mseminari mdogo
JF-Expert Member
- Aug 18, 2011
- 228
- 146
End of March nataka niweke tikiti
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
End of March nataka niweke tikiti
Nitatumia mvua. Kilimo maarifa. tajiri maji yote ya Mungu [emoji23] [emoji23] [emoji106]SAFI SANA. UTATUMIA MVUA YA MUNGU AU DRIP/ UTAMWAGILIA KWA MIFEREJI???
Nitatumia mvua. Kilimo maarifa. tajiri maji yote ya Mungu [emoji23] [emoji23] [emoji106]
Niliwahi sikia Kuna kukata matawi. Je nayo hufanywaje?UNAYATOA NA MIKONO YALE MATUNDA MENGINE YANAYOENDELEA BAADA YA HAYO 2, LAKINI 3 NI STARDARD KUBAKI YATAKUWA MAKUBWA KULIKO KUACHA 5 AU 7 KAMA WENGINE WANAVYOFANYA YALE YANAYOENDELA BAADA YA YALE 4 YA KWANZA UNAKUTA YANAKUWA MADOGO, NA HATA MENGINE HUWA HAYAFIKII HATUA YA KUKOMAA YANAKAUKA.
NEW NEW NEW 22/01/2016
=================================
BAADHI YA TAARIFA ZA ZIADA KWA WAKULIMA WA TIKITI
-Utahitaji kwa wastani gram 250-hadi 350 kupanda kwa eka 1
MBEGU Itakugharimu wastani kati ya TSH130,000 hadi 250,000TSH
-Utakuwa na miche kati ya 3200 hadi 3500 kwa eka 1
-Nafasi ya kupanda
xxx SM 90 Kutoka mche mmoja hadi mwingine, na sm 150=1.5Mita kutoka KATIKATI YA tuta moja hadi lingine-Njia ya umwagiliaji ni DRIP
AU sm 100 kutoka mche mmoja hadi mwingine, na sm 200=Mita 2 Kutoka katikati ya tuta moja hadi Lingine-Njia ya Umwagiliaji ni DRIP
KUMWAGILIA KWA MIFEREJI (Furrow Irrigation)
-Tengeneza jaruba la upana wa mita 2 hadi 3, lenye urefu wowote ule unaoweza kuhimili kutoa huduma urefu wa weza kuwa mita 5 hadi 10mita
-Kisha katikati ya jaruba pafanye pawe sunken-Pabonyee kidogo
-Utapanda mbegu zako kwa nafasi hizo hapo juu Sm 90 au 100 kutoka mche mpaka mwingine, panda pembeni mwa hizo pande nne za jaruba, upande chini kidogo karibu kabisa na kitako (chini) ya jaruba
-Kisha tikiti zitakapoanza kuota utazitrain zote zije kulala hapo katikati (sunken center)
Aina ya Mbegu- Mistari-MUDA WA KUKOMAA UKUBWA (KG) Kampuni
1.SUKARI F1-Mistari ya Punda milia siku 80-90 7-14 kg -East African Seed
2. -Julina F1-Mistari ya punda milia siku 85-90 8-12kg -Kibo seed
3.-Mshindi F1-Mistari ya punda milia Siku 75-80 5-9 kg -East West seed
4. -Daytona F1-Mistari ya Punda milia siku 75-80 10-12 kg -Kibo seed
5. -Jubilee/Tiger stripe-Mistari ya pundamilia siku75-85 5-12kg -East African Seed
6..-Creemson sweet Ni la kijani tu siku 80-85 5-10 kg -Kibo seed
BAADHI YA MBEGU ZINAZOHIMILI MAGONJWA
1.-Juliana is the best huhimii magonjwa mengi ya ukungu na wadudu
2.-Daytona F1-Huhimili sana magonjwa ya ukungu shambani
3.-Creemson Sweet-Hustahimili magonjwa ya Ubwiri Unga/Ubwiri Poda/Powdery Mildew
Niliwahi sikia Kuna kukata matawi. Je nayo hufanywaje?
Email nimeipata mkuu.chayowa
Kiongozi Nashukuru sana
-Kuhusu E-mail
-Email yako nimeiona na nimeshakujibu mkuu-Karibu sana
Kuhusu haya matuta ya Tikiti ya kutumia furrow
-Inakuwa hivi mkuu, Haya ni majaruba yanakuwa kama ya mpunga (kama ulishayaona) yanakuwa mapana, na hayainuki kuja juu, haya yanabonyea katikati au unayafanya yanakuwa flat tu, kwahiyo unachokifanya unavuta udongo kutoka pande zote nne zinainuka kiasi upana huwa tunashauri uwe angalau mita 2 hadi 3 urefu ni ule utakaoweza ila tunashauri angalau uwe mita 5 hivi
-Sasa kinachofanyika kiongozi, yanakuwa kama yale matuta ya nyanya ya kumwagilia kwa njia ya mifereji (furrow), yaani maji unayaingiza kwa block, huku zingine unafunga
-Mbegu za tikiti unazipanda chini/ukingoni mwa tuta karibu kabisa na hiyo furrow ili maji yanapopita kufuaa ile mifereji ya pembeni mwa tuta ile mbegu/miche ya tikiti inapata hayo maji
-Mche wa tikiti ukianza kutambaa sasa ndio unaanza kuutrain uje kulala/kutambalia pale katika ule upana wa mita 2 ulioacha mkuu, kwa hiyo Tikiti zote za pande zote nne unazileta zije kutambalia hapo juu mwa tuta lako
Nadhani umenipata
Asante nitafanya hivyo.mseminari mdogo
Unachosema kiongozi kipo pia kinafanyika ila si na wakulima wote, Ila kiutaalamu kinaruhusiwa, Ntaeleza hapa chini
1, Ni kuwa ukishahesabu katika kamba moja ukapata vile vitumba vyenye tikiti viko vitatu , baasi yale maua mengine yanayokuja kuleta tikiti la nne na kuendelea unayaondoa.
Na kiutaalamu tunashauri yale matunda 3 yawe katika main stem-Maana hii main stem (Shina kuu) ndiyo ina tissue muhimu za kusafirishia maji (Xylem) na chakula (Virutubisho) (Phloem), yaani matunda yawe katika shina/kamba mama ile KAMBA iliyotoka chini SIYO MATUNDA yaje kujitengenezea katika secondary brach (Tawi la pili) lililo gawanyika kutoka katika kamba kuu (Kamba mama) hayo huwa mengi yanakuwa madogo kwa sababu ya kukosa lishe, na baadhi huwa yanakufa/nyauka
2, Pia baada ya kupata yale matikiti matatu wapo ambao hukata ile kamba mbele ili chakula kisiendelle kwenda kule mbele ambako hakuna matikiti so unakuwa ni upotevu wa lishe ya bure, hata kama ni dawa za wadudu unakuwa unaspary kule mbele sehemu ambayo haina production inakuwa ni hasara,
chayowa
SAWA KIONGOZI PDF YA NYANYA IKIWA TAYARI NTASEMA
1. UMWAGIA MAJI YENYE MBOLEA UNAWEZA KUWA UNAUFANYA KWA KILA BAADA YA SIKU 7(kwa wiki mara moja, so unaweza kuwa unafanya kila jumatatu unamwagia asubuhi maji yenye mbolea)- KWA MAZAO AMBAYO HAYAMALIZI MWEZI KITALUNI. Hii iko applied sana kwa mashamba ambayo yamekuwa yakilimwa mara kwa mara-RUTUBA YA UDONGO UNAKUTA IKO CHINI SANA. LAKINI kama shamba ni virgin/HALIJAWAHI KULIMWA, utamwagia MAji yenye mbolea mara 2, ile wiki ya kwanza miche ikiota na ile wiki ya mwisho utakapokuwa unakaribia kuitoa iende shambani
2. NA UNAWEZA KUWA UNAMWAGILIA KILA BAADA YA SIKU 14 KWA MAZAO YANAYOMALIZA ZAIDI YA MWEZI KITALUNI KAMA KITUNGUU etc
Bila shaka umenipata.
Nimekupata sana mkuu.
Nashukuru mno mno
ndio, ni kama hivyo ila sio vimetobolewa na wadudu, vinakuwa vidoti kama hivyo ila vya brown ambayo ukifanya kama kukanyaga hilo tikiti linatoa maji.POLESANA MKUU; -JARIBU KUWA BRIEF KIDOGO ILI NIKUELEWE ZAIDI, NI VIDOT VYA NAMNA GANI (RANGI, SAIZI ETC)-VIKOJE HIVYO VIDOT???
JE NI SHIDA KAMA HIZI HAPA CHINI??/
![]()
![]()