Mbona Magufuli qliposema tuombe kwa ajili ya janga la corona ulimbeza?Wewe unawaza kibinadamu na Mungu ana mipango yake........
Lisilowezekana kwa binadamu, linawezekana kirahisi sana kwa Mungu wetu Mkuu kushinda vitu vyote
Acha kujidanganyaBado.. kikao kilichomfukuza ni batili kwa mujibu wa katiba, hivyo bado ni mwanachama hai
Siasa za Nyerere umezisoma ila hukuwapo..
Ni worse than this.... ila woga ulitawala.
Karatasi ya kura ilikuwa picha na kivuli....
Hapana... hapana mwingine zaidi yake
Ndio... tumemkubali anafaa aongoze milele
Sasa yeye mwenyewe kasema haina mamlaka hiyo, kwa hiyo hajafukuzwa, yeye kwa kutumia haki na ubobezi wake akachukue fomu.Hapana
Hajafukuzwa na mkutano Mkuu wala Halmashauri Kuu, bali ni hiyo Kamati Kuu ambayo katika utawala huu wa awamu ya tano "inajimwambafai" na kujona yenyewe ni sawasawa na mungu mtu
Crimea
Nani alimbeza?
Katika mambo machache sana ambayo nimewahi kumwuunga mkono Rais Magufuli ni kwa uamuzi wake wa kulitaka Taifa tumwombe Mungu ili atuepushe na janga la corona
Kama Membe hana support ya vyombo vya dola, anachokifanya ni kutwanga maji kwenye kinu.Katika moja ya hotuba zake muhimu kwa nchi hii wakati wa uhai wake Mwalimu Nyerere aliwahi kutoa utabiri kuwa upinzani wa dhati nchini utatoka ndani ya CCM
Kutokana na kujitokeza kwa mwanasiasa, Bernard Membe kudai kuwa amepania kuchukua fomu ya kugombea Urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, ndiko kunakonifanya nione kuwa utabiri wa Mwalimu Nyerere unaweza kuanza kutimia katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu
Kwa maelezo anayotupa yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa amepania kugombea nafasi ya Urais kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka huu, kwa tiketi ya CCM, tena akiendelea kusisitiza kuwa Kuna kundi kubwa sana la wanaccm linalomwunga mkono kwa uamuzi wake huo, ila kwa sasa hatawataja kwa kuhofia kuwa watafukuzwa ndani ya CCM, kutokana na uendeshwaji wa chama hicho ambao umejaa vitisho na kutotaka kusimamia Katiba ya chama chao kwa hivi sasa
Ingawa Mheshimiwa Membe, anaweza hesabika kuwa siyo mwanachama tena wa CCM, kwa kile kinachodaiwa kuwa amefukuzwa uanachama wa CCM, hata hivyo yeye mwenyewe amekaririwa akisema kuwa kikao kilichomfuta uanachama cha Kamati Kuu ya CCM ni batili, kwa kuwa kikao pekee cha kumfukuza yeye uanachama wake kilipaswa kuwa cha Halmashauri Kuu ya CCM, ambacho hadi sasa hakijakaa.
Pamoja na madai yake ya uvunjaji huo wa wazi wa Katiba ya CCM, katika kuvuliwa uanachama wake, Mheshimiwa Membe, kwa ujasiri mkubwa.na bila unafiki, ameendelea kudai kuwa yeye bado ni mwanachama halali wa CCM, kwa mujibu wa Katiba ya CCM.
Katika hali halisi inaonekana kuwa wapo wanaccm wengi nchini, ambao hawaafiki kwa mambo yanavyoendeshwa hapa nchini, ya uminywaji wa haki za binadamu, ukandamizaji wa demokrasia, kuvifungia vyombo makini mbalimbali vya habari na matumizi ya vyombo vya dola kuminya upinzani, kwa manufaa ya chama cha CCM , kwa hiyo wapo nyuma ya Mheshimiwa Membe, ambaye amejitokeza bila hofu yoyote, pamoja na hatari anayoiona kwake ya utawala huu wa "mkono wa chuma" kwa lengo la kuiokoa nchi yetu, isiendelee kuzama katika utawala huu usiozingatia Katiba ya chama chao wala Katiba ya nchi, ambayo viongozi wakuu wote wa nchi, waliapa kuitii na kuitekeleza kabla hawajaanza utumishi huo wa Umma
Hebu tusubiri tuone kama alivyotuambia yeye mwenyewe, Bernard Membe, kuwa lolote linaweza tokea, kati ya hivi sasa hadi mwezi October mwaka huu!
Nipe tofauti ya kimantiki kati ya utawala wa Nyerere na huu.
Aliposema tuombe badala ya kujifungia ndani kama viongozi wako wa chadema walivyokuwa wanataka ulikuja hapa kumuunga mkono?Huyo amekariri, kwa sababu yeye anamuunga mkono Magufuli kwa kila kitu, basi anadhani kila asiyemkubali Magufuli, basi anapinga kila kitu chake.
Nyerere alitofautiana na Kambona.ilibidi kambona akimbie nchi.Aliwafukuza kwa mujibu wa Katiba ya CCM.............
Yaani kwa kutumia vikao halali vilivyoainishwa katika Katiba ya CCM
Sivyo afanyavyo Jiwe, ambaye wala hafuati Katiba ya CCM, wala Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Yeye ni kutembeza ubabe na vitisho kwa kwenda mbele..................
Nyerere alikuwa mkono wa chuma....
Jifunze zaidi...
Unavyo visikia ni vitamu tu na nukuu zake nzuri
Aliposema tuombe badala ya kujifungia ndani kama viongozi wako wa chadema walivyokuwa wanataka ulikuja hapa kumuunga mkono?
Sawa..Ninajitambua vizuri sana, tena kwenye hiyo post nilisema kabisa, mimi simuungi mkono Magufuli kwenye mambo mengi, ila kwa hilo la kugomea lockdown yuko sahihi. Sina shaka na post hiyo, na uzuri hiyo post iko huku huku. Mimi sio bendera fuata upepo.
Una maoni gani kuhusu hili la Membe kubwata tu mitandaoni, wakati anajua fomu zinapopatikana ila haendi kuchukua?Ninajitambua vizuri sana, tena kwenye hiyo post nilisema kabisa, mimi simuungi mkono Magufuli kwenye mambo mengi, ila kwa hilo la kugomea lockdown yuko sahihi. Sina shaka na post hiyo, na uzuri hiyo post iko huku huku. Mimi sio bendera fuata upepo.
Nyerere alitofautiana na Kambona.ilibidi kambona akimbie nchi.
Sasa ngoja nikupe habari labda huijui, kaka zake wawili na kambona waliwekwa kizuizini na mwishoe wakaachiwa kwa sharti la kuondoka nchini.
Walikuwa wafanyakazi wa umma lakini walifukuzwa kazi.
Ugomvi wa kambona na Nyerere uliwagharimu mpaka ndugu zake
Nyerere alihakikisha hakuna damu ya ukoo wa kambona inabaki TzHawajui
Nyerere alihakikisha hakuna damu ya ukoo wa kambona inabaki Tz
Shida ya vijana wa sasa wanajua upande mmoja wa NyerereAnakufukuza TZ kisha anapiga simu nchi kibao wasikupokee wala kukupa kazi[emoji3]