Je, unamfahamu mnyama anayeitwa Nyegere/Honey Badger? Mnyama mwenye wivu kupindukia

Je, unamfahamu mnyama anayeitwa Nyegere/Honey Badger? Mnyama mwenye wivu kupindukia

Kwanza kakikuona hutoa saut kama machine ya kukatia miti,sio siri ni kakorofi na wivu uliopitiliza,ninaishi tabora huku ni balaa vipo kakikuona tu kanafoka,vijijin balaa sana tunakwepa koboko,nyegere,fisi,nge na vingine vingi,karibuni kwa utalii wa kuwaona nyegere na koboko na kuselfika nao!#ngw'abheja
 
Nyegere, melesi au mhilu (Mellivora capensis) ni mnyama mdogo wa familia Mustelidae anayetokea Afrika, Mashariki ya Kati na Uhindi.

Nyegere huishi peke yao kwenye shimo analolichimba yeye mwenyewe. Ni wachimbaji wazuri sana. Vile vidole vyao vyenye kucha ndefu na ngumu humsaidia sana kwenye kazi hii. Hata kama ardhi ni ngumu sana, ana uwezo wa kuchimba shimo linalomtosha kujificha katika kipindi kinachokadiriwa kuwa ni dakika kumi tu.

NYEGERE (Honey burger) a.k.a "The fearless animal" TABIA NA MAMBO YAKE MENGINE Nyegere ni mnyama mwenye wivu na mapenzi makubwa sana kwa jike lake, hutembea nyuma ya jike huku akiwa ameziba sehemu za siri za jike, hata jani tu likiigusa sehemu ya siri ya jike litararuliwa na kupokea kichapo cha hatari,maana wivu wake ni kuwa jani laitakuwa "limefaidi utamu" wa jike Nyegere anaweza kununua ugomvi mpaka kijiji cha sita, walina asali ndio waathirika wakubwa wa hasira za Nyegere,anaweza kuujambia mzinga akala kidogo asali na kupeleka kwa mke,mlina asali akifika na kupakua, nyegere ana uwezo ya kufuatilia harufu ya aliyeiba asali yake mpaka nyumbani, na akifika anavunja mlango na kuingia ndani na kumvamia mwizi wa asali yake (ukizingatia milango ya vijijini si imara). Watu wengi vijini wameuwawa kwa namna hii. Huko Singida aliwahi kusafiri zaidi ya kilomita saba usiku kwa usiku anafuata harufu ya mtu aliyelina mzinga wa asali aliyoijambia, alipofika akavunja mlango na kukuta wamelala watu wanne kwenye mkeka mmoja,akabagua yule mwizi wake, akagawa kichapo halafu akarudi porini kimya kimya Ni mnyama mdogo anayekula nyoka, kenge, majani, matunda, kenge, mizoga ya binadamu, chui, simba, duma, ndege n.k...kwa kifupi anakula kila kitu na ngozi yake ni ngumu sana kiasi kwamba mishale na mikuki au risasi ni ngumu kupenya..ukitaka kumuua ni kumpiga katika fuvu la kichwa chake na kitu kizito au risasi kichwani,katika guines world book of records yeye ndio the most fearless creature on the planet mwili wake haudhuriki na sumu ya nyoka wa kawaida na ikitokea ameumwa na nyoka mwenye sumu kali na sumu ikapenya kwenye damu yake itamfanya alale kwa masaa kadhaa tu kisha ataendelea na mambo yake. Ana meno makali/magumu sana yenye uwezo wa kupasua hata jumba la kobe.

Ashawahi kukutwa akipigana na simba na hata tembo na vifaru katika nyakati tofauti. Ni mvivu katika maswala ya nyumba yake hivyo basi anapojisikia uvivu hujilaza sehemu yoyote inayomfaa..ishaonekana akiwa kajiliza katika pango la mbwa mwitu kama kwake. Wanapatikana India,Kusini magharibi barani Asia na Afrika.

Source:Wikipedia
 
Angeacha hako katabia ka uvivu na kujilaza sehemu yoyote; huyu Nyegere angekua na tabia zote za binadamu wa kiume☺☺
 
Bila kusahau ngozi na mifupa yake hutumika kutengenezea limbwata pia ili mwanaume akupende na awe na wivu na ww.

Kuna mtu kaniambia hvyo
 
Bila kusahau ngozi na mifupa yake hutumika kutengenezea limbwata pia ili mwanaume akupende na awe na wivu na ww.

Kuna mtu kaniambia hvyo

Hakuna ujinga mkubwa kwa mwanamke kama huu wa kumfanya mwanaume akupende bila ridhaa yake
 
1. Picha yake tafadhali

2. Dawa yake ukishauchukua mzinga wake wa asali mnauweka kwenye ghala ambako hakuna kitu kingine zaidi ya asali na mmefunga kamera na maeneo ya ghala hakuna mlinzi wala mtu yeyote.

Aliyepeleka hiyo asali hapo akishaifungia ndani ya ghala anajipulizia manukato mbalimbali mwili mzima kisha anabadili nguo nyingine kurudi kwake.

Je, huyi nyuki atamfuata mrina asali hadi kwake pamoja na kuwa amevuruga harufu ya kijambo chake kwa manukato na kubadili nguo?

Nyuki akiingia kwenye ghala na asipoona mtu na haoni harufu ya kijambo chake ikitoka nje ya ghala atafanyaje?

NB: hilo ghala liko mbali na makazi ya mrina asali.

Nawaza na kujiuliza...
 
Kwa ambao hamjawah kumuona mbabe ndo huyu
 

Attachments

  • 37877113_108612570070759_1395785257902407680_n.jpg
    37877113_108612570070759_1395785257902407680_n.jpg
    12 KB · Views: 1
  • 29542933_121662222010293_1378809355980994852_n.jpg
    29542933_121662222010293_1378809355980994852_n.jpg
    16.6 KB · Views: 1
1. Picha yake tafadhali

2. Dawa yake ukishauchukua mzinga wake wa asali mnauweka kwenye ghala ambako hakuna kitu kingine zaidi ya asali na mmefunga kamera na maeneo ya ghala hakuna mlinzi wala mtu yeyote.

Aliyepeleka hiyo asali hapo akishaifungia ndani ya ghala anajipulizia manukato mbalimbali mwili mzima kisha anabadili nguo nyingine kurudi kwake.

Je, huyi nyuki atamfuata mrina asali hadi kwake pamoja na kuwa amevuruga harufu ya kijambo chake kwa manukato na kubadili nguo?

Nyuki akiingia kwenye ghala na asipoona mtu na haoni harufu ya kijambo chake ikitoka nje ya ghala atafanyaje?

NB: hilo ghala liko mbali na makazi ya mrina asali.

Nawaza na kujiuliza...
 

Attachments

  • 37877113_108612570070759_1395785257902407680_n.jpg
    37877113_108612570070759_1395785257902407680_n.jpg
    12 KB · Views: 1
7eb208fdef14ebe672fec5134828349a.jpg

9519be0a4136d19c361317f09f1b99f1.jpg

2d1d2d232acc2cc45ad5e8cc0873b4ad.jpg




1.Ni mnyama mdogo anayekula nyoka, kenge, majani, matunda, kenge, mizoga ya binadamu, chui, simba, duma, ndege n.k...kwa kifupi anakula kila kitu

2.ngozi yake ni ngumu sana kiasi kwamba mishale na mikuki au risasi ni ngumu kupenya..ukitaka kumuua ni kumpiga katika fuvu la kichwa chake na kitu kizito au risasi kichwani,

3.katika guines world book of records yeye ndio the most fearless creature on the planet

4.mwili wake haudhuriki na sumu ya nyoka wa kawaida na ikitokea ameumwa na nyoka mwenye sumu kali na sumu ikapenya kwenye damu yake itamfanya alale kwa masaa kadhaa tu kisha ataendelea na mambo yake

5.Ana meno makali/magumu sana yenye uwezo wa kupasua hata jumba la kobe

6.Ashawahi kukutwa akipigana na simba na hata tembo na vifaru katika nyakati tofauti

7.Anapenda kula asali, huwa anaupulizia hewa chafu mzinga na nyuki wote kulewa hivyo kula asali na kuondoka zake

8.Ni vigimu kumshambulia kwani ngozi yake inamfanya iwe rahisi kwake kujikaza na kujizungusha katika upande wowote anaotaka na kukujeruhi.

9.Ni mvivu katika maswala ya nyumba yake hivyo basi anapojisikia uvivu hujilaza sehemu yoyote inayomfaa..ishaonekana akiwa kajiliza katika pango la mbwa mwitu kama kwake.

Mengine angalia link ya youtube nimekuwekea chini[emoji116][emoji116][emoji116][emoji116]


Hiii mada ipo humu toka 2016, mleta mada umekopi uzi wa mkuu - barafu - na huja aknowledge popote!
 
Back
Top Bottom