Wacha uwongo, nyegere hajambii mzinga wa nyuki hata siku moja. Ni kweli kuwa yeye anakula asali na ndiyo maana anaitwa "Honey Badger," ila ikumbukwe kuwa asali si chakula pendwa ama pekee alikacho. Nyegere ni Omnivores maana kwamba anakula kila kitu bila ubaguzi, anakula nyoka tena mambas (koboko) na aina yote ya nyoka bila tatizo kwani ana anti venom inayomfanya asife kutokana na kugongwa na nyoka. Anakula pia wanyama wadogowadogo kama paka hata vitoto vya mbwa na aina zote za ndege mwituni. Akikuta asali anaishambulia bila tatizo na nyuki wala hawamsumbui. Kule kunuka kwake anatumi ile harufu kwa ajili ya ku-mark territories tu au akiwa under threat kutoka kwa wanyama wengine wakubwa kama Simba, chui, fisi, Rock python na wengineo. Anawajambia kuwatishia.