Uchaguzi 2020 Je, utabiri wa Mwalimu Nyerere kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM kuanza kutokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu?

Uchaguzi 2020 Je, utabiri wa Mwalimu Nyerere kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM kuanza kutokea katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu?

Wewe unawaza kibinadamu na Mungu ana mipango yake........

Lisilowezekana kwa binadamu, linawezekana kirahisi sana kwa Mungu wetu Mkuu kushinda vitu vyote
Mbona Magufuli qliposema tuombe kwa ajili ya janga la corona ulimbeza?
 
Hivi kwa nini mnamfanya Nyerere kama nabii..alianzisha vyama vingi kwa katiba ya chama kimoja..Dictatorships
 
Mbona Magufuli qliposema tuombe kwa ajili ya janga la corona ulimbeza?
Crimea
Nani alimbeza?

Katika mambo machache sana ambayo nimewahi kumwuunga mkono Rais Magufuli ni kwa uamuzi wake wa kulitaka Taifa tumwombe Mungu ili atuepushe na janga la corona
 
Siasa za Nyerere umezisoma ila hukuwapo..
Ni worse than this.... ila woga ulitawala.

Karatasi ya kura ilikuwa picha na kivuli....

Hapana... hapana mwingine zaidi yake
Ndio... tumemkubali anafaa aongoze milele

Nipe tofauti ya kimantiki kati ya utawala wa Nyerere na huu.
 
Hapana

Hajafukuzwa na mkutano Mkuu wala Halmashauri Kuu, bali ni hiyo Kamati Kuu ambayo katika utawala huu wa awamu ya tano "inajimwambafai" na kujona yenyewe ni sawasawa na mungu mtu
Sasa yeye mwenyewe kasema haina mamlaka hiyo, kwa hiyo hajafukuzwa, yeye kwa kutumia haki na ubobezi wake akachukue fomu.
 
Crimea
Nani alimbeza?

Katika mambo machache sana ambayo nimewahi kumwuunga mkono Rais Magufuli ni kwa uamuzi wake wa kulitaka Taifa tumwombe Mungu ili atuepushe na janga la corona

Huyo amekariri, kwa sababu yeye anamuunga mkono Magufuli kwa kila kitu, basi anadhani kila asiyemkubali Magufuli, basi anapinga kila kitu chake.
 
Katika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM

Kutokana na kujitokeza kwa mwanasiasa, Bernard Membe kudai kuwa amepania kuchukua fomu ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, ndiko kunakonifanya nione kuwa utabiri wa Mwalimu Nyerere unaweza kuanza kutimia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu

Kwa maelezo anayotupa yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa amepania kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, tena akiendelea kusisitiza kuwa Kuna kundi kubwa sana la wanaccm linalomwunga mkono kwa uamuzi wake huo, ila kwa sasa hatawataja kwa kuhofia kuwa watafukuzwa ndani ya CCM, kutokana na uendeshwaji wa chama hicho ambao umejaa vitisho na kutotaka kusimamia Katiba ya chama chao kwa hivi sasa

Ingawa Mheshimiwa Membe, anaweza hesabika kuwa siyo mwanachama tena wa CCM, kwa kile kinachodaiwa kuwa amefukuzwa uanachama wa CCM, hata hivyo yeye mwenyewe amekaririwa akisema kuwa kikao kilichomfuta uanachama cha Kamati Kuu ya CCM ni batili, kwa kuwa kikao pekee cha kumfukuza yeye uanachama wake kilipaswa kuwa cha Halmashauri Kuu ya CCM, ambacho hadi sasa hakijakaa.

Pamoja na madai yake ya uvunjaji huo wa wazi wa Katiba ya CCM, katika kuvuliwa uanachama wake, Mheshimiwa Membe, kwa ujasiri mkubwa.na bila unafiki, ameendelea kudai kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa CCM, kwa mujibu wa Katiba ya CCM.

Katika hali halisi inaonekana kuwa wapo wanaccm wengi nchini, ambao hawaafiki kwa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini, ya uminywaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kuvifungia vyombo makini mbalimbali vya habari na matumizi ya vyombo vya dola kuminya upinzani, kwa manufaa ya chama cha CCM , kwa hiyo wapo nyuma ya Mheshimiwa Membe, ambaye amejitokeza bila hofu yoyote, pamoja na hatari anayoiona kwake ya utawala huu wa "mkono wa chuma" kwa lengo la kuiokoa nchi yetu, isiendelee kuzama katika utawala huu usiozingatia Katiba ya chama chao wala Katiba ya nchi, ambayo viongozi wakuu wote wa nchi, waliapa kuitii na kuitekeleza kabla hawajaanza utumishi huo wa Umma

Hebu tusubiri tuone kama alivyotuambia yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa lolote linaweza tokea, kati ya hivi sasa hadi mwezi October mwaka huu!
Kama Membe hana support ya vyombo vya dola, anachokifanya ni kutwanga maji kwenye kinu.
 
Huyo amekariri, kwa sababu yeye anamuunga mkono Magufuli kwa kila kitu, basi anadhani kila asiyemkubali Magufuli, basi anapinga kila kitu chake.
Aliposema tuombe badala ya kujifungia ndani kama viongozi wako wa chadema walivyokuwa wanataka ulikuja hapa kumuunga mkono?
 
Aliwafukuza kwa mujibu wa Katiba ya CCM.............

Yaani kwa kutumia vikao halali vilivyoainishwa katika Katiba ya CCM

Sivyo afanyavyo Jiwe, ambaye wala hafuati Katiba ya CCM, wala Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Yeye ni kutembeza ubabe na vitisho kwa kwenda mbele..................
Nyerere alitofautiana na Kambona.ilibidi kambona akimbie nchi.
Sasa ngoja nikupe habari labda huijui, kaka zake wawili na kambona waliwekwa kizuizini na mwishoe wakaachiwa kwa sharti la kuondoka nchini.
Walikuwa wafanyakazi wa umma lakini walifukuzwa kazi.
Ugomvi wa kambona na Nyerere uliwagharimu mpaka ndugu zake
 
Aliposema tuombe badala ya kujifungia ndani kama viongozi wako wa chadema walivyokuwa wanataka ulikuja hapa kumuunga mkono?

Ninajitambua vizuri sana, tena kwenye hiyo post nilisema kabisa, mimi simuungi mkono Magufuli kwenye mambo mengi, ila kwa hilo la kugomea lockdown yuko sahihi. Sina shaka na post hiyo, na uzuri hiyo post iko huku huku. Mimi sio bendera fuata upepo.
 
Sawa..
 
Una maoni gani kuhusu hili la Membe kubwata tu mitandaoni, wakati anajua fomu zinapopatikana ila haendi kuchukua?
 
Me kwa mtizamo wangu:;
kama huyo "kachero mbobezi," alishindwa kupata uraisi kipindi cha "ndugu" yake.ije iwe sasa yupo nje ya mfumo!!!!!!😳.mfa maji haishiwi kutapatapa.
sidhani hata atatokaje huko mtama hadi dodoma kuchukua fomu(maana njia itakua imatapakaaa magogo).Na ajiadhae kuigharimu familia na ndugu na hao jamaa zake sita baada ya hizi mbwembwe zake kugonga mwamba.Hakika atajuta kwa anachokifanya kwa sasa.
 
Hawajui

Back
Top Bottom