Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

Uchaguzi 2020 Je, Unaweza kupita Ubungo Interchange usiseme asante Magufuli? Mtakubaliana na mimi, asante stahiki ni kura zote kwa Magufuli

Magufuli anatenda lile analoliongea na tabia hiyo inampatia heshima kubwa kwa watu.

Nimemkosoa Lissu mwenye agenda mbaya zilizojificha katika ujengaji wake wa hoja.
Wapi 50ml kila kijiji?
Wapi laptop za walimu?
Wapi umoja kama taifa?
Wapi uhuru wa kujieleza?
Kulikoni mauaji ya wakosoaji?

Ccm hamna utu na mmeiharibu nchi, ilikuwa kisiwa cha amani sasa inaelekea kuwa Sudan
 
Acha Niseme hivi kama Mh Rais Magufuli atapita tena tutalia na kusaga meno hata wale wanao jiona salama hawataamini.

Lissu alishasema wakimalizana na sisi watakuja kwenu tunaenda kuangamiza umoja na mshikamano wa taifa letu.

Kiongozi ambae anajua kachaguliwa na wananchi hawezi kusema mkiniletea wapinzani sileti maendeleo hii kauli inaniumiza sana.

Huu ni ubaguzi wa wazi kabisa ila tume wanaona sawa tu
Mungu yupo. Tanzania itaenda kuandika historia nyingine walikuwepo wababe ambao wananchi walikuwa wanapata kila kitu lakini walikufa kama mbwa. R.I.P Kanali Muammar Gaddafi ulikuwa ni nembo ya Afrika lakini watu walikosa uhuru wa kujieleza kutoa ya moyoni tu.

Tusiruhusu Tanzania yetu kubaguana kiitikadi hatukuzoea hivyo sisi
 
Jibu ni jepesi saana hizo pesa ziliwekezwa sehemu nyingine kama kuimarisha sekta za elimu,afya,wafanyakazi kuongezewa mishahara kila mwaka, kujenga mazingira mazuri ya kufanya biashara kwa wafanya biashara bila kuwabambikiza kodizi sizokuwa na kichwa.

Ethiopia inaongoza kwa "flyover" za maana Africa sio kama ka kwetu lakini wananchi wake ni maskini wa kutupwa.

Naona umesahau pia kumsifia kwa kuweza kujenga uwanja wa ndege nyumbani kwake kwa ajili ya watalii wa kisukuma jambo ambalo halikufanyika miaka 50 iliyopita.
 
Naomba sababu tatu tu, kwanini nisiseme ahsante walipa kodi watiifu niseme ahsante Magufuli ambaye tumemtuma asimamie vizuri fedha zetu ili zilete maendeleo kama hayo!?
aliyeleta mada amekimbia. upambe una gharama
 
Kwahiyo hata Kikwete ambaye huu mradi ukianzia kwenye serikali yake tusimkumbuke kama mlimvofanya lile daraja la Kigamboni? Kwa nini watu wa huko ni wabaguzi sana?
 
Pesa itoe world Bank tena ya mkopo, pongezi apate magufuli? Ukiwa na njaa na mpumbavu kama wewe unaweza fanya huo ujinga
Mkuu mwanafunzi wa Chuo kikuu akikopa pesa bodi ya mikopo, degree anayopata ni yake au ni ya bodi ya mkopo? Pongezi anapewa yeye au bodi iliyomkopesha.

Na vipi ukikopa fedha bank ukajenga nyumba, hiyo nyumba unajisifia ni yako au unasema ni ya bank iliyokukopesha?. Tuwe wakweli interchange hii ni mali yetu siyo ya Bank ya Dunia.Fedha ni za yetu kwa kuwa tutazirejesha. Tungewza kukopa na zikaliwa. Magufuli Oyee.
 
Yani majukumu ya serikali leo hii inageuka fadhila? Halafu huyu anaesema haya ni mtu mwenye LL.b hahahah...😀😀😀😀
Halafu pesa ya Mabeberu... Leo tunaishangilia kukamilisha mradi. Hivi mpaka Sasa kuna nini Magufuli ameacomplish kwa pesa zetu bila mchango wa Mabeberu....!!?
 
“You don't necessarily need atomic bombs to destroy a nation. Politicians like Paskali Mayala who value their pockets than the life of citizens always do that every day.” ~ Israelmore Ayivor
 
Pasco nduki kakimbia uzi wake leo utalala na viatu uache kupost ujinga ujinga ndugu yangu watu wananjaa we unaleta ishu za daraja
 
Kuna kiongozi na mwanafalsafa mmoja maarufu Duniani (jina nimelisahau) aliwahi kusema kuwa kama kuna mpiga kura anamchagua kiongozi wa nchi kwa sababu serikali imejenga barabara, reli, au madaraja, basi mpiga kura huyo ni mjinga. Maana hayo kila serikali hufanya.

Kwa hiyo, huo ujinga ubaki nao mwenyewe, Mayala. Sisi wengine tunahitaji kiongozi mwenye uwezo mkubwa zaidi wa kutengeneza mazingira wezeshi ya kumpa mwananchi maendeleo binafsi, ikiwa ni pamoja na kuupa thamani utu wake, kulinda uhuru wake, kuliko ujenzi wa interchange 1 iliyopo Ubungo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Paskali ni mwanasheria lakini hajui logic kabisa!
Ni kweli kabisa wale wote waliokuwa wanakwama kwenye foleni inabidi washukuru. Lakini hawa ni wachache mno katika jamii nzima ya watanzania.

Ni vigumu sana kumshawishi mtu wa Tandahimba ashukuru kwa sababu kuna interchange ya kileo Ubungo wakati yeye barabara kwenda kijijini kwake au Mtwara haipitiki. Itakuwa unamtonesha kidonda.

Amandla...
 
Labda wa dar, wa namtumbo, newala, buserere, tarime ana kipi Cha kumshawishi kwamba Kodi yake atanufaika nayo vipi
 
Nimekudharau mno mayala. Unaandika vitu vya kijinga siku hizi.
 
Nobody can give you freedom. Nobody can give you equality or justice or anything. If you're a man, you take it.” ~ Malcolm X
 
Back
Top Bottom