Je, unataka kulima mazao ya mbogamboga na matunda lakini unakosa maarifa sahihi? Karibu tushauriane hapa

Kilimo Maarifa.
Asante kwa hizi taarifa.Ninajipanga kulima eka moja kwanza Kijiji cha shauri moyo Rufiji. Nitamwagilia kwa mifereji.Elimu hii itanisaidia.
 
KWA MICHE HIYO 3200 HADI 3500 KWA SUKARI F1 NAWEZA KUPATA MATUNDA MANGAPI? JE KWENYE SHAMBA LA TIKITI NAWEZA CHANGANYA NA MAZAO MENGINE, JE NAWEZA KUPANDA KWENYE SHAMBA NILILOCHIMBA VIAZI NA MAGONJWA YALIYOKUWA KWENYE VIAZI KAMA MNYAUKO YAWEZA KUDHURU TIKITI? NITATUMIA MBOLEA KIASI KUANZIA KUPANDA NA KUKUZIA. ASANTE SANA.
 
Taarifa nzuri [emoji817] ✔
Elimu madhubuti [emoji817] [emoji818]

Swali nitafanyaje ili matunda ya baki mawili tu? Asante
 
Niliwahi sikia Kuna kukata matawi. Je nayo hufanywaje?
 

Mkuuu niendelee kutoa Shukrani nyingi kwa elimu yako. Kuhusu document ya kitunguu nimekuemail. Sasa hapa kwenye tikiti napata shida kuelewa haya matuta ya kutumia furrow. Naomba more elaboration mkuu.
Nakushukuru
 
mseminari mdogo


Unachosema kiongozi kipo pia kinafanyika ila si na wakulima wote, Ila kiutaalamu kinaruhusiwa, Ntaeleza hapa chini

1, Ni kuwa ukishahesabu katika kamba moja ukapata vile vitumba vyenye tikiti viko vitatu , baasi yale maua mengine yanayokuja kuleta tikiti la nne na kuendelea unayaondoa.

Na kiutaalamu tunashauri yale matunda 3 yawe katika main stem-Maana hii main stem (Shina kuu) ndiyo ina tissue muhimu za kusafirishia maji (Xylem) na chakula (Virutubisho) (Phloem), yaani matunda yawe katika shina/kamba mama ile KAMBA iliyotoka chini SIYO MATUNDA yaje kujitengenezea katika secondary brach (Tawi la pili) lililo gawanyika kutoka katika kamba kuu (Kamba mama) hayo huwa mengi yanakuwa madogo kwa sababu ya kukosa lishe, na baadhi huwa yanakufa/nyauka

2, Pia baada ya kupata yale matikiti matatu wapo ambao hukata ile kamba mbele ili chakula kisiendelle kwenda kule mbele ambako hakuna matikiti so unakuwa ni upotevu wa lishe ya bure, hata kama ni dawa za wadudu unakuwa unaspary kule mbele sehemu ambayo haina production inakuwa ni hasara,


Niliwahi sikia Kuna kukata matawi. Je nayo hufanywaje?
 
Email nimeipata mkuu.
Matuta nimeyapata sasa vizuri. Hii ni nzuri kwa sisi ambao ndio tunachipuka tusio na drips kwa sasa.
Pdf ya kitunguu wow.. Tam sana. Hapa ninavyopita niko kama naangalia filam mkuu. Inaeleweka vyema sana sana. Inanionesha shambani kabisa from kuanza hadi kuanza kufunga pesa baada ya kuvuna. Nitaifanyia kazi ilasavyo.
Nashukuru tena mkuu.
 
Asante nitafanya hivyo.

Sent from my PTM-Z-mini using JamiiForums mobile app
 
Mkuu tunaisubiri kwa hamu hiyo. Hivi mkuu kumwagilia nyanya kitaluni na maji yenye mchanganyiko wa mbolea niufanye angau mara ngapi tofauti na ule wa kawaida wa kila siku asubuhi na jioni?
 
NAOMBA KUULIZA JE NAWEZA KUPANDA NYANYA AINA YA ANNA FI SEHEMU YA WAZI NA SIO KWENYE GREEN HOUSE NA IKAZAA VIZURI. JE EDEN F1 NAWEZA MWEZI WA TISA ILI NIVUNE MWEZI WA KUMI NA MOJA NA MBILI KWA NJIA YA KUMWAGILIA, AU INAFAA MASIKA TU. ASANTE
 
 
kilimomaarifa.tajiri nimelima matikiti sasa yako tayarikuvunwa ila kuna ugonjwa wanaita dot.com yaani matikiti yanakuwa na vidoti kwa chini kule kunakogusa chini je kuna namna yeyote ya kuzuia huu ugonjwa? ili wakati mwingine nikilima niweze kutibu kabla
 
Mkuu Habari,naomba Kufahamu Mambo Yafuatayo: 1.Kuna Dawa Inaitwa Swing Sc Nimeambiwa Ni Dawa Ya Kuzuia Mnyauko(wilt) Kwenye Mimea Kwamba Inapulizwa Kwenye Mashimo Kabla Ya Kupandikiza Sasa Naomba Kujua Ni Kweli? Pia Naomba Kujua Ni Kwa Namna Gani Naweza Kuzuia Athar Za Mvua Kwenye Kitalu Cha Nyanya? Namaanisha Maji Kupita Kiasi Na Ukungu Na Je Net Au Nyasi Zinaweza Kusaidia? Pia Kuna Ugonjwa Wa Kiuno Wa Miche Ya Nyanya Mara Kadhaa Nimeona Ukitokea Hata Kama Kitalu Kilichomwa Moto Kabla Ya Kuatika Mbegu. Nini Husababisha? Na Ninatibu Vipi Ugonjwa Huu Kwa Miche Ambayo Tayari Imeathirika? Na Je Kuna Dawa Yeyote Ambayo Naweza Kupuliza Kama Kinga?
 
POLESANA MKUU; -JARIBU KUWA BRIEF KIDOGO ILI NIKUELEWE ZAIDI, NI VIDOT VYA NAMNA GANI (RANGI, SAIZI ETC)-VIKOJE HIVYO VIDOT???

JE NI SHIDA KAMA HIZI HAPA CHINI??/

ndio, ni kama hivyo ila sio vimetobolewa na wadudu, vinakuwa vidoti kama hivyo ila vya brown ambayo ukifanya kama kukanyaga hilo tikiti linatoa maji.
 
Mkuu kilimo nyanya imekubali kitaluni ila vilepeo weupe nimewaona around leo. Nina duduall na dimethoate zaweza kuwadhibiti au nikatafutr nyingine? Nilikuwa jumamosi nizipeleke shambani je niendelee kuwashughulikia hawa jamaa kwanza hadi wafie mbali au naweza hamisha baada ya kupiga dawa tu. Nashukuru mkuu
 
Dah mkuu moyo wabubujika kwa furaha. Mungu akupe faraja ya moyo wako.. Nimefarijika sana. Nakumbuka sana mkuu.. Kiganja kimoja kimenyooka kwenye kita 15 zangu.. Starter soln. Ngoja nipambane.. Nina imani ndio njia inanyooka ya matamanio ya moyo wangu. Kuwa mkulima bora..

Nashukuru
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…