]

10. Kutokana na kufanana kwao kwa kimwili, nyegere wana tezi hatari chini ya mkia wake wenye maji yenye harufu kali.. Kwa ujumla, hutumiwa tu kuashiria umiliki wa eneo.

11. Kwakutumia kucha zao ndefu nyegere huchimba sana na anaweza akachimba umbali zaidi kwenda chini na hata kwenye mti wanakucha ngumu sana

12. KWA kawaida nyegere ni mvivuuu sana yan akijisikia kulala anaweza akalala sehemu yoyote ile hajali kama shimo la panya au nyoka au chochote yeye analala[emoji3][emoji3][emoji3]

13. Ni kweli kwamba nyegere yupo kwenye kitabu cha maajabu ya dunia kama "Kiumbe wa Ulimwengu asioogopa chochote, Wao ni wavamizi na wenye utayali wa vita muda wote ya kupigana hata kwa fisi, simba chui wao vita tu.

14. Kama hujui nyegere anakula kitu chochotee kile sio ndege sio majani sio mnyama yeye anakigeuza msosi mpka anaposhiba.

15. Nyegere anangozi ngumu sana yenye kuhimili mishale ulishwahi kuona nungu nungu akituoa miba basi ile miba ni kama zile stick za meno kwa nyegere [emoji3][emoji3][emoji3]

16. Wao wanameno ni yenye nguvu na magumu sanaa meno ya nyegere yanvunja lile gamba la kobe unalojua kama biscut[emoji3]

17. Nyegere ni mnyama msafi sana sio mchafu kama wanyama wengine walao nyama haogopi na msafi muda wote.

Nyegere

Ni mdudu pia ambaye hapendi kukanyaga umande
 
Zamani umewahi kukutana na kibwana mdogo flani uwezo wa kukipiga unacho ila unaogopa timbwili lake?

Vipo vi bwana mdogo flani yaani unaweza piga halafu wewe ukachoka.kanakufuata tu kanakupiga na mawe,gogo,mchanga na kila kitu....yaani inabidi wewe ukimbie sasa.. basi ndo Nyegere.

Yaani Nyegere usije ukapumbazwa na jina lao maana hapo utawaza Nyege... Achana na hbr hizo. Hivi vinyama ni vibishi....acha. huwa vina mapepo flani hivi...ukikitibua hakikuangalii usoni. Ndo wale watu wanakwambia "nguse kama sijakuchana chana na viwembe"

Wanyama wana vifahamu hivi viumbe....we imajini vinakunywa sumu ya nyoka ndo kilevi chao...eeeehhh....usibishe.hata nyoka akikagonga...kanaanguka kama kamekufa ...halafu ghafla kanainuka kuliendeleza chezo.kakimuua kanamnyonya mate....kanalewa.kanaalala kakikoroma.

Sasa jichanganye kukaamsha... Utajuta.Ukikosana na Nyegere atakufuata popote uendapo.... Yaani kama utapanda gari ukamwacha atakuja tu akifuata barabara na kuulizia njian... Washkaji mliona gari flani imepita hapa.... Mpaka katafika kwako.

Yaani Nyegere anaweza kukuma mguu halafu asiuachie. Ukapiga mpaka wewe ukakaribia kufa kwa kuchoka. Unaweza ukakachoma choma na kisu kakang'ang'ania tu mguu huku kanavuja damu kinoma.yaani ni vibishi.

Ukikuta kimemgomea simba kupisha njia ndo utacheka.kanagoma kabisa na wala hakakwepeshi macho...sasa simba huwa wanaelewa kuwa hiki kibwana mdogo ikatokea tu kimeshika sehemu ndo basi.hakiachii. mwishowe simba huwa anasema ....dogo we jifanye kukomaa kuna siku ntakiwasha hapa tuonane wabaya" basi utasikia "usintishe wala nini...hayo manyama tu hata kwenye sambusa yapo" simba hapo anajifanya hajasikia anaondoka.

Sasa shida kubwa ya hivi vimnyama. Wewe huwa unasema xxxxx ana wivu sana....siwezi ishi naye nmechoka.huyo hana wivu. Nyegere ana wivu bwana. Ana wivu balaaa. Hafai.

Akiwa anatembea na mkewe yeye anakuwa nyuma analinda uchi wa mkewe. Ikatokea hata jani likagusa tu. ..asalaleeee....balaa lake.katalichana chana jani kinyama na kulifakilia mbali.kakiamini jani limefaidi utamu wake. Yaani kana wivu haka kamnyama acha. Hapo mkewe atasema 'baba ukwaju...yaani jani kugusa tu inakuwa issue..?twende bwana" kanajibu huku kametuna kanahema.

" Na wewe usinchanganye saahizi ntakuchenjia..." Hapo wife anajua itakuwa issue basi ili wafike salama anakikisha sehemu zake za siri haziguswi na jani lolote njiani.

Hawa wanyama wanapenda asali kinyama.... Unajua vinakula wanyama na wadudu wa ajabu halafu vinashushia na juice ya sumu ya nyoka. Sasa usiombe vikajamba ..unaweza kukufa hapo hapo kama afya yako haina amani...yaani ina mgogoro.

Basi huwa vinaenda ilipo asali...vinatoa gesi kwa nyuma (ashakum si matusi, vinajamba) hapo nyuki ule ukali wao huwa si kitu.. wanalewa wanalala. Kanaenda kuchukua asali.kanakula mpaka kabavimbiwa.

Na wakati mwingine vinaweza kutoa harufu flani kali sana ya kukwaza matakoni kukera tu wapita njia...ni tukorofi sana hutu tumnyama. Yaani bora uende ukawachokoze fisi walioketi wanapiga stories kuliko kuanzisha beef na haka kamnyama.

Huwa hakasamehi. Unaweza ukatibuana nako leo ila baada ya miaka miwli ukikutana nako hakakuulizi kuwa why siku ile ulinifanyia hivi?kanalianzisha upyaaaa.

Wanyama wengi hupenda kutengeneza amani nako sababu wanajua.kabishi kinyama.katukutu,kakorofi na hakaambiliki.

Huyo ndo Nyegere. Kaa mbali naye ukienda porini...anaweza kukufuata hadi kwako.na kama upo ndani kanakusubiria mlangoni....ni kama kanakuwa kanakudai hivi ....
 
1630277851606.png
1630277950493.png
1630278156624.png


1630277833277.png
 
Duh asante kwa kutushurikisha

Kanaitwaje jina lake kizungu nukatafute makala yake YouTube
 
Habari za nyegere kunyonya sumu ya nyoka ni yakutunga,ukweli ni kwamba nyegere huwa anakula nyoka,na sio kweli kwamba kinywaji chake ni sumu ya nyoka hapa unapotosha,ukweli ni kwamba huyu mnyama huwa akigongwa na nyoka analewa kwa muda mchache na baada ya hapo huwa amnakaa sawa na anaendelea kuhangaika nae mpaka anamuua na kumfanya Chakula.
Jitahidi kumsoma vizuri mpaka umfahamu ndipo ushushe uzi JF vinginevyo utapotosha kundi kubwa sana humu.
Kifupi nyegere anahangaika na nyoka kama kitoweo na sio kunyonya sumu ya nyoka.
 
Sema umeiwasilisha vizuri sana, inahamasisha kuendelea kusomwa.
Kweli jamaa kaiwasilisha mada hii kuhusu nyegere kisanii. Yaani kaongeza manjonjo, madoido na mbwembwe ili kumvuta msomaji aweze kutiririka naye vizuri

Hapo anaposema nyegere anaongea na simba au binadamu ni mtindo tu wa kuhadithia facts kumuhusu huyo mnyama ili story isichoshe
 
Kweli jamaa kaiwasilisha mada hii kuhusu nyegere kisanii. Yaani kaongeza manjonjo, madoido na mbwembwe ili kumvuta msomaji aweze kutiririka naye vizuri

Hapo anaposema nyegere anaongea na simba au binadamu ni mtindo tu wa kuhadithia facts kumuhusu huyo mnyama ili story isichoshe
Hata mimi nimelazimika kuimaliza dadadeek
 
Mkuu huyo mzee hiyo mikono kalimjambia? Hako kajamaa basi ni noma...kesho ntaenda kufanya presentation ofisini kuhusu haka kamnyama...bosi aki-mind kivyake
Tupo mrejesho wa prezenteshen ofisin kwako bosi aliipokea vp
 
Back
Top Bottom