Je, ushawahi kuhisi tukio kabla ya kutokea na likatokea? Tuelezane, kwako ilikuwaje?

Je, ushawahi kuhisi tukio kabla ya kutokea na likatokea? Tuelezane, kwako ilikuwaje?

Kuna mtu nilimuwaza na kupata hali kama hanipendi kutokana hasa na namna ambavyo hunitizama(ni shangazi wa kambo) baada ya siku 3 alinipigia eti kunisalimia ilhali hajawahi kunipigia simu ya kunisalimia, imetokea wiki hii hii
 
Wakati mwingine hisia sio za kupuuzwa. Kuna nyakati unaweza kuwa mahali fulani ukahisi jambo, lakini kwa kujifanya jeuri au kutosikia sauti ya ndani, unajikuta unayapitia yale yale ambayo ulionywa mapema.

Kwa kifupi, visa kama hivi vipo vingi sana kwenye maisha ya kila siku. Ngoja nikupe mfano wa moja lililonitokea zamani, halafu na wewe utatuambia lako lilivyokuwa.

Siku moja, kipindi kile cha nyuma, nilikuwa nimetoka kununua kasimu kangu ka Nokia. Enzi hizo vinatok bado vinaonekana kama ndilo dili la mjini yaani ukiwa nacho unatembea kifua mbele.

Ilipofika usiku, kama kawaida, ikabidi niende chooni. Sasa unajua vyoo vile vya kulenga… kabla sijaingia ndani, kuna kitu ndani yangu kikanionya:
“Acha simu nje, utakaacha huko.”

Lakini kwa nini nisikilize? Mimi nikajifanya jeuri. Aisee, ningejua…

Basi safari ikaendelea. Sijamaliza hata ‘kukata gogo’ vizuri, gafla bin vuu — pluup!
Nikashtuka! Nikahamaki!
“Aaaah! Tubwiliiii!”

Kasimu kangu ka Nokia tayari kazama chooni! Hapo ndio nikakumbuka ile hisia ya mwanzo… lakini too late.

D9 nitakuwepo
Nilitaka nichangie nitoe bongo nondoz na madini ya kutosha ila nilivyoona umesema "D9 utakuwepo" nimeacha kuchangia uzi
 
1.Kuna siku niko na mwana tunakula gambe saa 4 asubuhi tena siku ya kazi ghafla wakaingia ******* wawili wakatusalimia wakakaa kwenye viti nikawaza ni Askari halafu ikaishia hapo ndipo mmoja akaanza kujitambulisha wao ni Askari akatoa kitambulisho akanipa nikiangalie kisha akaanza kutuuliza maswali kwanini tunalewa mda wa kazi

2.Tarehe 30/10/2025 siku iliyoifuatia siku ya uchaguzi niliwakuta jamaa ninaowafahamu wakiwa wamekaa sehemu kando ya barabara wakiwaangalia polisi wanavyopita wakienda na kurudi huku wakipiga mabomu,pia walikuwa wanaongelea habari za kumdiss samia,katika wale jamaa ninaowajua alikwepo pia mtu ambaye sura yake ni ngeni nae akichangia mada nikamuhisi tofauti kimoyomoyo kuwa ni askari nikataka nimwambie inawezekana yeye ni Askari ila nikapotezea,mara wale Askari waliokuwa wanapita kwenye gari wakatupa kibomu karibu na tulipokuwa hakikulipuka kikawa tu kinafuka moshi watu wakanyanyuka kwenda kukifunika na mchanga hata yule msenge niliyekuwa namtilia mashaka nae alienda hapo ndipo jamaa mmoja akatustua akasema nyie jamaa mnaakaje na Askari wale jamaa wawili mliokuwa nao ni Askari japo mimi nilimuhisi mmoja
Ilitakiwa aseme mnakaaje na snitch
 
Kwanza nimekumiss mamii...
Pili; hili nami huwa linanitokea sana. Upo powa lakini?
😍😍 Weeehh.!!
Niko pouwa, vipi wewe?

Na wewe inakutokea kumbe?
Sijui kwanini huwa hivyo?

Au tuliwahi kuishi hapo mwanzo tumerudi tena kwa mara ya pili? 😹
 
Kuna mtu nilimuwaza na kupata hali kama hanipendi kutokana hasa na namna ambavyo hunitizama(ni shangazi wa kambo) baada ya siku 3 alinipigia eti kunisalimia ilhali hajawahi kunipigia simu ya kunisalimia, imetokea wiki hii hii
Uyo Kuna mchezo mchafu kakufanyia alikuwa anakupigia simu ahakiki kama alichokufanyia kimefanya kazi mshukuru sana Mungu wako
 
Huwa akinuia jambo subconsciously anaweka juhudi na maarifa ili litimie. Halafu likitimia anajiaminisha kuwa ana nguvu za ziada 😂

Chura siyo wa kuondolewa kwa manuizi!
Wapo wenye uwezo huo wa kunuia kitu na kikatokea ila inahitaji kujitayarisha,

Mfano mwingine kipindi cha MO29, kuna shosti yangu mmoja mumewe ni wale mashehe wa wilaya (waganga) sasa hicho kipindi akawa anajifanya kuuliza sana nini kinawndelea DSM kujifanya anaulizia km niko salama, ila nafsi ikanishuhudia huyu taarifa anampelekea mumewe, kuna uwezekano ni mmoja wa waganga wa chura,,

--- maana mumewe huyo alikuwepo dar na aliondoka tarehe 28 haraka haraka akimwambia mkewe kuwa anahisi harufu ya damu kutatokea mauaji,,, hili aliniambia 29th Oct asubuhi kabla hata mtandao haujazimwa,,, ila nikapuuza
 
Kwa nini uendekeze nyeto wakati Wanawake wapo wengi , na huoni kwenye nyeto unakosa vitu vingi sana tofauti na yenyewe ?

Kwa nini usitafute Mke wa kuoa ?
Ww kwa hao wanawake umepata nn cha maana ambacho mm nmekosa?
 
Mimi huwa naona kitu kabla hakijatokea na siku ikifika nasema tayari yametimia..!!

Kuna sehemu sijawahi kufika toka nizaliwe ila siku nikifika najua kila kitu mpaka njia za mitaa na maduka bila kuambiwa.!!
You're partially foreseer. A Precog
 
Mimi huwa naona kitu kabla hakijatokea na siku ikifika nasema tayari yametimia..!!

Kuna sehemu sijawahi kufika toka nizaliwe ila siku nikifika najua kila kitu mpaka njia za mitaa na maduka bila kuambiwa.!!
Baby huu sasa ni uongo😂
 
You're partially foreseer. A Precog
Ohh!! Kwahiyo naweza kufanya jambo nikapiga pesa?

Kuna siku niliona kiumbe cha ajabu kinanifanyia massage nikakifukuza, kesho yake baba mwenye nyumba akanitumia mtu anipe notisi. 😹

Kuna hii nyingine mpaka najishangaa, nikiingia duka lolote kununua mahitaji basi ghafla linajaa wateja lakini nikiondoka na wateja wanaondoka..!!

Hii inanitokea sana hata dukani kwangu, vijana wanalalamika biashara ngumu lakini nikifika tu wateja wanajaa mpaka wengine wanasahau chenchi, vijana wananihisi tofauti labda kigagula 😹😹😹
 
Siku Moja kabla ya juzi usiku nipo zangu jamiiforum napitia thread Moja hivi " bundi kulia usiku inamaana gani ?? "

Baada kama ya siku mbili nikiwa nimelala,, ilipofika saa Tisa na dk 31 nasikia kama kitu kimetua juu ya bati katika nyumba niyokuwa nimelala ,, baada ya dk 2 nasikiamlio wa bundi .. nikajiseema Yale Yale niliosoma kwenye Ile thread ..

Basi bwana nikaamka nikachukuwa coprin ya maji kwenye droo sehemu ambayo Huwa ninaweka vifaa mpaka uwanjani ili niweze kuona vizuri juu ya bati ,, basi baada ya kuona location ya sehemu alipo bundi yule namrudhia Ile coprin ya maji yule bundi anaamua kukimbia

Wakati hayo yakiendelea Moja ya mpangaji ( jinsi ke ) ananiona na Mimi namuona kwa kupitia dirisha .. Asubuhi inafika ,, yule jirani ananiambia bundi huyu ni wiki Sasa amekuwa na tabia ya kuja hapo hapo ulipomfukuza leo na kuanzia kulia usiku,, nikamjibu kuwa Kuna sehemu nimesoma kuwa bundi akiwa Analia usiku katika mtaa Fulani wanadai si ishara nzuri lazima msiba utatokea tu katika mtaa huo hivyo nikama Huwa anatoa taarifa ..

JIrani akesema mmhh uongo huo bundi anamahusiano yapi na msiba ,, nikajibu kule nilikosoma wamesema bundi anauwezo wa kutabili mauti ya mtu au kunusa seli zinazokufa ktk mwili wa mtu anayeumwa hivyo yeye huweza kujua kuwa muda si mrefu mtu huyu atakufa ... Yule mpangaji akasema ya kweli hayaa ??

Nikamwambia bwana Mimi sijui ila kwa kifupi tu huyu ndege kulia Lia usiku kama vile Huwa analeta uchuro tuu basi tukaachana na Kila mtu akaendelea na mishe zake


Eehh !! Imefika saa sita mchana ,, tunaona watu wengi wanaelekea kwenye Moja ya nyumba ambayo haipo mbali sanaa na pale tunapoishi ikabidi na sisi tuunge ule msafara ili kujua Kuna Nini huko??....
Eehh !! tunafika pale tunakuta jamaa kajitundika ( kinyinyonga )

Kuuliza kulikoni
Wanasema jamaa baada ya kuona mkewe yapata siku tatu hajarudi nyumbani basi akawa kajifungia ndani Sasa majirani walipoona mbona huyu Leo Toka Asubuhi hajatoka wakaenda kumwambia Moja wa aliyekuwa rafiki yake ,,, alipofika pale na kujaribu kufungua mlango kwa nguvu ndiyo kumuona rafiki yake akiwa kajinyonga ndiyo kuwaambia majirani na majirani kuamua kumjulisha mwenyekiti na taratibu nyingine za kuwataarifu polisi na kumsitili zikaendelea

JIrani haishi kunitazama na kuniuliza maswali mengi ila nilichofanya nikumpa Ile thread na yeye apate kujisomea mwenye na kujiongezea maarifa ili nisije onekana mchawi buree kumbe walaa ...
 
Baby huu sasa ni uongo😂
Baby kweli tena 😹😹😹

Unajua kuna mtaa nilihamishwa kkoo kwa pesa ndefu kisa nauza sana..!!

Jirani yangu akaamua anivue kwa pesa ili nimuachie wateja wake. Maana nilikua nasepa na kijiji..!!
 
Back
Top Bottom