johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 97,869
- 171,716
Vyama kwa Afrika havina umuhimu kwa wananchi ni magenge ya kupiga pesa za wananchi.Andika vyama vifutwe kabisa
Mimi napendekeza Rais anapostaafu ashitakiwe kwa mujibu wa sheria iwapo alikiuka utaratibu wakati anatawala .Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo
Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi
Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa
Karibu
Usiseme Afrika sema Chato na Sukuma gang empire vyama vya siasa havina umuhimu.Vyama kwa Afrika havina umuhimu kwa wananchi ni magenge ya kupiga pesa za wananchi.
Hii point ni muhimu hizi kazi za kiuongozi ziwe kadhi za wito.Pia viongozi wa mkoa wapunguzwe, pia mtu akifanya kazi miaka mitano arudi mtaani akajiajiri, waingie wengine mzigoni(kuhusu uzoefu mimi sijui, sababu siyo HRM)
Rais wa Tanzania lazima atoke Tanganyika, Haiingii akilini kisiwa chenye watu milion mbili, kitoe marais wawili kuongoza watu milion 60,Waziri wa Katiba na Sheria ameshapuliza kipyenga cha mchakato wa Katiba Mpya hivyo ni vema tukaanza kuchangia mawazo
Binafsi napendekeza Ruzuku ya vyama vya Siasa iondolewe ili vyama vijifunze Kujitegemea ili vikiingia madarakani visiwe Mchwa wa kutafuna Kodi za Wananchi
Toa mapendekezo yako wahusika watayaona na kuyachukua kutoka hapa
Karibu
Pia chama cha Mambuzi kirejeshe viwanja na mali zote,Naunga mkono hoja, vyama viendeshwe na wanachama.