Je, upangaji wa matokeo bado ni changamoto ligi ya championship?

Je, upangaji wa matokeo bado ni changamoto ligi ya championship?

carnage21

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
591
Reaction score
1,382
PAMBA WALALAMIKA KUFANYIWA FIGISU

Uongozi wa klabu ya Pamba ya Jijini Mwanza umeomba uongozi wa TFF kuchunguza Upangaji wa matokeo kwenye Mchezo wao wa jana 1st leg play off dhidi ya Mashujaa FC mchezo uliofanyika Mkoani Kigoma ambao Pamba kupoteza (4 - 0).

Wadai wamefanyiwa uhuni, Wachezaji wao wameoneshwa kadi za njano (7) + (1) nyekundu ndani ya dakika (11') kipindi cha kwanza mchezo ukiwa (0-0).

Kipindi cha pili wakaoneshwa kadi zingine (2) nyekundu zikawa jumla kadi (3) nyekundu... Kama haitoshi mwamuzi akawapa penati mbili Mashujaa FC na Mpira kumalizika (4 - 0)

Pia kuna mchezaji wao amejeruhiwa na mbwa wa makomandoo wa Mashujaa FC.

Haya yote yametokea jana tu,je ni kweli upangaji wa matokeo ni changamoto Tanzania hasa ligi ya championship??
FB_IMG_16847257153158933.jpg
 
Shida inaonekana mishahara ya marefa haijitoshelezi ndo maana wanakua rahisi kurubuniwa
Asiachwe hivihivi, refa hata akichukuwa pesa kuna njia za kuibeba timu itumie uwezo wake wewe kazi yako ni kuwapa advantage zinazotokea na siyo kulazimisha timu ishinde hata kama haina uwezo.
 
timu za majeshi ziwe na ligi yao wataua watu, siku moja nliangalia mechi ya Rhino rangers na Pamba ile mechi ilikua zaidi ya vita mbaya zaidi Pamba alikua nyumbani ila alinyanyasika kama yupo away
Aisee na ruvu shooting ndo hao wanashuka huko itakua balaa tupu
 
Mbao ni team isiyo na Nia thabit, kila msimu ujingaujinga Kuna metch tatu mlipoteza mfulizo zile ndo zingewapeleka ligikuu direct kabisaa nyie mkafanya ujinga.
MWANZA Yotee tiamajitiamaji.

Waacheni wanajeshi wakaipambanie KG.
 
Pamba ilikua ipande tangia mwaka jana mpira wa bongo ni fitna na uhuni mwingi,mji wa Mwanza auna watu wa aina iyo ndio maana Pamba wanapata tabu sana kupanda maranyingi wananyang'anywa tonge mdomoni.
 
timu za majeshi ziwe na ligi yao wataua watu, siku moja nliangalia mechi ya Rhino rangers na Pamba ile mechi ilikua zaidi ya vita mbaya zaidi Pamba alikua nyumbani ila alinyanyasika kama yupo away
Hivi wanaruhusu taasisi moja kuwa na timu zaidi ya mbili ktk ligi au mashindano ?
 
Back
Top Bottom